Ufisadi wa Nyumba za Serikali

1. Mkuu siwezi kukusaidia hasira zako against serikali na CCM, mimi sio rais au mwenyekiti wa CCM, inaonekana kuwa maswali yako mengi yanahitaji kujibiwa na hao au bunge, laini sio hapa JF. Vipi ukienda huko serikalini wakakupa data za jinsi walivyoziuza, mimi ninachojua ni kuwa ninawafahamu wananchi wengi sana hasa toka serikalini ambao bila ya kuuziwa hizo nyumba wasingekuwa na nyumba, kwa hiyo hapa mwenye akili ataamua propaganda na uongo uko wapi.

2. Msimamo wangu unaeleweka hapa, kuhisia na taifa letu, CCM, na upinzani, sina haja ya kurudia rudia mkuu besides hiyo personal attack ambayo nimeshasema kuwa ni nje ya sheria za JF, kwa sababu dataz nilizonazo ni kuwa hata wewe umenunua moja ya hizo nyumba za serikali, na hufanyi kazi serikalini je ni kweli mkuu since unaonekana kupenmda sana personal attacks?

3. CRDB na TANESCO, ni mashirika na sio maazimio ya taifa, tunaweza kuishi bila maazimio lakini sio bila benki au shirika la umeme, vipi mkuu yaaani tuanze tena kuelimishana na haya mambo madogo madogo tean huku kwenye uwanja mzito wa Jambo Forums?
 
Hiki ni kipindi pekee cha vugu vugu la kuhanika ufisadi. Hivi mtumishi wa serikali anapoagiza nje na kuuza dawa kwa wananchi za kuhatarisha maisha ya wanawake wakati wa kujifungua , eti kwa kuwa kapewa dau kubwa toka kwa Mhindi(mtengenezaji), huo ni ufisadi au ufirauni?
Mambo haya yanafanyika Medical Stores Department (MSD). Krugenzi ya ununuzi imekuwa inafanya mambo yasiyo ya kibinadamu kwa Watazania, kwa kuingia mikataba yenye maslahi yao tu, na hivyo kupelekea upungufu mkubwa wa dawa katika Zahanati na vituo vya afya. Ni asilimia 60% tu upatikana kwa wananchi na si kwa wakati muafaka.
Mkurugenzi Mkuu ambaye alipatiwa kazi hiyo akitokea Marekani ambako aliishi kwa miaka mingi, hana ufahamu mzuri juu ya shughuli zote za MSD, na hivyo anapodanganywa chochote hawezi kujinasua. Amekubali ushauri mwingi potofu, na hivo manunuzi mengi yanafanywa kwa matakwa ya mkurugenzi wa ununuzi na maofisa wake! Director General(DG) wa MSD ambaye ni mototo wa aliyekuwa IGP, Phillemon Mgaya alibebwa sana na fisadi wa kimataifa Mh. Edward Lowasa( Lowasa ni rafiki wa karibu wa Phillemon Mgaya) ili kuogezewa mkataba wa miaka miwili tangia Januari 2008.
Manuanuzi ya ajabu yaliyofanyika:
1. Maji ya uchungu(Oxytocin Injection) ambayo ni dawa ya kuongeza uchungu kwa kinamama wakati wa kujifungua, ilinunuliwa kwa wingi na ki maajabu toka India kwa Vital Healthcare(mojawapo ya batch ni V7137). Zilinunuliwa container 3. Dawa hii hivi sasa ni sumu, maana zimetunzwa kwenye joto la kawaida la 30oC badala ya 2-8oC, hii ni kutokana na kwamba MSD ina uwezo wa kutunza vitu katika ubaridi si zaidi ya robo container. Hata hivyo wafisadi wa krugenzi ya ununuzi walimshauri Vital healthcare afute (kwa mark pen) kwenye kasha la nje, maagizo juu ya utunzaji katika ubaridi. Dawa hizi sasa hivi zinauzwa kwa vituo vyote vya serikali, zinatunzwa katika joto la Dar, ila chupa za ndani zinaonyesha mahitaji kamili ya joto la 2-8oC. Ubadhilifu huu ulimwingizia mkurugenzi wa ununuzi dolla za marekani 27,000.
2. Mwishoni mwa Mwaka jana zilinunuliwa container 150 za futi 40 za maji ya kuwawekea wagonjwa mwilini. Ujazo huu unazidi uwezo wa MSD kutunza mizigo hii kwa asilimia 100, na unazidi mahitaji ya nchi kwa miaka mine.Maji haya yalikaa juani kwenye ma container kwa miezi kadhaa baada ya bohari zote kujaa sana na mengine yalilazimishwa kwenda kanda zote za MSD bila mafanikio.Inakisiwa maji haya yataisha mwaka 2010, ingawaje muda wake wa kuisha matumizi ni 2009. Fununu zilizopo ni kwamba ufirauni huu ulifanywa baada ya kampuni inayotengeneza maji hayo kutoa dau la dolla za marekani 120,000 kwa mkurugenzi na ofisa wa ununuzi. Mwenyekiti wa MSD tender bodi ambayye si mtaaluma kabisa wa madawa au manunuzi yalimpita pembeni.
3. Madawa ya kupunguza makali ya virus ya ukimwi(ARVs imekuwa chanagmoto mpya kwa DG na MSD. Mpaka leo hii DG ajui kwamba kukosekana kwa dawa hizi ni kazi ya ufirauni wa krugenzi ya ununuzi . Dawa hizi zimepungua sana tangia November 2007, hadi leo hii, Global Fund na PEPFAR wanajua fika kinachotokea MSD , ila DG haelewi kuwa anaingizwa mtatani. Tender na mikataba vinatolewa kwa watu waliokwisha jijenga kwa Krugenzi ya Ununuzi. Mikataba ikishatolewa na maofisa uchukua chao, na kwaida mtu akisha kupa ongo ataleta dawa kwa wakati anapotaka na quality anayotaka. Sababu hiyo imesababisha dawa kutokuja kwa wakati. Imefikia wakati wanapigwa vita vikali sana watengenezaji wa dawu hizi wa hapa nchi wasiuze dawa zao katika soko la nchi hii. Mfano mzuri ni Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical industries (TPI) ambacho licha ya kupewa changamoto na serikali kuanza kuzalisha dawa hizi hapa nchini ili kuuwanusuru wananchi, kimekuwa kikiwekewa vikwazzo vingi sana na krugenzi ya ununzi.
Je tutafika kama afya ya mtu inawekwa rehani?
 
