Ufugaji wa Bata: Aina za bata, ujuzi, gharama, changamoto, faida na masoko

Naomba nijibu kwa kadiri ya ujuzi wangu, Bata wote wanapenda maji, Bata wakikosa maji na wakaweza kujua yanapo patikana watakuwa ukiwafungulia wanaruka kuyafwata kwahiyo unajiweka ktk hatari ya kupoteza mifugo kila mara.
Kushu migomba Bata huaharibu migomba, kwanza ile michanga huwa wanaiwahi kiharibu kwakuwa ni michanga, pili ile mikubwa huwa wanaiharibu kwa kuchimba kwenye shina pale panaunyevu unyevu na baadhi ya wadudu.
Bata furaha yake kubwa ipo kwenye kucheza na maji kwamfano Bukini wakishamaliza kula huwa wanapenda kuogelea na maji yakichafuka watapiga kelele wakiwa pembeni ya bwawa mpaka uya badili, Pekini,indian runer,sweedih, na hawa wakawaida pindi tu wanapo kuwa wameshiba vyema hupenda kuoga hasa kipindi cha mchana na ni njia ya kujipooza na joto.
Kuhusu utagaji kwakweli Bukuni nichangamoto sana maana utagaji wao ni apole pole sana na nikwamsimu, pekini waohutaga vyema lakini ni aghalabu kulalia. Nimezungumzia uzoefu wangu nakubali kukosolewa pale nilipo kosea.
 
Bata wa kawaida ana uwezo wa kuatamia na kutotoa mayai mangapi?
 
Nikianza na swali lako la kwanza maji ni muhimu sana kwa bata, wachangiaji wengi wamejibu vizuri, ila mimi nitaongezea kwenye suala la utagaji, bata anapooga anarekebisha joto la mwili wake hivyo humfanya hata atage kwa haraka.

Kuhusu suala la migomba, ndugu bata anaharibu migomba, kwa sisi wenye bata tunajua, tena mate yake noma
akiushambulia mgomba unaweza ukafa kabisa. Mimi wangu mmoja ulikufa.
 
Asa
Asante
 
Ahsante mtoa post kwa Uzi mzuri! Kwa muda mrefu nimekua ktk mawazo ya kufuga bata MAJI kwa maana wanalipa Sana huko nyuma niliwahi kufuga!
Sasa nakusudia kufuga kwa large scale, changamoto iliyo mbele yangu ni namna ya kuliandaa bwawa la kuogelea bata! Na hasa liwe na uwezo wa kuyabadilisha MAJI pindi yanapochafuka!
Ni kwa namna gani nitaweza kujenga bwawa lenye urahisi wa kubadili MAJI? Na eneo langu halina mteremko?
 
Weka inlet na outlet system kwa ajir ya kubadili maji yako
 
Wewe ni mtu wa tatu sasa unaniambia hawa bata ni ghali sana, kwani bei ya bata huyu mwenye mwezi au miezi miwili ni shilingi ngapi mkuu?
 
Mkuu Sasa hivi suala la ufugaji nalo limekua garama sana mbona zaman hayo hayakuepo Mambo ya madawa na Bata wanakula mpaka uchafu wa kwenye makaro ya maji taka na hakuna dawa Wala Nini
 
Mkuu nadhani gharama za madawa chanjo pamoja na hayo maradhi yote ya bata yanategemea zaidi mkoa unaoishi, mazingira ya eneo hilo, pamoja na hali ya hewa ya hapo. Nina bibi yangu anafuga hao bata hajui hata neoxychick ni kitu gani na bata wake hawafi.
Mkuu Sasa hivi suala la ufugaji nalo limekua garama sana mbona zaman hayo hayakuepo Mambo ya madawa na Bata wanakula mpaka uchafu wa kwenye makaro ya maji taka na hakuna dawa Wala Nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…