Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
18,585
Reaction score
16,780
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..

Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,
Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!

Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!

Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..

==================================================================================================
Majibu ya SAA YA UFUFUO NA UZIMA
==================================================================================================
 
WATU ZAIDI YA 20
WARUDISHWA
KUTOKA KWENYE
MISUKULE HUKO
ARUSHA KWENYE
MKUTANO WA MCH. GWAJIMA. Habari inatoka Gospel Media News
 
Huwa sipendi kuzungumzia mambo ya imani hasa yanayozungumzia habari ya Yesu Kristo. Lakini kwa hili la kufufua watu imenitia mashaka, kuna watu wengi misukule walijitokeza kwenye mkutano wa Gwajima, baadhi wanasema walikufa miaka 15/20 iliyopita, moja akasema ametoka mortuary alikuwa amekufa wiki mbili zilizopita. Kilichonifanya niwe na mashaka ni jinsi waliofufuliwa hawajulikani kwa mtu yeyote. Nilidhani mtu aliyefufuka angesema yeye ni fulani, alikuwa anafanya kazi sehemu fulani, na ndugu zake ni fulani na fulani, ama balozi wake ni fulani na alikuwa anasali kanisa fulani au msikiti fulani. Bahati mbaya hakuna hata moja aliyejitokeza akajitambulisha.

Mimi nadhani Gwajima alikuja na misukule yake kuwadanganya watu. Kama kweli amefufua watu hebu tujiulize hao watu wako wapi kama siyo amewachukua?

Mungu atupatie maarifa na hekima ya kutambua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mkuu Mungi! binafsi nilishtuka sana nilipoona eti Gwajima afufua misukule zaidi ya 20 Arusha..
haya ni maigizo ya jukwaani kabisa na anayafanya bila uoga akidhani watanzania wote akili zetu zinafanana..

Sitaamini kamwe kwenye ufufuo wa aina hii..
Mungu naomba usinitoe katika imani niliyonayo,
inayonifunza katika kuyakabili maisha kwa njia ya halali! kutafuta kwa jasho..

Dah! mkuu watu8 huwa nakumbuka sana hoja yako uliowahi kuitoa sehemu juu ya kuwaamini watu kama kina Gwajima!

Hili la misukule mh! hapana kabisa!!
 
Last edited by a moderator:
Haya maswali tungemuuliza pdidy,maana nae yuko kwenye msafara wa huyo mchungaji atwambie walipo hao misukule,nakumbuka juzi aliweka picha ya msukule mmoja hapa.
 
Kama mtu kafa kwa mapenzi ya Mungu hakuna wa kumfufua lakini kuna watu wanakufa kwa ushirikina hawa kama unaamini kwa jina la YESU wanatoka kwenye hiyo dunia ya misukule.
Hivi vitu vimefanywa hata na waganga wa kienyeji lakini wengine mkaamini lakini kwa YESU mnaona utapeli!
huko kanda ya ziwa ni majuzi mtoto aliyekufa na kuzikwa lakini ameonekana na kuwa gumzo hadi humu JF.
Sikatai ulaghai wa wachungaji wa siku hizi lakini tunapojadili haya tusi limit uwezo wa Mungu (ni kufuru) tukidhani tunaponda uwezo wa wachungaji.
Zungumzieni utapeli wa wachungaji lakini si uwezo wa MUNGU.
 
WATU ZAIDI YA 20
WARUDISHWA
KUTOKA KWENYE
MISUKULE HUKO
ARUSHA KWENYE
MKUTANO WA MCH. GWAJIMA. Habari inatoka Gospel Media News

shida kubwa ya watanzania wengi hawajui maandiko
napia hawamwamini mungu
wamekuwa wachunguzi;
wana roh ya tomazo:
neno la mungu limeweka wazi na ishara hizi zitaambatana na hao wamwamio yesu kwajina la yesu tutafufua wafu;
pia nitoe ufafanizi kidogo sii kweli ukifa nikweli umekufa wengine wanachukuliwa kichawi na kiroh wewe ujafa umeibwa tu
neno linasema watu hawa wamechukuliwa wako kwenye mashimo wala hapana asemae rudisha:
hivyo kazi ya mtu yeyote anaye mwamini kirsto amepewa mamlaka ya kurudisha mateka:
wacheni kucheza na kazi za mungu
 

