Ufugaji wa kisasa wa Sungura: Ushauri wa masoko na faida za ufugaji

Ufugaji wa kisasa wa Sungura: Ushauri wa masoko na faida za ufugaji

Mfanye research kwenye hio suala kabla hamjaingia kufuga
 
smart people huwa wanaishi kwa kujiuliza maswali ndio kisha wanafanya uamuzi...

swali kwa nini hao wanaokuuzia sungura wachanga wasiwafuge wao na kwenda kuwauza congo?

kuna kitu wanaficha...


Kaka hao jamaaa mwenyew nimewasikia tuu wanaitwa TBCC wao ndyo wanakupa sungura na unawafuga na watanunua kwako siku yoyote hao sungura baada ya kukua kilo 8000/= na wananunua kwa idadi yoyote ile wafatilie mtandaoni
 
Mi nahitaji kufuga sungura mbegu yake naweza pata kwa sh ngapi?kwa anaejua anisaidie
 
Nimewahi kuwafuga miaka ya 2000-2008 nikiwa primary school, niliwanunua na kuuza hata 800/=(mia nane),huyo ni sungura aliyekomaa kabisa, sasa haiwezekani thamani yake ifikie hapo sasa
 
qJue4JD.jpg
Mkuu, inauzwa kwa bei hiyo sehemu gani ? Soko lipo La uhakika ? Maana ukute wanataka tani 20 tuu halafu waahirishe na kusitisha unuaji wa sungura.
 
Mkuu, inauzwa kwa bei hiyo sehemu gani ? Soko lipo La uhakika ? Maana ukute wanataka tani 20 tuu halafu waahirishe na kusitisha unuaji wa sungura.
Mkuu nadhani ingekuwa vyema ungemuuliza hilo swali mtoa mada au kama utaweza pita kwenye tovuti yao ipo kwenye bandiko ilo uwaulize wahusika wenyewe, mimi nilifanya msaada kubandika tovuti ya hao jamaa.
 
Nina ndugu yangu anafuga sungura kule Arusha. Bei ya kilo moja ni zaidi ya shilingi 10,000 na sungura aliyelishwa vizuri anatoa hata kilo 3. Kuna kampuni ya wakenya iliwapelekea hilo dili wakawafundisha jinsi ya kufuga, kuwajengea mabanda, kuwauzia sungura wazazi na kutoa huduma zote za ugani. Kampuni hii inafanya kazi Dar pia. Mwanzoni hawa watu walikuwa na tija ya hali ya juu na wafuga sungura walipata faida kubwa. Sasa hivi choka mbaya. Wanalipa kwa shida sana. Mfugaji anaweza kukaa miezi mitatu hajalipwa na akilipwa analipwa sehemu tu ya madai yake. Ubaya zaidi ni kuwa hakuna mahali pengine pa kwenda kuuza hao sungura. Nadhani suluhisho ni kuachana na ufugaji wa mkataba mfanye tafiti kujua soko la sungura lilipo wafugaji muungane muwe mnauza wenyewe kwenye hayo masoko; au hizi kampuni ziwe huria wafugaji wachague wanakotaka.
 
Ndiyo wanamtoa mtu kimaisha tena sana

Sent From Samsung S9 edge using JamiiForum mobile app
 
Back
Top Bottom