Bin Maryam alizungumzia jambo moja la msingi lakini hakuna aliye'pick up on it.'

Cha msingi hapa ni dhana nzima ya serikali kutoa nyumba kwa wafanyakazi wake? Hii ni sahihi kweli?

Na wakati wanatoa hizo nyumba, wangapi waliofaidi hiyo huduma? Kama ni sera ya serikali palifanyika jitihada gani kuhakikisha kuwa wale wote wanaostahili kupewa nyumba walipewa nyumba? Maana wakuu kukaa mahotelini kwa kukosa nyumba hakukuanza leo. Nakumbuka kabla ya kuuzwa hizo nyumba palikuwa na malalamiko mengi kuwa wanaopewa hizo nyumba ni vidosho vya wakubwa. Matatizo kwenye hizo nyumba hayakuanzia kuuzwa kwake.

Haya mengine ni ya utekelezaji. Naamini kuwa ungekuwepo utaratibu mzuri na wa wazi yote haya yasingetokea. Tamaa za watu ziliingia kwenye mradi na kuuchafua. kama tunaamini kuwa hii ni sera sahihi tunaishauri nini serikali ili iweze kuendelea kuwapangisha watu kwenye nyumba. Sio nyumba zote zilizouuzwa na uwezo wa kujenga nyingine upo, ili mradi pawe na nia.
 


