Changamoto kubwa kwa kanga ni vifo vya ghafla kwa vifaranga. Mwanzoni nilichanganyikiwa unakuta kifaranga mzima kabisa akilowa kidogo tu na hata ukimgusa mikono ikiwa na vimajimaji ghafla anaanza kutetemeka na ndani ya nusu saa amekufa. Akipata stress kidogo amekufa.
Tatizo lingine ni udhaifu wa miguu yaani anatambalia tumbo miguu ime paralyze kabisaa na baada ya muda anakufa
Nilikuwa na vifaranga 200 kila siku wanakufa 10-20 mpaka wakabaki 92
Suluhisho:
Nilikwenda kwa mzee daktari dukani nikamueleza nahitaji chanjo ya kanga na nikampa sababu, akaniambia kanga huwa hashambuliwi na magonjwa Kama kuku na hivyo chanjo haina maana ila vifo kwa vifaranga ni kutokana na upungufu mkubwa wa vitamin A. Alinipa aminovet ya kuwachanganyia kwenye maji (bei 6000) niliwapa mchana ule ule siku ya pili walikufa 2 ambao walikuwa dhaifu na siku ya 3 hakuna kifo na ndiyo ukawa mwisho wa vifo.
Hii iminovet unawapa kila siku na wanaipenda sana, ukiwawekea maji pure hawanywi
Asante sana mzee wangu
Sent using
Jamii Forums mobile app