Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
18,585
Reaction score
16,780
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..

Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,
Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!

Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!

Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..

==================================================================================================
Majibu ya SAA YA UFUFUO NA UZIMA
==================================================================================================
- Ndugu wana JF
- Nawasalimu kwa lugha, kabila na mitindo yenu pia

- Ikumbukwa mnamo Jumatatu ya October 14[SUP]th[/SUP], mwaka huu kama siku 27 zilizo pita, -saa kumi na dk 25, Kupitia jukwaa hili hili ndugu yetu mpendwa kiwatengu -alituletea maada hapa inayosema Ufufuaji wa Misukule!! Inatofauti gani na Maigizo?.-

- Maada yake hii ilionekana kupenya miongoni mwa wanajamvi wengi, kiasi cha watazamaji 4,444 na zaidi ya wachangiaji 221, waliojaza zaidi ya kurasa 12 za jamvi hili. Nawapongeza Moderators kwa kuruhusu uwazi huu wa taarifa ndani ya Jukwaa hili Nguli la kifikra na ni imani yangu kwamba basi Mtatoa Muda mwingine huu kwa ajili ya Saa ya Ufufuo na Uzima kufafanua baadhi ya hoja lakini pia kujibu maswali mbalimbali kwa sababu Saa ya Ufufuo na Uzima Tupo na hata siku moja hatujawahi kuwa na kigugumizi kumjibu kila mtu mwenye wazo, dukuduku au swali juu ha huduma yetu.maana-

- 1Petro 3: 15 -Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.

- Kwa neno hilo basi Saa ya Ufufuo na Uzima tukaona hapana shaka ni vema basi tukatafuta muda muafaka ingawa kidogo tuweze kuelezea na kujibu kila anaye taka kuuliza Juu ya Tumaini la Imani yetu wa dini, kabila na dhehebu lolote. Ingwawa Muda wetu ni Kiduchu mno, Tumekuwa na Mikutano mikubwa yenye ishara kubwa za miujiza iliyoanzia Mjini Arusha tarehe septemba 27 hadi Octoba 10 kwenye viwanja vya wazi vya Relini, UNGA LIMITED. Nikupe picha ZA -mkutano wetu wa Arusha,-

- -View attachment 120505 View attachment 120506

- Ambapo watu wengi walifunguliwa, Misukule kurudishwa na Uponyaji mkubwa wa magonjwa kiasi wakazi wengi wa Arusha hawakupenda huduma hii iondoke Mkoani mwao Mtu mmoja mjini hapo mwenye ekari zaidi ya nane akatoa eneo lake bure ili Huduma hii iendelee jijini Arusha maeneo ya Engosheraton, Sokini 1, Unga limited ambapo mpaka sasa huduma inaendelea hapo.-
- Opereshini ya Saa ya Ufufuo na Uzimaikaendelea mjini Moshi kwenye Viwanja vya wazi vya Mashujaa, October 20-27 Moshi nikupe pia picha mbili za mkutano wa Moshi..
View attachment 120508 View attachment 120511

--
- ..
- '
- Maajabu yalizidi mno hapo Moshi, maelefu ya watu waliyashuhudia maajabu hayo lakini lililotia fora ni kurudishwa kwa misukule ambao waliwekwa strategy kwa ajili ya Kukamua ng'ombe wakati wa kurudi machungani au asubuhi, misukule hao wanasema wao kazi yao ilikuwa wakati masaa ya jioni ng'ombe wanakaribia kukamuliwa wao bila kuonekana na binaadam wa kawaida huenda kuiba maziwa kwa kuwakamua ng'ombe hao. Na mwenye maziwa akija kukamua ng'ombe anaambulia patupu iwe jioni au asubuhi na kuwalaumu watunza ng'ombe labda wameruhusu ndama akanyonya kumbe misukule weshaiba. Sio lengo langu kuongelea shuhuda tele za misukule hao lakini mkutano ulifurika mno kiasi Yule Mangi mashuhuri wa Kilimanjaro, aliyegombea Kiti cha urais Kipindi kile na mwalimu Nyerere nadhani tunaakiba ya Historia hiyo akajitolea Jengo kubwa sana ambalo hapo awali lilikuwa Godown kubwa mno maeneo ya Pasua, Moshi Mjini karibu na machinjio kuu ya Mji, -ambapo umati wa watu ulimiminika baada ya tarehe za mkutano kuisha hapo uwanjani na kuelekea Ndani ya jengo hilo ambapo -Huduma inaendelea hapo hadi sasa.-

