Mkuu Deo Corleone umenena mkuu mpaka haya mambo yanachosha sasa huwezi kufungua jukwaa usikutane na habari za hao jamaa na zinakuwa hizo hizo kuanzia asubuhi watu wanashindana kuanzisha topicHuku ndo kwa kushinda na kupata maujuzi. Sio kila siku lema,kinana,mbowe zitto,
Wana JF,
Nimeona mm pia nitoe testimonial kwa faida ya wajasiriamali wanaopenda kilimo na ufugaji.
Ndoto yangu imekuwa kutafuta ujasiriamali utakaoniwezesha kuachana na ajira at 40yrs.Baada ya kujaribu biashara mbalimbali nikagundua kuwa faida zilizopo kwenye kilimo na ufugaji ni kubwa mno especially kama una kamtaji ka kuanzia kapo.Nikaanza kutafuta mashamba.Nikapata kadhaa ila hili la Maseyu ndilo hasa linazaa matunda.kwa wale wanajua morogoro road,hicho kijiji kipo baada ya bwawani au km6 kabla ya mikese.Shamba lipo km1.5 toka barabarani.Nilinunua eka 100 mwaka 2011.Immediately nikaanza kufyeka na kung'oa visiki.Nikalima eka10 za mahindi na alizeti mwishoni 2012.Nililima eka 2 za tikiti maji.mazao yanastawi si mchezo.masika ya 2013 nikalima eka 20 za alizeti na mahindi.pia nikaanzisha mradi wa nguruwe.
Nilianza na nguruwe 8 jike na dume mmoja.sasa nina nguruwe kama 70 hv.Nilipata changamoto kidogo,nguruwe watatu walikufa.kwa changamoto hizo nimepata uzoefu mkubwa. Mambo mengi kama kuchoma chanjo na kutibu baadhi ya magonjwa naweza kufanya mwenyewe kwa maana madaktari nao ni changamoto.nategemea kuanza kuuza nguruwe wakubwa by April.wadogo nauza though soko lake sio kubwa sana.
Pamoja na upunyufu wa mvuA mazao yangu ya vule yamekomaa.nna tikiti kama eka10 na mahindi kama eka25.
Nextmonth nategemea kulima eka kama 70 hv.nataka kulima mahindi,alizeti,ufuta,mtama na maboga.vyote kwa biashara na chakula ya mifugo yangu.
Nataka niweze kuuza nguruwe 20 kila mwezi by this year.
Mwaka jana nimevuna zaidi ya gunia 200 za mahindi na 150 za alizeti.fuso 2 za tikiti maji.Cha zaidi nimetoa ajira kwa vijana kazaa
Tatizo la maji shambani nimetatua last year kwa ku design bwawa na matank cheap.
Karibuni wajasiriamali,future ipo kwenye kilimo.unauza mazao yako hamna mtu anakuuliza kodi! Hahaa
Karibu kaka,
Aliyeleta mchanganuo wa chakula ni mm.Hiyo heading ya topic yangu nna maanisha kuwa ufugaji na kilimo vikienda pamoja,utaweza kupata manufaa kwa kiwango kikubwa kwa maana hizo sector zina leverage each other.Bei za vyakula hubadilika sana,ukilima mwenyewe inakupa unafuu sana
Haswaa Mamajoe,Kabisa maana gharama kubwa ufugaji wowote ni chakula, ninapenda kutanuka kwenye kuku huku mjini lakini chakula nitalima kiasi mimi mwenyewe. Ninapenda kuongeza aina ya mifugo kama mbuzi nayo nimefanya utafiti majani nitaotesha mwenyewe. Ukilima hata sehemu tu ya chakula cha mifugo unapunguza gharama sana na hivyo kuweza kutanuka/kukua ila kwa kununua chakula ni kupoteza muda tu biashara haikui
baada ya gharama za uzalishaji unapata faida ya pesa kama kiasi gani?
Haswaa Mamajoe,
Nilipiga hesabu.ukinunua chakula cha nguruwe kilichochanganywa tayari cost ni 600/kg.Nikichanganya mwenyewe lakini nikanunua ingredients ni about 320/kg.lakini nikitumia mazao niliyolima it goes down to about 100/kg.pia napata mbolea.Incredible!
