Ufugaji samaki kwa Vizimba (Cage Fish Farming)

Ufugaji samaki kwa Vizimba (Cage Fish Farming)

babilas25

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
482
Reaction score
353
Ufugaji wa samaki kwa vizimba ni njia rahisi na yenye tija kwa wafugaji samaki kibiashara. Nitakuelezea hapa hatua na gharama zake na mambo mengine ya kuzingatia.

1.Vibali vya uendashaji wa shuguli za ukuzaji viumbe hai majini

I)Mhutasari wa kikao cha serikali ya kijiji au mtaa ambapo mradi utafanyika.

II)TAFIRI- Kufanya survey kwenye eneo ambapo vizimba vitawekwa, kupima kina cha maji, ubora wa maji, mkondo wa maji, ukubwa mawimbi n.k. galama ni Tsh. 2,700,000/=

III)NEMC-Kufanya Environmental Impact Assessment, galama yao n 4,200,000/=

IV)Bonde la Ziwa Victoria- Kutoa kibali cha matumizi ya maji

V)Barua ya Afsa uvuvi wa eneo husika

VI) Kibari kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi idara ya ukuzaji viumbe hai majini.

2.Kutengeneza kizimba na Kupanda vifaranga.
-Kizimba chenye urefu wa mita6, upana mita6 na kina cha mita6, kinaweza kubeba vifaranga 10,000.
-Galama za kutengeneza kizimba ni 3,500,000/= na vifaranga tsh.2,000,000 kwa vifaranga 10,000.

3.Galama za vyakula.
Kilo1 ya samaki ni sawa na kilo1.3 za chakula. Hivyo matalajio ya mavuno yatategemea pia kiasi cha chakula.
Mfano; samaki 10,000 wanaweza kufika wastani wa kilo 2500 mpaka 3000.
Hivyo watakula kilo 3250 mpaka 3900.
Vyakula vimegawanyika katika makundi 3
  • Starter
  • Glower
  • Finisher

(Galama ni kati tsh2500/kg mpaka 3000/kg)

4.Galama ya usimamizi na ulinzi wa mradi (Ni makubaliano)

5.Mavuno; Kwenye kizimba cha ukubwa wa mita za eneo 36 kinaweza kubeba vifaranga mpaka 10,000 vya sato, Matarajio ya kuvuna ni samaki 8500 mpaka 9000 ambao wanakadiliwa kuwa na uzito wa gram 400 mpaka 600
Wastani wa mavuno ni tani 2.5 kwa miezi 6.

===================
Unahitaji kufuga samaki kwa njia ya vizimba, Karibu Imani Aqua farm.
Huduma tunazotoa n pamoja na
-Ushauri wa kitalaam juu ya ukuzaji viumbe maji
-Hatua za kufuata kabla hujaanza kufuga samaki
-Kutengeneza na kufunga vizimba vya kufugia samaki
-Mbegu bora ya samaki
-Usimamizi wa miradi ya ufugaji samaki kwa vizimba.
Tunapatika mwanza Luchelele.
Kwa mawasiliano zaidi tupigie +255764123459
Cc:Babilas25
 
Hujaeleza samaki gani wanakaa 10,000 kwenye mita za eneo 36 au aina zote?

Pia yaani nikitaka kuanzisha kamradi ka Ufugaji samaki Lazima niwe na NEMC, kibali Cha wizara
 
Hujaeleza samaki gani wanakaa 10,000 kwenye mita za eneo 36 au aina zote?

Pia; yaani nikitaka kuanzisha kamradi ka Ufugaji samaki Lazima niwe na NEMC, kibali Cha wizara, bonde.....eeeeeeegepah!!
Samaki aina ya sato mkuu
Kuanzisha mradi wa ufugaji kwa kutumia vizimba lazima upitie kwenye mamlaka hizo au unaweza jishikiza kwa watu wenye vibali kwa makubaluano maalum.
 
VizimbaView attachment 1762341
JamiiForums739291204.jpg
 
Je, nikitaka kufugia morogoro au Katavi, je hizo mamlaka za ziwa victoria ninapaswa kuziona?
 