--
- Hatujaishia hapo, sasa Saa ya Ufufuo na Uzima Tunaikabili Tanga kuanzia tarehe 24[SUP]th[/SUP] mwezi huu wa 11, tutakuwa Tanga Viwanja vya Tangamano hapo mjini. Tanga sio mbali kila mwenye dukuduku na maswali tafadhali aje ajionee mwenyewe. Aione misukule na ikiwezekana aihoji apendavyo. Ikumbukwe tanga ni mojawapo ya miji mkongwe kuliko yote katika Historia ya nchi yetu ukiacha Zanzibar, Tanga iliundwa mji tokea 1891, Ikumbukwe jina Tanganyika limetokana na kata Moja Iliyoko mji wa Tanga inayoitwa Tanganyika, Tulipaki msafara na kupiga -picha Eneo hilo tafadhali niionyeshe..
View attachment 120513

--
- Hivyo kwenye historia ya nchi hii -Tanga ina uzito mKubwa lakini Uchawi na ushirikina huupoteza -mji kwenye mstari wa mafanikio. Tembea yetu Tanga tumeona watoto wadogo machizi wengi tukiuliza sababu wakaazi wanasema wazazi wao wamewafanya hivyo. Lakini tunaiombea Tanga na tunaamini Kuanzia tarehe 24 mkutano utapoanza Tanga watu hawa watafunguliwa na naomba stay tuned kusikia kile Mungu atachofanya ndani ya Mji huu. Jambo hili ni chanda cha Mungu ni la wazi na kila mtu aweke bidii kulijua.-

--
- Ahsante kwa kunivumilia kusoma Mukhtasari wa Shughuli za Saa ya Ufufuo na Uzima si lengo langu hasa ila ningependa kukushirikisha na nashukuru sana kwa Muda wako kuwa nami hadi sasa . Wewe ni wa thamani Kuu. Labda sasa nieleze hasa kile kiini cha Hoja ambacho kilikuwa lengo la Sred.. Misukule.. -why misukule..-

--
- Kimsingi Misukule Kila mtu anajua ni nini, ama kwa tafsiri ngeni au mpya sote tunajua msukule ni nini atayesema hajui msukule ni nini huyu atakuwa ni mbishi na sidhani kama tuna nafasi na wabishi. Lakini kwa tafsiri nyepesi msukule ni Roho zinazotangatanga, zinazoishi nje ya miili au ndani ya miili mingine. Mwanadamu ni nini, mwanadamu ni Roho inayokaa ndani ya nyumba na nyumba inaitwa Mwili. Mwanadamu anaweza kuwa ndani ya mwili au nje ya mwili embu ona kweli hii kwenye biblia-
--
- 1thesalonike5:23 -Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
- -
- Tunaelewa kwamba mwanadamu ana mwili, nafsi na roho..lakini Roho ndio itiayo uzima mwili haufai kitu. Basi kifo ni nini, Kifo ni Utengano kati ya Roho na mwili. Roho inaondoka mtu akifa inaenda pahala na the body decay. Nadhani kweli hii wote tunaifaham. Niseme wazi tu kwamba watu wote kufa tutakufa, penda usipende na kufa kwetu ni faida na Kuishi ni Kristo. Lakini kuna neno jingine la Mungu embu litafakari kutoka Kwenye Kitabu cha ufunuo uone jambo hili la ajabu kabisa..
Ufunuo 18:

11 -Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;-
-12 -bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito -chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, -na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha -pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha -chuma, na cha marimari;-
-13 -na mdalasini, na iliki, na uvumba, -na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, -na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho -za wanadamu.

--
- Tunagundua kumbe kuna biashara wajanja huwa wanafanya kimashetani, na moja ya bidhaa hizo ni Miili na Roho zetu wanadamu. Kumbe na Roho za wanadam is among commodities deals within those people thought themselves clever. Kumbe kuna watu wameibiwa Roho, wameibiwa miili Biblia inasema. Ndio maana basi ukaja ufunuo kwenye Isaya 42:22 -Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na -kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; -wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana -asemaye, Rudisha.

