Nina ndugu yangu anafuga sungura kule Arusha. Bei ya kilo moja ni zaidi ya shilingi 10,000 na sungura aliyelishwa vizuri anatoa hata kilo 3. Kuna kampuni ya wakenya iliwapelekea hilo dili wakawafundisha jinsi ya kufuga, kuwajengea mabanda, kuwauzia sungura wazazi na kutoa huduma zote za ugani. Kampuni hii inafanya kazi Dar pia. Mwanzoni hawa watu walikuwa na tija ya hali ya juu na wafuga sungura walipata faida kubwa. Sasa hivi choka mbaya. Wanalipa kwa shida sana. Mfugaji anaweza kukaa miezi mitatu hajalipwa na akilipwa analipwa sehemu tu ya madai yake. Ubaya zaidi ni kuwa hakuna mahali pengine pa kwenda kuuza hao sungura. Nadhani suluhisho ni kuachana na ufugaji wa mkataba mfanye tafiti kujua soko la sungura lilipo wafugaji muungane muwe mnauza wenyewe kwenye hayo masoko; au hizi kampuni ziwe huria wafugaji wachague wanakotaka.