Kwenye huu mfumo wa kizimba lazma kutakua na changamoto ya virutubisho au vyakula kutoka nje cafe kwa sababu ya mawimbi hvo atuwezi kukadiria moja kwa moja kua kila kilo moja ya samaki atatumia 1.3 naomba utuelezee jinsi ya kuikabiri chngamoto hii maana bila hvo samaki awatakua wanafikia uzito stahiki
Ufugaji wa samaki kwa vizimba ni njia rahisi na yenye tija kwa wafugaji samaki kibiashara. Nitakuelezea hapa hatua na gharama zake na mambo mengine ya kuzingatia.

1.Vibali vya uendashaji wa shuguli za ukuzaji viumbe hai majini

I)Mhutasari wa kikao cha serikali ya kijiji au mtaa ambapo mradi utafanyika.

II)TAFIRI- Kufanya survey kwenye eneo ambapo vizimba vitawekwa, kupima kina cha maji, ubora wa maji, mkondo wa maji, ukubwa mawimbi n.k. galama ni Tsh. 2,700,000/=

III)NEMC-Kufanya Environmental Impact Assessment, galama yao n 4,200,000/=

IV)Bonde la Ziwa Victoria- Kutoa kibali cha matumizi ya maji

V)Barua ya Afsa uvuvi wa eneo husika

VI) Kibari kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi idara ya ukuzaji viumbe hai majini.

2.Kutengeneza kizimba na Kupanda vifaranga.
-Kizimba chenye urefu wa mita6, upana mita6 na kina cha mita6, kinaweza kubeba vifaranga 10,000.
-Galama za kutengeneza kizimba ni 3,500,000/= na vifaranga tsh.2,000,000 kwa vifaranga 10,000.

3.Galama za vyakula.
Kilo1 ya samaki ni sawa na kilo1.3 za chakula. Hivyo matalajio ya mavuno yatategemea pia kiasi cha chakula.
Mfano; samaki 10,000 wanaweza kufika wastani wa kilo 2500 mpaka 3000.
Hivyo watakula kilo 3250 mpaka 3900.
Vyakula vimegawanyika katika makundi 3
  • Starter
  • Glower
  • Finisher

(Galama ni kati tsh2500/kg mpaka 3000/kg)

4.Galama ya usimamizi na ulinzi wa mradi (Ni makubaliano)

5.Mavuno; Kwenye kizimba cha ukubwa wa mita za eneo 36 kinaweza kubeba vifaranga mpaka 10,000 vya sato, Matarajio ya kuvuna ni samaki 8500 mpaka 9000 ambao wanakadiliwa kuwa na uzito wa gram 400 mpaka 600
Wastani wa mavuno ni tani 2.5 kwa miezi 6.
Cc.Babilas 25
 
Kwenye huu mfumo wa kizimba lazma kutakua na changamoto ya virutubisho au vyakula kutoka nje cafe kwa sababu ya mawimbi hvo atuwezi kukadiria moja kwa moja kua kila kilo moja ya samaki atatumia 1.3 naomba utuelezee jinsi ya kuikabiri chngamoto hii maana bila hvo samaki awatakua wanafikia uzito stahiki
Asante kwa swali,
Ufugaji kwa njia ya vizimba ni miungoni mwa njia bora na rahisi ya ufugaji wa Samaki na yenye tija.

Nakwenda kwenye swali lako; mawimbi hayana asali ya moja kwa moja kwenye chakula na hayawezi punguz virutubisho kwenye chakula, kwa njia hii ya ufugaji upotevu wa chakula ni kidogo ukilinganisha na mifumo mingine ya ufugaji, Lisha Samaki wako kwa wakati na kwakufuata maelekezo ya watalaam.

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Huu ufugani unawafaa watu wa kando na vyanzi vikkubwa vya maji na hawana maeneo kama huko unguja pemba mafia ukereme na maeneo kama hayo...
 
Haitokei ajali hapo hicho kizimba kikachanika samaki wakapotelea ziwani?uimara wa hizo nyavu ukoje?
 
Kwanza Samaki wa kuwafuga mabwawani hivyo sio watamu kabisaa

Siwapendi
 
Vibali kama nasafirisha silaha vile. Nilipie milioni 4 ya kibali huo si ni mtaji wa kujenga bwawa dogo kwa simenti kwenye kiwanja changu
Shida ipo kwa watunga sera wetu, watu wanashindwa kuweza kujiajiri sababu kubwa ikiwa ni pamoja na hii
 
Back
Top Bottom