...........Daaahhhh..........anyway karibu sana JF pntimba
sijui nianzie wapi na hayo yako hapo juu........ngoja niendelee kutafakari.....maana huuu moshi si wa kawaida.....pengine inabidi uanzishiwe mada yake kabisaaa..........UBADHIRIFU wa MSD
 

Sio uongo huwezi kuondoa usongo nilionao kwa hii sirikali ya CCM. Lakini wewe kama mtetezi wao mkuu nilitegemea utakuwa na ushahidi wa hayo unayoongea. Lakini inaelekea unaongelea kutokea hewani tu.


Nashukuru kwa kuniongezea nyumba nilizonazo, lakini kama ungejibu hoja kwa hoja ingesaidia zaidi kuliko nyumba hewa. Narudia tena, Watanzania hawashindwi kuitumikia nchi yao vema kama wafanyavyo nje, na kutatua matatizo kama hayo yaliyokuwepo kwenye nyumba za serikali, tatizo ni siasa na uongozi mbaya wa CCM ndio unaoimaliza nchi.
 

Nina imani kuwa ufanisi unatokana na watu kufanya kile walichotumwa kufanya. Idara za serikali zishughulikie mambo yalioanzisha idara hizo. Kwa mtaji huo, katika posti zangu zilizopita nilisema kuwa uuzaji wa nyumba ni sahihi. Kwa mfano wizara ya mambo ya nje ishughulikie kazi zake na sio wapi wafanyakazi wake watakaa. Hilo ni suala la kipato cha mfanyakazi na soko la nyumba. Kwa mtaji huu I DON'T CARE nani aliyepata hizo nyumba, ninachoangalia ni kuwa serikali inaachana na kufanya kazi ambazo sio zake.

Na kuhusu mafanikio ya China, tusiangalie mafanikio yao na bila kuangalia historia yao.

Unapofanya mabadiliko makubwa katika jamii unachofanya ni kuleta CHAOS katika mfumo ulipo. Na hili mafanikio yapatikane ni lazima stabilization iwepo na hiyo ndio tofauti kubwa kati yetu na China. Viongozi wa China kwa uchache walikuwa tayari kusimamia nadharia zao. Kwa upande mwingine viongozi wetu wanaanza na sherehe kubwa na baadaye hawaonekani kuwa wako serious na kile wanachofanya. Siasa zao nyingi ni rhetoric za ku-lament ubepari na ukoloni na wanaona sifa kufanya kinyume na kile alichofanya mkoloni bila kuangalia mafanikio ya yale wanayofanya.
 
1. Siku zote niko open minded na very positive person, siwezi kuja hapa kila siku na machungu tuu na kulaumu kila mtu mwingine lakini not myself, viongozi walioko kwenye power wamechaguliwa na wananchi, hawakujiweka tu wenyewe, hilo ninaliheshimu sana, na ni kuheshimu demokrasia pia, CCM haikujiweka kwenye power, imechaguliwa na wananchi, sasa ninatakiwa, kwanza kuwa na heshima nao, na pia kuwa na Constructive Criticism, kwa mfano mimi na baadhi ya wananchi hapa tuliilalia macho Richimonduli, mpaka mwisho na kuona Waziri Mkuu na mawaziri wawili tena marafiki wa karibu na rais wakijiuzulu, hata bongo nzima JF tumepata credit kwa hilo kwamba ndiyo chanzo cha the whole saga, sasa hatuwezi kuanza kujishushia heshima yetu hapa kwa kuanza kukurupuka ovyo na attacks bila facts au angalau dataz, mkuu hii JF sasa ni chombo muhimu sana cha haabari za siasa ya nchi yetu, kwa hiyo ni lazima tuwe makini na tunachosema, sio kuropoka ropoka ovyo bila sababu, yes ninaona jinsi tulivyoingiliwa sasa hapa JF, lakini hawatadumu maana the originals tuko macho sana na tunajua kinachoendelea! JF haikufika hapa mkuu kwa kurusha unfounded shutuma kila siku tena nonstop kwa CCM na serikali, no mkuu! Hapa mkuu tunaziangalia ishus kwa makini na kwa undani sana, kwa hiyo hili la kuuzwa kwa nyumba za serikali I am sorry kuwa sikubaliani na hizi shutuma kwa sababu kuna wananchi wengi sana wafanyakazi wa serikali ninaowafahamu wamenufaika nao, na ninajua kua wachache pia walionufaika kwa ujanja, lakini percent yapo ndogo sana kiasi kwamba I am willing to live with it.

