Moja kati ya delicate animals, wanahitaji mazingira yasiyowapa stress ili wakue vyema mfano chakula, maji pamoja na sehemu ya kuishi
CHAKULA:
Kama unataka ukuaji mzuri ni vyema kuzingatia fomula nzuri ya chakula, pia kuwapatia majani kwa wingi ambayo ni msaada sana kwenye kupata vitamins, na formula ya chakula nitakuwekea baadae ukihitaji.
MAJI
Maji pia ni muhimu kuwabadilishia kila siku maana yakiingia mkojo wao hata kidogo hunuka sana hivyo huwafanya kutokunywa, pia waweza wachanganyia industrial vitamins na minerals kwenye maji pamoja na antibiotics kwa ajili ya afya zao.
BANDA
Hapa ndio huwa kuna changamoto kwa sababu kama banda lisipokuwa vizuri basi utapoteza watoto wengi. Na watapotea kipindi cha kuzaliwa na kwenye ukuuaji, kama wakizaliwa alafu banda halipo vizuri basi wanaweza kufa kwa baridi, kukanyagwa au kuumwa na vidudu
Sent using
Jamii Forums mobile app