--

- Kwa maana kama hiyo basi saa ya Ufufuo na Uzima, na kila mwenye Moyo huu tunaungana kwa kazi hii ya Kuwarudisha haoo walioibiwa. Baadhi ya wachungaji wa Moshi na Arusha nao wameanza kurudisha misukule na shuhuda ni Nyingi sana.-

--
- Basicall Misukule iko ya aina nyingi lakini leo niongelee tatu tu wa sentensi fupi nisikuchoshe
--
- 1:- Watu ambao -tunadhani wamekufa kwa mapenzi ya Mungu kumbe wamechukuliwa kiuchawi. Tunazika -migomba, vinu na madude mengine huku tukiwa tumechezewa macho. Ni kama -mazingaombwe vile, mtu anachoma mkuki kichwani na anatembea akidai yeye ni profesa bingwapotea -na ataonyesha mazingaombwe hayo sehemu fulani kwa kiingilio lakini -kibaolojia jambo hilo haliwezekani. Ni kuchezea macho watu tu ambacho wachawi -wanafanya na tukiomba wanadamu wenzetu hawa wanarudi. Zipo dalili tele utaziona -msibani, kama ndugu yako amechukuliwa kichawi. mfano -jeneza zito kuliko kawaida, gari kukataa kwenda, mwili wa marehemu -mreefu sana kuliko kawaida na mauzauza mengi msibani. Ukiona hali kama hiyo -usizembee ni kuomba na kumwita mtu huyo kwa jina lake, Yesu alimwita Lazaro 'NJOOOO -HUKU NJE" na wewe ita -Njooo kwa jina La Yesu na unaweza kushangaa kitachotokea hutaamini. Watu hawa wapo na wanashuhudia waziwazi. Sio -kwamba hawafahamiki kama wadau wengi walivyosema wana familia zao na familia -zao zimetoa ushahidi wa wazi wazi.

--
- 2;- Kuna watu huchukuliwa wazimawazima, utakuta ndani ya jamii mtu anapotea. Mjomba alipoteaga zamani, baba aliondoka hakurudi tena, mwanangu mwaka wa nane aliondokaga nyumbani hatujui alipo, ni watu wengi sana wamekumbwa na kadhia hii, jamii haina majibu na jambo hili. Watu hawa wapo, wamefichwa kwenye majumba ya watu, wanabeba maboksi, wanakata miwa, wanafanya kazi za mahotelini na nyinginezo, wakiitwa wanarudi na tunazo shuhuda nyingi za audio na dvd za watu hawa.

--
- 3:- Aina hii ya Tatu ni watu wengi sana, Kimwili tunao ila Kiroho hawapo. mtu anachukuliwa roho na mwili unabakia. Mwili ule unapandiwa roho nyingine ya shetani na mtu huyo anaendelea kufanya operation za maisha kama kawaida akipretend ni yeye wa asili kumbe ni maroho ya kishetani. Hii ni common sana kwenye jamii zetu watu wengi ni misukule lakini barabarani wanakatiza na kazi wanafanya. Unaweza kuoa au kuolewa na msukule bila kujua na hapo ndippo utapokoma kwenye ndoa. Nikupe baadhi ya tabia ya misukule hawa.

- a) - Mume msukule:- -Ana tabia ya ukali uliopitiliza, hawezi kabisa kutembea na mkewe kwa -njia ya kawaida lazima iwe kinyume na maumbile, lazima atembeee na -mwanamke yeyote ndani ya nyumba yake iwe housegirl au ndugu yeyote ndani -ya nyumba yake (si wote wanaotembea na h/g ni misukule ila ishara -kwa misukule kuna dalili ambazo siwezi sisema hapa utazigundua kwa aliye -tembea na msukule). hawezi kuwazia maendeleo zaidi ya pombe, kipigo na tabia ambazo mwanadamu wa kawaida hawezi kuzifanya

- b) - Mke msukule:- ni mkorofi, mgomvi, anatokwa na damu sana, anaota anapaa au kula nyama usiku, magonjwa mwilini hayaishi kila siku ni mgonjwa madawa na madawa. Ni ngumu kubeba mimba na akibeba hutoka.-

- c) - Mtoto msukule; unashangaa tu mtoto kawa mjingamjinga, masomo yalikuwa mazuri la kwanza, pili tatu lakini ghafla ameshuka hadi wa mwisho na wala hana bidii ya kusoma unaweza ukapiga mtoto bure kumbe keshachukuliwa.