Asante sana niliishawahi kufikiria kuhusu kuchanganya chakula mwenyewe cha kuku nikapiga hesabu kwa kununua mahindi ni sawa tu na kununua chakula kamili, lakini sasa nitalima alizeti, mahindi na mtama hivyo nitanunua vilivyobaki tu gharama itapungua. Nilitaka kufugia mbuzi huku mjini nimeona ni gharama, nitaotesha majani na miti ya virutubisho shambani hivyo nitapunguza sana gharama. Mjini itakuwa kama depot tu za kuletea mifugo na kuiuza maana soko ni kubwa Nashukuru kwa kunifungua macho nitakutafuta zaidi nikiwa na maswali.
Za siku Mama Joe, Naona umeongelea mbuzi hapa, vipi biashara yake kwa Dar inalipa, nina hekari kama 70 hivi Rufiji huko pembeni ya mto na kwa tahmini ya haraka ardhi ya huko inakubali sana majani yale marefu yanayoliwa na mifugo na maji yapo ya kutosha,
Nilikuwa ninampango wa kufuga nguruwe ila naona wakazi wengi pale ni waislamu na mto tunashare nao kwa hiyo kelele ni nyingi si unajua tena, na wao ndio wenyeji wangu.
Kama una info zozote za Mbuzi hasa wale wanao zaa mapacha naomba unipe kwa maana ya bei ya sokoni na ni wangapi wanaweza kutunzwa kwa hekari moja maana nitakuwa nawalimia majani(maji yapo ya kutosha mwaka mzima).
Shukrani sana
Capital kubwa ilikuwa kununua shamba,nilipata eka 100 kwa 10m.Hayo mengine niliweza kuyafanya on a monthly bases.nimeajiriwa so every month nilikuwa natenga kiasi kwenda shamba. Baada ya kuanza kilimo,sehemu kubwa shamba linajiendesha.na kilimo kule ni relatively cheap.in tye next 3 years nitakuwa mbali sana
Asante sana niliishawahi kufikiria kuhusu kuchanganya chakula mwenyewe cha kuku nikapiga hesabu kwa kununua mahindi ni sawa tu na kununua chakula kamili, lakini sasa nitalima alizeti, mahindi na mtama hivyo nitanunua vilivyobaki tu gharama itapungua. Nilitaka kufugia mbuzi huku mjini nimeona ni gharama, nitaotesha majani na miti ya virutubisho shambani hivyo nitapunguza sana gharama. Mjini itakuwa kama depot tu za kuletea mifugo na kuiuza maana soko ni kubwa Nashukuru kwa kunifungua macho nitakutafuta zaidi nikiwa na maswali.
Mkuu Deo Corleone umenena mkuu mpaka haya mambo yanachosha sasa huwezi kufungua jukwaa usikutane na habari za hao jamaa na zinakuwa hizo hizo kuanzia asubuhi watu wanashindana kuanzisha topic
Karibu mkuuI wish Mimi nipigwe bann nisione thread hatamoja ya Huko siasani zinabore sana
back to topic Mkuu MalafyaleP mwaka huu nitajitahidi nianze na heka kumi and please I will ask your assistance tupo pamoja sanaa mkuu
Mkuu hongera sana, naomba unijuze kuhusu kilimo cha ufuta, kuanzia upatikanaji wa mbegu, kilimo chenyewe kinachukua muda gani hadi mavuno na soko lake, je maeneo ya korogwe mkoani tanga kwa kilimo cha ufuta na alizeti naweza kupata?
Mkuu Dolevaby tupe elimu zaidi tafadhaliKwa kiasi kikubwa UFUTA unakubali maeneo mengi 7bu hauhitaji MVUA nyingi! ziko mbegu aina nyingi mfano,LINDI 2OO2 hii ukitunza shamba vzr unavuna 1-1.2tons Mbegu kwenye maduka ya Pembejeo ila kuwa makini na kitu FEKI Ukiwa seriuos nishtue
Unaitamanisha hadi nasimamisha kucha. Natafuta sana kisehemu karibu na Dar, japo nifuge hata njiwa tu.
Kongosho sikujua kwamba kucha nazo huwa zinasimama, kwangu kilichosimama ni vinyweleo pekee. ON a serious note, nimeguswa sana na thread ya Malafyale ila nataka kuwa mwangalifu sana nisiishie kwenye mihemuko tu bila kuchukua hatua kama ilivyonitoeka mara kadhaa. Eee Mungu Baba nisaidei nichukue hatua this time kiukweli kabisa kabisa. Malafyale nitakusumbua sana kwenye hili ila unaonekana uko tayari kusaidia so thanks in advance.