Ufugaji na kilimo unalipa sana


Mkuu hongera sana na asante kwa kushare na sisi hii kitu.
Naomba nijue,
1. Sehemu unayofugia ni porini au ni karibu na makazi ya watu? Hali ya usalama ikoje huko?
2. Kwa wastani nguruwe mmoja mkubwa anauzwa kwa bei gani? na mdogo wa kuanza nae unamnunua kwa sh. ngapi?
3. Wanachukua muda gani kuwa wakubwa hadi kufikia kuuzwa?
4. Vipi mazao mengine ya nafaka kama shayiri na ufuta unakubali maeneo hayo?

Asante mkuu na samahani kwa kukuchosha kwa maswali.
 
mKUU Mbimbinho,
ahsante.
1. sehemu ninayofugia ni shambani mbali kidogo na makazi ya watu. Usalama upo kwani kuna vijana pale wanaangalia
2. Nguruwe mkubwa anauzwa kuanzia 200,000-400,000 inategemea ana uzito gani. Nguruwe mdogo alietoka kuachishwa anauzwa kwa shs.30,000-40,000 inategemea na uzito
3. Nguruwe huchukua miezi 6-8 kufika uzito wa kuuzwa .inategemea na matunzo
4. Ufuta una stawi sana! Masika hii nategemea kulima eka10 za ufuta.

Nashauri kama upo interested tembelea wafugaji na wakulima walio karibu kupata uzoefu.
 
Mkuu nimevutiwa na uzi wako.
Nami nipo kwenye hz harakt bado nakusanya nguvu.
Hivi ufuta kwa heka unaweza vuna gunia ngap kwa wastani?nipo dodoma je maeneo gani ufuta unakubali?na mahitaji yake ya hali ya hewa yapoje na gharama zake kwa heka ni kiasi gani??
 
Heka 100 ulinunua kwa sh ngapi? Ulianza lini kufuga nguruwe au 9 na mpka leo wapo 70? Maelezo mengi hayajakamilika gunia 200 na 150. Ulilima lini?
Maelezo yote ya mtaji kesha sema someni thread hizi kabla ya kuuliza. Hata hivyo suala la magunia 200 au 150 si kitu cha stusha kwani mahindi kimsingi huchukua takribani siku 90 unavuna! Kama alipanda ekari kuimi hayo magunia 150 hadi 200 ni cha mtoto Mr!
 
kaka asante sana, nimekipata kitabu hiki "the law of success by Napoelon Hill" kina page 130 na pia nimekipata kitabu hiki "the richest man in babylon" http://www.ccsales.com/the_richest_man_in_babylon.pdf

NAOMBA LINK YA KITABU CHA the law of success by Napoelon Hill na kitabu cha THink and grow rich by Napoelon Hill
 
Wadau kitu kikubwa ni kuthubutu kutenda kwa ufahamu wangu uthubutu ndio mtaji tosha mana ukiwa na nia unaweze kuanza hata kwa kukodi mashamba hata ekari 1 na baada ya kuilima na kuihudumia itakupa mtaji. kwa upande wangu nimeanza kwa kukodi ekari 10 ambazo 5 nimepanda mahindi na 5 nategemea kupanda maharage mwezi 2. feedback nitawapa june this year.
 
Ahsante mzee mkaruka.
Watu wengine wanakosa initiative kidogo tu ya kusoma threads kabla ya kuuliza maswali.Pia nadhani ni vema kuuliza maswali ya msingi.
 

Asante sana mkuu MalafyaleP

Mkuu kama nitakusumbua tena, kwa sasa mimi target yangu ni kulima Ufuta mwakani, hivo kwa sasa hivi nafanya kautafiti fulani hivi, then later on after a year or two ndo nitarudi kufuga.
Tafadhali naomba nisaidie kwenye ufuta, faida, soko na changamoto za kilimo hiki sina uzoefu wa kutosha na pia ghrama zake za uzalishaji kwa eka. Kwa sasa nina shamba kama ekari 40 maeneo ya vigwaza karibu na chalinze, hopefully ardhi hazitofautiani sana.
 
