Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara


Kwanini baba asipande watoto wake
 
Kwanini baba asipande watoto wake

..wafugaji wanasema beberu akipanda binti yake kutatokea kitu kinaitwa " inbreeding."

..nimeangalia kwenye mtandao madhara ya inbreeding ni kama yalivyoelezwa hapo chini.

The most obvious effects of inbreeding are poorer reproductive efficiency including higher mortality rates, lower growth rates and a higher frequency of hereditary abnormalities. This has been shown by numerous studies with cattle, horses, sheep, swine and laboratory animals.
 

Hii imatokea endapo kuna magonjwa ya kurithi katika huo uzao.

Je mtoto na mama ni ruksa kuzaana au dada na kaka katika hao mifugo?
 
Mbuzi single mother dili ila kwa dada zetu.....
 
Hii imatokea endapo kuna magonjwa ya kurithi katika huo uzao.

Je mtoto na mama ni ruksa kuzaana au dada na kaka katika hao mifugo?
..nilivyoelewa ni hivi.

..beberu asimpande binti yake.

..beberu asimpande mama yake.

..beberu asimpande dada yake.

NB.

..ngoja nitatafuta video inayoelezea vizuri topic ya inbreeding.
 
Unataka elimu gani ndugu tukusaidie ktk ufugaji wa Mbuzi?
 
Naomba niwasaideni kitu hapa kuagiza Mbuzi south Afrika hakuna urasimu wowowte mimi nazungumzia uzoefu na ninacho kifahamu, mwakajana mfugaji mwenzetu kaleta Red kalahar bila ya shaka na ktk umoja wetu wote walio agiza wamepata, shida ni moja kubwa hata kule south kunawapigaji sana. mnacho takiwa ni kufwata waagizaji wanaojuwa wazalishaji wa ukweli, hata ukienda uganda hata Mubende watakupiga tu ninaushahidi kwakweli. Mbogo Ranchese, Mavuno Farm, Biswalo, Usangu, ASAS. Hao ni waagizaji wa kweli na watakupatia kitu unacho hitaji, wakikuzulumu njoo Nyumbani kwangu nakulipa Mubende 1 bure kabisa.
 
Nazungumzia utafiti wa kujuwa mbegu unazotaka kufuga uzichaguwe vyema maana mwisho wa siku unaweza pewa Mbuzi mwonekano ni mzuri lakini kwenye uzalishaji ni majanga, tembeleeni shsmbani farm na Mavuno farm mtajifunza kitu, walioko Dar karibuni Nyumbani kwangu kibamba kwa mangi njootusome zaidi. Kufuga Mbegu yoyote ya kigeniinakupasa kutafuta abc zake ili ikusaidie kujua jinsi ya kuendesha huo mradi, Shamban farm na Mavuno na Mbogo watawasidia sana.
 

Great
 
Asante kwa haya
Je mlifanikiwa kuwaleta kwa njia gani ya ndege au kwa usafiri wa kawaida
Na je mlikuwa kama kikundi au na je vibali vinatokaje?
 
Asante kwa elimu hii mkuu
Hao gala wanapatikana kwa bei gani?
 
Huyo jamaa wa Ghana yuko vizuri sana

Sasa mkuu kama nanunua hao Boer kama alivyosema yeye alijifunza na anajufinza mengi kama hali ya hewa kwa hao mbuzi

Sijui pia kwetu kama Bara wataishi vizuri haya ndio ya kuzingatia pia
 
Asante kwa haya
Je mlifanikiwa kuwaleta kwa njia gani ya ndege au kwa usafiri wa kawaida
Na je mlikuwa kama kikundi au na je vibali vinatokaje?
Sisi ni TAGOFA chama cha wafugaji Mbuzi Tz na mletaji ni mwanachama , Mbuzi waliletwa kwa njia ya bara bara na hata ASAS last week kaleta Ngombe kutoka south kwa njia ya bara bara. Msafirishaji anashughulikia vibali vyote wewe unapokea Mbuzi mwenye nyaraka kamili, nawaomba ruhusa niweke number zao humu mtaweza wasiliana nao moja kwa moja.
 
Huyo jamaa wa Ghana yuko vizuri sana

Sasa mkuu kama nanunua hao Boer kama alivyosema yeye alijifunza na anajufinza mengi kama hali ya hewa kwa hao mbuzi

Sijui pia kwetu kama Bara wataishi vizuri haya ndio ya kuzingatia pia
Wanaishi kabisa bila ya shaka naomba mtembelee Shamban farm Biswalo utaona na kujifunza kitu juu ya ufugaji wa hawa Mbuzi.
 
Asante kwa elimu hii mkuu
Hao gala wanapatikana kwa bei gani?
Galla/isiolo huwa wanapatikana majike wakubwa amabao tayari kupandwa na kuzaa ni sh laki 2, madume ndio wana bei ni kuanzia laki 2 mpaka 5 inategemeana na ukubwa na umri wa Mbuzi, napo wakati wakununuwa unapashwa uangalie swala la umri ni muhimu sana hasa kwa Dume usije chukuwa mwenye umri mkubwa sana akashindwa kutumika vyema.
 
Ntashukuru sana kwa namba zao

Ila ASAS nawajua na mwanangu alisoma na mmoja wa watoto wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…