- d) - Housegirl msukule:- kifupi hapo ndoa hakuna, watoto wakimwona wanalia sana ila yeye anapretend kuwapenda na ukienda kazini huku nyuma watoto wananyukwa isivyo kawaida. Mchunguze bint yako unaporudi kazini. Na lazima amfanyizie vimbwanga mumeo na kifupi lazima aisambaratishe nyumba.watu wengi -wanayashabikia matukio haya kama ni ya kawaida kwenye jamii, sure i am -telling you hao si binaadamu wa kawaida. wanawake na wanaume wanaojiuza -asilimia kubwa ni misukule, na jambo baya ni kwamba ukitembea tu na -msukule na wewe unachukuliwa.. jichunguze mara baada ya kutembea na mtu -fulani ham ya maisha ilitoweka, bidii ya kazi ilikwisha, unachoka sana -na kulalalala masaa yote, ni mvivu kupindukia.. HAUPO.!!

- e) - Bosi msukule:- kama wewe ni mlolkole siku ukifanya maombi sana basi ofisini utapata matatizo mengi from huyo bosi msukule.
- Kuna category nyingi kwa leo niishie hizo

--
- Watu wote hawa wanarudishwa, na si kwamba hawajulikani, wanajulikana vizuri kabisa kwa jamii zao na jambo hili ni wazi kabisa hata kwenye mikutano yetu huwa tunaweka namba zao za simu kwa mwenye simu ili ampigie na kujiridhisha na kila hoja anayotaka aeleweshwe.-

LAKINI ZAIDI TEMBELEA-
website: UFUFUO NA UZIMA (GCTC)
blogu: -ufufuonauzima.blogspot.com
au jiunge na facebook Group: Ufufuo Crew
au nitumie E-mail: bihagaze@yahoo.co.uk
au piga simu moja kwa moja 0713254210
 
WATU ZAIDI YA 20
WARUDISHWA
KUTOKA KWENYE
MISUKULE HUKO
ARUSHA KWENYE
MKUTANO WA MCH. GWAJIMA. Habari inatoka Gospel Media News
 
Huwa sipendi kuzungumzia mambo ya imani hasa yanayozungumzia habari ya Yesu Kristo. Lakini kwa hili la kufufua watu imenitia mashaka, kuna watu wengi misukule walijitokeza kwenye mkutano wa Gwajima, baadhi wanasema walikufa miaka 15/20 iliyopita, moja akasema ametoka mortuary alikuwa amekufa wiki mbili zilizopita. Kilichonifanya niwe na mashaka ni jinsi waliofufuliwa hawajulikani kwa mtu yeyote. Nilidhani mtu aliyefufuka angesema yeye ni fulani, alikuwa anafanya kazi sehemu fulani, na ndugu zake ni fulani na fulani, ama balozi wake ni fulani na alikuwa anasali kanisa fulani au msikiti fulani. Bahati mbaya hakuna hata moja aliyejitokeza akajitambulisha.

Mimi nadhani Gwajima alikuja na misukule yake kuwadanganya watu. Kama kweli amefufua watu hebu tujiulize hao watu wako wapi kama siyo amewachukua?

Mungu atupatie maarifa na hekima ya kutambua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mkuu Mungi! binafsi nilishtuka sana nilipoona eti Gwajima afufua misukule zaidi ya 20 Arusha..
haya ni maigizo ya jukwaani kabisa na anayafanya bila uoga akidhani watanzania wote akili zetu zinafanana..

Sitaamini kamwe kwenye ufufuo wa aina hii..
Mungu naomba usinitoe katika imani niliyonayo,
inayonifunza katika kuyakabili maisha kwa njia ya halali! kutafuta kwa jasho..

Dah! mkuu watu8 huwa nakumbuka sana hoja yako uliowahi kuitoa sehemu juu ya kuwaamini watu kama kina Gwajima!

Hili la misukule mh! hapana kabisa!!
 
Last edited by a moderator:
Haya maswali tungemuuliza pdidy,maana nae yuko kwenye msafara wa huyo mchungaji atwambie walipo hao misukule,nakumbuka juzi aliweka picha ya msukule mmoja hapa.
 