Last edited by a moderator:
Ok.mi sijawahi lima ufuta ila jirani yangu alilima mwaka jana.
Ufuta ni high value crop.kwa kilo inaweza fika 3500 na wanakufuata shambani.
Ufuta unahimili vizuri uchache wa mvua na kwa heka ukipata mbegu nzuri kama lindi unaweza pata kilo 1000.
Unahitaji kupiga dawa wadudu waharibifu.
Changamoto kubwa ni uvunaji.usipojipanga vizuri sehemu kubwa inapotea shambani.unahitaji kujua wakati muafaka wa kuvuna .
Nimeona kuna threads kuhusu ufuta,jaribu ku peruse.
Je huko vigwaza wanachi wanalima nn? Kama kuna mazao wanalima masika,ufuta utakuwa unakubali maana maeneo yote ya pwani ufuta unastawi
 
Last edited by a moderator:

Mimi nililimisha Handeni mwaka jana kila ekari moja nikapata kilo 400 (@3,200/=)
 

Asante sana mkuu, Nitafuatilia nipate hints za namna ya uvunaji. Pia nafikiria kumtafuta bwana shamba/Mtaalamu wa mambo ya shamba wa maeneo ya karibu or kibaha hata kwa kumlipa but aweze kunisaidia kwa karibu zaidi kuhusu ushauri na nini muhimu kilimo kinahitaji. Unajua sie wengine hatujawahi kuwa shambani so mambo mengi hatuyajui.

Maeneo ya kule nimesikia watu wanalima sana mihogo, na baadhi ya nafaka, sina hakika ni nafaka zipi, but kuna mtu alishawahi niambia kuwa baadhi wanalima ufuta pia.
 

Mimi nililimisha Handeni mwaka jana kila ekari moja nikapata kilo 400 (@3,200/=)

Mkuu kwa sasa bado unaendelea kulima?? na hiyo bei ni bei ya shambani or ya sokoni?
Vipi kuna changamoto gani ulizopitia??
Vipi unafikiri ungeweza kuvuna zaidi ya hizo kilo 400 kwa Ekari moja???

Samahani mkuu kwa maswali, but tuvumiliane mkuu.
 
kwa sisi wakulima hii ni ndoto...ila ushauri wangu jiunge na act
 
Mkuu kwa sasa bado unaendelea kulima?? na hiyo bei ni bei ya shambani or ya sokoni?
Vipi kuna changamoto gani ulizopitia??
Vipi unafikiri ungeweza kuvuna zaidi ya hizo kilo 400 kwa Ekari moja???

Samahani mkuu kwa maswali, but tuvumiliane mkuu.

Mwaka jana nililimisha eka 5 tu mwaka huu nalimisha 50. changamoto ni nyingi muhimu zikiwa:


  1. [*=1]Kuyajua majira ya kilimo vizuri

    [*=1]Aina ya mbegu. Mwaka huu nimepata mbegu toka Mtwara ambayo ni nzuri kidogo.
    [*=1]Watu wa kule wakorofi sana lazima waingie shamba kukusaidia kuvuna(kwa kukuibia)
    [*=1]Muda wa usimamizi na ufuatiliaji.
    [*=1]​Mvua isiyokuwa ya uhakika
 

Safi sana mkuu.
Naomba kuuliza, je huko unakofanyia shughuli zako za kilimo hakuna migogoro na wafugaji ?
Nauliza hivyo maana huku kwetu sisi wafugaji wanakera sana.
Sasa nataka kuhama kabisa ili nitafute shamba jingine ambalo hakutakuwa na kero za wafugaji.
Kama huko kwako huko salama, maweza kukutafuta ili na mimi nije kupata shamba huko.
Asante mkuu.
 

Mkuu kama vipi itabidi unipe contact yako, siku ukipata mbegu bora zaidi nitaomba unishtue na mimi maana natarajia kulima mwakani Mungu akinijalia.
Na average mbegu wanauzaje kwa kilo? Nasikia pia ufuta mweupe ndo unalipa zaidi, kama ukipata mbegu yake itakuwa nzuri zaidi.
Kuhusu mvua nimesikia ufuta hauhitaji mvua nyingi kama mahindi, zaidi mvua inahitajika sana katika zile phase za mwanzoni kabisa, ni kweli??
Mkuu MalafyaleP msaada kama ukipata mbegu bora zaidi za ufuta.

Nimejipanga kuhudhuria maonesho ya nane nane mwaka huu popote pale yatakapofanyika. Hopefully nitapata something.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…