Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

M

Maelezo ya mtoa mada si nadharia ni halisi,sijatenda ila nimeshuhudia kwa macho.Tunachokwama wengi wetu ni usimamizi.Kuku ufugaji wake ni sawa na mkulima wa bustani.Matokeo yenye tija kubwa yanategemea mno nidhamu ya usimamizi kuliko vitu vyote.

Narudia tena ni maelekezo halisi,ongeza nidhamu kwenye usimamizi.Ninatofautiana naye kidogo kwenye eneo la uwiano wa jogoo na mitetea.Kwa sasa wataalam wanashauri jogoo 1 mitetea 5,kwa mitetea 10 unahitaji jogoo 2 ili washindane.
 
Chakula chao simple sana chukua pumba dagaa mifupa mashudu ya shudu ya alizeti na dcp apo umekomesha kuku wananenepa na wanataga sana
 
Hivi hawa kuku chotara huwa wanataga na kuatamia mayai na kutotoa kama wa kienyeji?
 
Hivi hawa kuku chotara huwa wanataga na kuatamia mayai na kutotoa kama wa kienyeji?
Inategemea na jamii ya kuku chotara, wengine ni watagaji wazuri ila sio waatamiaji wazuri na wengine wanafanya vyote kwa uzuri sana.

Tumia mabwana shamba walio karibu na wewe na hasa tafuta wafugaji waliofuga kwa muda wa kuanzia mwaka kuku chotara hawa wanakuwa na experience nzuri zaidi na kwa mwaka mmoja anakuwa amepitia changamoto na kutumia njia mbali mbali kuzitatua kwa hiyo watakupa hoja zenye tija.

Kitu kikubwa cha kuogopa ni ushauri wa watu ambao hawaja fanya bado. Mara nyingi hutoa hoja zilizo jaa misisimuko na mara nyingi hawana experience ya field, experience ya kufanya ni tofauti na ina mantik sana kuliko experience ya kufuatilia kwa macho na vitabuni.

Ningekusihi ufuatilie aina mbali mbali za jamii za kuku chotara ili ujiridhishe ni aina ipi ungependelea na unauwezo nayo kuifuga.

Asante kwa kusoma, uwe na siku njema.
 
nahitaji sana ufugaji wa kuku wa kienyeje je, kipi nizingatie kabla ya kuanza huu ufugaji..............maombi msaada wenu ndugu zangu.
 
Lengo hasa kubwa ni kujua kama mayai wanayotaga jwa kupandwa na jogoo yanaweza kutotoleka nankutoa vufaranga. Kuhatamia hata incubator inaweza kufanya kazi
 
mkuu mi naitaji sana kufuga kuku wa kizungu na mabanda nishajenga tatizo mpaka sasa sijajua naanzia wapi pia najrbu kupata ushauri kwa watalaam ila nahis bado kuna kitu natafuta naitaj unisaidie
 
Wakuu humu, heshima mbele. Nimefuga kuku kama 100 hivi wa kienyeji, na nawalisha pumba za mahindi mchanganyiko na mashudu, dagaa na madini. Wanaenda vizuri, ila shida ni kwenye utagaji, wanataga wachache na sio kila siku, anaweza kutaga leo, akaruka siku tatu ndio anataga tena. Nilikua naomba msaada humu, kwa wazoefu, namna ya kumfanya kuku wa kienyeji kutaga kwa mfululizo. Kuna majogoo 10 within.
Ahsante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…