Wana JF,
Nimeona mm pia nitoe testimonial kwa faida ya wajasiriamali wanaopenda kilimo na ufugaji.
Ndoto yangu imekuwa kutafuta ujasiriamali utakaoniwezesha kuachana na ajira at 40yrs.Baada ya kujaribu biashara mbalimbali nikagundua kuwa faida zilizopo kwenye kilimo na ufugaji ni kubwa mno especially kama una kamtaji ka kuanzia kapo.Nikaanza kutafuta mashamba.Nikapata kadhaa ila hili la Maseyu ndilo hasa linazaa matunda.kwa wale wanajua morogoro road,hicho kijiji kipo baada ya bwawani au km6 kabla ya mikese.Shamba lipo km1.5 toka barabarani.Nilinunua eka 100 mwaka 2011.Immediately nikaanza kufyeka na kung'oa visiki.Nikalima eka10 za mahindi na alizeti mwishoni 2012.Nililima eka 2 za tikiti maji.mazao yanastawi si mchezo.masika ya 2013 nikalima eka 20 za alizeti na mahindi.pia nikaanzisha mradi wa nguruwe.
Nilianza na nguruwe 8 jike na dume mmoja.sasa nina nguruwe kama 70 hv.Nilipata changamoto kidogo,nguruwe watatu walikufa.kwa changamoto hizo nimepata uzoefu mkubwa. Mambo mengi kama kuchoma chanjo na kutibu baadhi ya magonjwa naweza kufanya mwenyewe kwa maana madaktari nao ni changamoto.nategemea kuanza kuuza nguruwe wakubwa by April.wadogo nauza though soko lake sio kubwa sana.
Pamoja na upunyufu wa mvuA mazao yangu ya vule yamekomaa.nna tikiti kama eka10 na mahindi kama eka25.
Nextmonth nategemea kulima eka kama 70 hv.nataka kulima mahindi,alizeti,ufuta,mtama na maboga.vyote kwa biashara na chakula ya mifugo yangu.
Nataka niweze kuuza nguruwe 20 kila mwezi by this year.
Mwaka jana nimevuna zaidi ya gunia 200 za mahindi na 150 za alizeti.fuso 2 za tikiti maji.Cha zaidi nimetoa ajira kwa vijana kazaa
Tatizo la maji shambani nimetatua last year kwa ku design bwawa na matank cheap.
Karibuni wajasiriamali,future ipo kwenye kilimo.unauza mazao yako hamna mtu anakuuliza kodi! Hahaa