tuwache kuingiza neno la mungu
kwenye ushabiki usiokuwa na mpango Mungi@kama unakataa kitu kataa kwa neno mimi neno la mungu linaniambia nikimwamini nitafanya zile kazi yesu alikuwa anazifanya tena na kubwa zaidi ya hapo sioni koza kunyanganya mchawi mtu na kuleta kwa yesu
kwani watu wanaopinga tu kwa akilizao ndio mwisho wa akili zao
 
Last edited by a moderator:
Mimi huwa nachokaga na haya mambo. Sijawahi kufika katika hizo ibada ila nachojiuliza hao wanaoitwa misukule inafikaje hapo kwa Gwajima..yaani kama huyo alietoka Mortuary alikuja mwenyewe au? Duuh...
 
Mimi ni Mkatoliki lakini ninayeamini YESU aliyesema kwa imani hata milima itang'oka sembuse haya?
Pondeni wachungaji lakini acheni kulimit uwezo wa Mungu.
Mleta mada ungesema huamini kama wale misukule kweli nisingeshangaa lakini futa kauli ya kutoamini miujiza kwavile huoni kanisani kwako.Mimi kwenye mikutano ya Karistimatic nimeshuhudia miujiza mizito hivyo sishangai uwezo wa Mungu.
 
Mimi huwa nachokaga na haya mambo. Sijawahi kufika katika hizo ibada ila nachojiuliza hao wanaoitwa misukule inafikaje hapo kwa Gwajima..yaani kama huyo alietoka Mortuary alikuja mwenyewe au? Duuh...

mambo haya mungu aliwaficha wenye hekima na akili akawafunulia watoto wadogo
uwezi kuelewa
 
mbona unajichananya?...hujui unachokiandika,yap kuna maigizo ila sio kweli kwamba haiwezejkani kufanyika,Yesu amamwenyewe aliahidi kwamba kazi alizoifanya hata sisi tunaweza kuzifanya na zaidi....so what area you talking about?...vp nyie kwenu hamuwezi fanya?
 
Mimi huwa nachokaga na haya mambo. Sijawahi kufika katika hizo ibada ila nachojiuliza hao wanaoitwa misukule inafikaje hapo kwa Gwajima..yaani kama huyo alietoka Mortuary alikuja mwenyewe au? Duuh...

Wewe hupaswi kumuamini mchungaji bali amini uweza wa jina la YESU.
Kutokuamini kwenu kuna shangaza mbona mnaamini ulinzi wa majini lakini mkisikia muujiza wa MUNGU doubt kibao na vijisababu visivyoisha.
 


halafu kwa hali ya kawaida tu haiwezekani mtu aliyekufa zamani kiasi hicho afufuliwe bana,tunakumbuka yesu alimfufua lazaro siku ya tatu tena alikuwa tayari ananuka,tunakumbuka elisha alimfufua mtoto wa mwanamke mshunami tena baada ya siku tatu tu,hapo sciense inataka kutueleza alikufa kwa muda mrefu mwili wake hauwezi kurejea kwa sababu utakuwa umekosa chakula kwa muda mrefu,tuache utani kwenye mambo ya Mungu jamani
 


unazungumziaje issue ya babu wa loliondo?wabongo ndio zao bana kukurupuka halafu kimyaaaaaaaa,mimi natoka Arusha lakini issue ya babu ilinifanya nirudi nyuma na kujiuliza maswali kibao,ndugu zangu walilazimisha nisafiri ili nikale kikombe cha babu,lakini niligoma muda si muda tukasikia story kuhusu babu,haahahaaa,wabongo bana
 

kuna mengi yakufanya zaidi ya kuigiza na misukule..
Kuna mafundisho mengi sana ambayo watanzania wanayahitaji katika kujikwamua na umaskini..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…