Ufugaji wa Nyuki ni Ajira nzuri kwa mtu makini. Na wala usihofu kuhusu soko, weka mkazo katika kuhakikisha unazalisha asali ya kutosha. Na hili utalifanikisha pale tu ukiweza kutumia pembejeo (m.f mizinga, n.k) zilizoboreshwa.
Mizinga inayopendekezwa ni ile ya
Tanzania Top Bar Hives. Natofautiana na Malila, mizinga hii inauzwa kati ya TShs. 35,000-50,000 mmoja. Na hata ukitengeneza mwemyewe, gharama ya mbao na vifaa vingine haiwezi kuwa chini ya TShs. 20,000! Mizinga hii ndo imethibitisha uwezo wa kuzalisha makundi makubwa ya nyuki na hivyo kufanya uzalishaji wake wa mazao ya nyuki (asali, royal jery, propolis, nta) nao pia kuwa mzuri. Ni rahisi kupandisha mzinga huu na pia ni rahisi kupakua/kulina asali kwa kutumia mzinga huu.
Unaweza kupata ushauri na maelezo zaidi juu ya Ufugaji na maelekezo ya wapi utapata pembejeo kupitia watu wafuatao:
Dr. Mushtaq Osman-UDSM
Dr. Danstan Kabialo-Afri Honey/Tanzania Honey Council
Mr. Sosthenes Sambua-TPSF
Mr. David Kamala-Tanzania National Beekeeping Supply Ltd
Mr. Jumanne Msuya-MNRT Beekeeping Division
Hawa niliowataja watakushauri haraka na kwa wepesi. Wamebobea na kuzama vilivyo katika sekta hiyo. Iwapo utasoma hapa na kama una dhamira thabiti juu ya ombi lako, nitakuwa tayari kukuunganisha na yoyote kati ya hao watu niliowataja. Japo mara nyingine wao hutoza ghalama kidogo ya thamani ya muda, taarifa na maarifa.
Ericus Kimasha,
+255-71-3-177-372
E-mail: ekimasha@gmail.com