newmzalendo
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 1,385
- 568
Mkiunganisha nguvu mtafanikiwa haraka, kwa mfano,mwezi jana nilipokuwa kijiji kimoja kinaitwa Chogo huko Iringa,niliona mzinga mmoja unafikia Tsh 8000/ kuutengeneza kisasa pale pale kijijini na wenyewe wanasema una ujazo wa debe moja na nusu. Mavuno ni mara mbili kwa mwaka.
Mkuu Malila ,kijiji cha Chogo kipo wapi?Je wanaweza kuituma Dar mizinga kwa bei nafuu.
jamani yeyote anayejua kuhusu ufugaji wa nyuki, mizinga na jinsi ya kulina anieleweshe. natamani kufanya biashara hii nkimaliza chuo.
Mkuu nashukuru sana kwa message hii ina manufaa sana!!.
thanks
Dah afadhali umeamua kuanza harakati za kijiajiri mapema. Na mimi nataka kujiajiri nitafurahi kupata maelekezo juu ya ufugaji nyuki
Nadhani the best way to tackle hii issue ni kuangalia from selling point of view, market.... Je unaweza kununua asali lets say from Tabora ukaipackage vizuri na kuiza nchi za nje au sehemu nyingine. From my research other people make more money from bees than the bee keepers just like the middle men wanavyotengeneza pesa zaidi kuliko wakulima wenyewe. Kwahiyo soma hiyo link niliyokupa hapo juu kuhusu kufuga nyuki ila kama unataka kama biashara pekee utatengeneza more money kuinunua kwa jumla from tabora (including nta) package vizuri na kuresale kwenye supermarkets, au nchi nyingine My point being to make profit from eggs you dont need kufuga kuku unless you love and you are ready kufuga kuku na kuna forum ya wafuga nyuki Can you make a living with Bees - Beesource Beekeeping Forums
Nadhani the best way to tackle hii issue ni kuangalia from selling point of view, market.... .. From my research other people make more money from bees than the bee keepers just like the middle men wanavyotengeneza pesa zaidi kuliko wakulima wenyewe. [/url]
Ufugaji wa Nyuki ni Ajira nzuri kwa mtu makini. Na wala usihofu kuhusu soko, weka mkazo katika kuhakikisha unazalisha asali ya kutosha. Na hili utalifanikisha pale tu ukiweza kutumia pembejeo (m.f mizinga, n.k) zilizoboreshwa.
Mizinga inayopendekezwa ni ile ya Tanzania Top Bar Hives. Natofautiana na Malila, mizinga hii inauzwa kati ya TShs. 35,000-50,000 mmoja. Na hata ukitengeneza mwemyewe, gharama ya mbao na vifaa vingine haiwezi kuwa chini ya TShs. 20,000! Mizinga hii ndo imethibitisha uwezo wa kuzalisha makundi makubwa ya nyuki na hivyo kufanya uzalishaji wake wa mazao ya nyuki (asali, royal jery, propolis, nta) nao pia kuwa mzuri. Ni rahisi kupandisha mzinga huu na pia ni rahisi kupakua/kulina asali kwa kutumia mzinga huu.
Unaweza kupata ushauri na maelezo zaidi juu ya Ufugaji na maelekezo ya wapi utapata pembejeo kupitia watu wafuatao:
Dr. Mushtaq Osman-UDSM
Dr. Danstan Kabialo-Afri Honey/Tanzania Honey Council
Mr. Sosthenes Sambua-TPSF
Mr. David Kamala-Tanzania National Beekeeping Supply Ltd
Mr. Jumanne Msuya-MNRT Beekeeping Division
Hawa niliowataja watakushauri haraka na kwa wepesi. Wamebobea na kuzama vilivyo katika sekta hiyo. Iwapo utasoma hapa na kama una dhamira thabiti juu ya ombi lako, nitakuwa tayari kukuunganisha na yoyote kati ya hao watu niliowataja. Japo mara nyingine wao hutoza ghalama kidogo ya thamani ya muda, taarifa na maarifa.
Ericus Kimasha,
+255-71-3-177-372
E-mail: ekimasha@gmail.com
Ninataka kujikita rasmi kwenye ujasirimali ambao hautakua na risk kubwa. Nimefikiri Ufugaji wa Nyuki unaweza kuwa na tija kwa sababu hawahitaji chanjo, maji, umeme, ni kuweka mzinga na kwenda tu kuvuna kila inapojaa.
Ni nani mwenye taarifa kuhusu mradi kama huu?
- Ni wapi hasa kunafaa kwa ufugaji? nawezafuga vizuri mikoa ya pwani?
- risk zake ni zipi?
- soko lake likoje?