Kama mtu kafa kwa mapenzi ya Mungu hakuna wa kumfufua lakini kuna watu wanakufa kwa ushirikina hawa kama unaamini kwa jina la YESU wanatoka kwenye hiyo dunia ya misukule.
Hivi vitu vimefanywa hata na waganga wa kienyeji lakini wengine mkaamini lakini kwa YESU mnaona utapeli!
huko kanda ya ziwa ni majuzi mtoto aliyekufa na kuzikwa lakini ameonekana na kuwa gumzo hadi humu JF.
Sikatai ulaghai wa wachungaji wa siku hizi lakini tunapojadili haya tusi limit uwezo wa Mungu (ni kufuru) tukidhani tunaponda uwezo wa wachungaji.
Zungumzieni utapeli wa wachungaji lakini si uwezo wa MUNGU.
 
WATU ZAIDI YA 20
WARUDISHWA
KUTOKA KWENYE
MISUKULE HUKO
ARUSHA KWENYE
MKUTANO WA MCH. GWAJIMA. Habari inatoka Gospel Media News

shida kubwa ya watanzania wengi hawajui maandiko
napia hawamwamini mungu
wamekuwa wachunguzi;
wana roh ya tomazo:
neno la mungu limeweka wazi na ishara hizi zitaambatana na hao wamwamio yesu kwajina la yesu tutafufua wafu;
pia nitoe ufafanizi kidogo sii kweli ukifa nikweli umekufa wengine wanachukuliwa kichawi na kiroh wewe ujafa umeibwa tu
neno linasema watu hawa wamechukuliwa wako kwenye mashimo wala hapana asemae rudisha:
hivyo kazi ya mtu yeyote anaye mwamini kirsto amepewa mamlaka ya kurudisha mateka:
wacheni kucheza na kazi za mungu
 
Huwa sipendi kuzungumzia mambo ya imani hasa yanayozungumzia habari ya Yesu Kristo. Lakini kwa hili la kufufua watu imenitia mashaka, kuna watu wengi misukule walijitokeza kwenye mkutano wa Gwajima, baadhi wanasema walikufa miaka 15/20 iliyopita, moja akasema ametoka mortuary alikuwa amekufa wiki mbili zilizopita. Kilichonifanya niwe na mashaka ni jinsi waliofufuliwa hawajulikani kwa mtu yeyote. Nilidhani mtu aliyefufuka angesema yeye ni fulani, alikuwa anafanya kazi sehemu fulani, na ndugu zake ni fulani na fulani, ama balozi wake ni fulani na alikuwa anasali kanisa fulani au msikiti fulani. Bahati mbaya hakuna hata moja aliyejitokeza akajitambulisha.

Mimi nadhani Gwajima alikuja na misukule yake kuwadanganya watu. Kama kweli amefufua watu hebu tujiulize hao watu wako wapi kama siyo amewachukua?

Mungu atupatie maarifa na hekima ya kutambua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

tuwache kuingiza neno la mungu
kwenye ushabiki usiokuwa na mpango Mungi@kama unakataa kitu kataa kwa neno mimi neno la mungu linaniambia nikimwamini nitafanya zile kazi yesu alikuwa anazifanya tena na kubwa zaidi ya hapo sioni koza kunyanganya mchawi mtu na kuleta kwa yesu
kwani watu wanaopinga tu kwa akilizao ndio mwisho wa akili zao
 
Last edited by a moderator:
Mimi huwa nachokaga na haya mambo. Sijawahi kufika katika hizo ibada ila nachojiuliza hao wanaoitwa misukule inafikaje hapo kwa Gwajima..yaani kama huyo alietoka Mortuary alikuja mwenyewe au? Duuh...
 
Mimi ni Mkatoliki lakini ninayeamini YESU aliyesema kwa imani hata milima itang'oka sembuse haya?
Pondeni wachungaji lakini acheni kulimit uwezo wa Mungu.
Mleta mada ungesema huamini kama wale misukule kweli nisingeshangaa lakini futa kauli ya kutoamini miujiza kwavile huoni kanisani kwako.Mimi kwenye mikutano ya Karistimatic nimeshuhudia miujiza mizito hivyo sishangai uwezo wa Mungu.
 
Mimi huwa nachokaga na haya mambo. Sijawahi kufika katika hizo ibada ila nachojiuliza hao wanaoitwa misukule inafikaje hapo kwa Gwajima..yaani kama huyo alietoka Mortuary alikuja mwenyewe au? Duuh...

mambo haya mungu aliwaficha wenye hekima na akili akawafunulia watoto wadogo
uwezi kuelewa
 
mbona unajichananya?...hujui unachokiandika,yap kuna maigizo ila sio kweli kwamba haiwezejkani kufanyika,Yesu amamwenyewe aliahidi kwamba kazi alizoifanya hata sisi tunaweza kuzifanya na zaidi....so what area you talking about?...vp nyie kwenu hamuwezi fanya?
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..

Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,
Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!

Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!

Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..
 
Mimi huwa nachokaga na haya mambo. Sijawahi kufika katika hizo ibada ila nachojiuliza hao wanaoitwa misukule inafikaje hapo kwa Gwajima..yaani kama huyo alietoka Mortuary alikuja mwenyewe au? Duuh...

Wewe hupaswi kumuamini mchungaji bali amini uweza wa jina la YESU.
Kutokuamini kwenu kuna shangaza mbona mnaamini ulinzi wa majini lakini mkisikia muujiza wa MUNGU doubt kibao na vijisababu visivyoisha.
 
Huwa sipendi kuzungumzia mambo ya imani hasa yanayozungumzia habari ya Yesu Kristo. Lakini kwa hili la kufufua watu imenitia mashaka, kuna watu wengi misukule walijitokeza kwenye mkutano wa Gwajima, baadhi wanasema walikufa miaka 15/20 iliyopita, moja akasema ametoka mortuary alikuwa amekufa wiki mbili zilizopita. Kilichonifanya niwe na mashaka ni jinsi waliofufuliwa hawajulikani kwa mtu yeyote. Nilidhani mtu aliyefufuka angesema yeye ni fulani, alikuwa anafanya kazi sehemu fulani, na ndugu zake ni fulani na fulani, ama balozi wake ni fulani na alikuwa anasali kanisa fulani au msikiti fulani. Bahati mbaya hakuna hata moja aliyejitokeza akajitambulisha.

Mimi nadhani Gwajima alikuja na misukule yake kuwadanganya watu. Kama kweli amefufua watu hebu tujiulize hao watu wako wapi kama siyo amewachukua?

Mungu atupatie maarifa na hekima ya kutambua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

halafu kwa hali ya kawaida tu haiwezekani mtu aliyekufa zamani kiasi hicho afufuliwe bana,tunakumbuka yesu alimfufua lazaro siku ya tatu tena alikuwa tayari ananuka,tunakumbuka elisha alimfufua mtoto wa mwanamke mshunami tena baada ya siku tatu tu,hapo sciense inataka kutueleza alikufa kwa muda mrefu mwili wake hauwezi kurejea kwa sababu utakuwa umekosa chakula kwa muda mrefu,tuache utani kwenye mambo ya Mungu jamani
 
shida kubwa ya watanzania wengi hawajui maandiko
napia hawamwamini mungu
wamekuwa wachunguzi;
wana roh ya tomazo:
neno la mungu limeweka wazi na ishara hizi zitaambatana na hao wamwamio yesu kwajina la yesu tutafufua wafu;
pia nitoe ufafanizi kidogo sii kweli ukifa nikweli umekufa wengine wanachukuliwa kichawi na kiroh wewe ujafa umeibwa tu
neno linasema watu hawa wamechukuliwa wako kwenye mashimo wala hapana asemae rudisha:
hivyo kazi ya mtu yeyote anaye mwamini kirsto amepewa mamlaka ya kurudisha mateka:
wacheni kucheza na kazi za mungu

unazungumziaje issue ya babu wa loliondo?wabongo ndio zao bana kukurupuka halafu kimyaaaaaaaa,mimi natoka Arusha lakini issue ya babu ilinifanya nirudi nyuma na kujiuliza maswali kibao,ndugu zangu walilazimisha nisafiri ili nikale kikombe cha babu,lakini niligoma muda si muda tukasikia story kuhusu babu,haahahaaa,wabongo bana
 
mbona unajichananya?...hujui unachokiandika,yap kuna maigizo ila sio kweli kwamba haiwezejkani kufanyika,Yesu amamwenyewe aliahidi kwamba kazi alizoifanya hata sisi tunaweza kuzifanya na zaidi....so what area you talking about?...vp nyie kwenu hamuwezi fanya?

kuna mengi yakufanya zaidi ya kuigiza na misukule..
Kuna mafundisho mengi sana ambayo watanzania wanayahitaji katika kujikwamua na umaskini..
 
Back
Top Bottom