2. Uongozi mbaya wa CCM haupo, ila kuna viongozi wachache wasiokuwa na uwezo wa kuongoza ndani ya CCM na serikali, now that has nothing to do na CCM collectivelly, unasema tatizo ni siasa za CCM halafu unasema CRDB inafanya vizuri, sasa inafanyaje vizuri kwenye mazingira ya siasa hizo hizo mbovu za CCM?

CCM collectivelly, ingekuwa na siasa mbovu Lowassa, Karamagi, Msabaha, wasingejiuzulu, taifa letu lisingefikia lilipo leo, jamani hapa bongo sio majuu naona wengi sana tunachanganya hilo, na kufikiri bongo tunatakiwa ku-operate kama majuu, no! hii ni bongo mambo yetu kuanzia uchaguzi wa viongozi mpaka maadili yetu kiuongozi ni ya ki-bongo bongo, kwa hiyo tusitegemee mabadiliko yatatokea kama umeme, hapana inatakiwa sacrifice wakuu na inapaswa kuwa clear kuwa hakuna wa kumfanyia mwingine ila ni sisi wenyewe kujiingiza huko kwenye siasa.

Kwa hiyo mkuu mimi sio mtetezi wa CCM na serikali yake, mimi mwannchi wa bongo mwenye upeo wa kuchanganua na kulinganua siasa ya nchi yangu in a positive way, na with an open mind, na in the process understanding kwamba bongo sio Ulaya, pia kwamba wa-Tanzania baada ya kuwa under one party rule kwa muda mrefu sana na kutojua anything kuhusu uwajibikaji, itachukua muda sana kupata mabadiliko tena kwenye hilo niko very realistic kwamba huenda it will happen kwenye another generation, lakini sio hii yetu, na kwamba sio kila kiongozi wetu ni fisadi, kwamba sio kila maamuzi ya serikali yana walakini wa ufisadi, na kwamba tatizo sio CCM, bali ni kwanza sisi wananchi halafu ndio viongozi wetu,

Na kama huamini kuwa sisi wananchi pia ni tatizo kubwa kwa taifa letu kisiasa, hebu pitia threads zote hapa Jambo Forums uone!

Ahsante Mkuu.
 
1. Mkuu Maryam, maneno yako ni mazito na ni very educating, keep it up.

2. Mkuu Pintimba, ingawa hiii inatakiwa kuwa na topic yake, lakini nitaigusa anyways,

(a). Oscar Mgaya, hajakaa muda mrefu sana USA kama ulivyosema, alienda huko kati kati ya the 90s, kusoma degree ya kwanza na ya pili, na alipomaliza alifanya kazi kidogo na kurudi bongo, sasa hii haiwezi in anyway or sense kuwa amesahau mienendo na mzingara yetu ya bongo, haya majina kabla hamjayarusha kuweni makini angalau kidogo, waliomuajiri si walihitaji qualifications ambazo alizonyesha

(b). Kwamba hana uzoefu au uelewa, I mean somewheree unajichanganya, maana unasema kuwa hana uzoefu na uelewa wa MSD, halafu unasema kua anashauriwa na somebody else, je huyo anyemshauri naye hana uzoefu na ni nani huko MSD? Je ni nini uzoefu wa hili shirika kuhusiana na uagizaji wa hayo madawa? ni shirika la nani anyways?

3. Una-raise some very interesting ishus, ambazo tunahitaji kuzi-examine kwa makini kabla ya kutoa hukumu, lakini thanks you a lot kwa hizi dataz.
 
Wakuu,
Issue ya MSD tumeitengenezea thread yake inayoitwa;

Lowassa tena Yumo: Ufisadi Madawa MSD

Naomba tuendelee na hili la Nyumba za serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…