Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Soko la kuku esp kama unaishi Dar wala sio la kufikiria sana. Wale kuku wa kienyeji tunaonunua pale kisutu ukiuliza wanatokea wapi ndo utashangaa na kuamini kua hii sekta ina-underproduce. Mimi nafuga wa kisasa na wakifikia wiki 4 nakua nishauza robo tatu ya banda in advance
 
Elimu nzuri sana hii,pesa nje nje kwa mtu makin
i
 
Mkuu, mimi pia ni mmoja wao, namaanisha ndio nimeingia kwenye ujasilimali wa kuku ingawa bado sina ujuzi nao wa kutosha. Nimeanza na kuku 200 wa mayai (kuku wa kisasa) Itakuwa jambo jema sana kam utanitumia database yako walau kwa upeo zaidi. Ubarikiwe.
 
Naulizia bei ya incubator ndogo.Ningependelea incubator ya kiwandani kwa sababu nimeshindwa ku-regulate joto kwenye incubator ya jua kali.Hali ya hewa inabadilika sana na kufanya mabadiliko makubwa kwenye joto la incubator za jua kali.

incubator ya mayai 390 ni tzs 4m. Mayai ya kutotoleshea layers na broilers unanunua wapi kwa bei gani?
 
kwa wawle wafugaji mlioendelea kuna incubator zinauzwa mpaka hapa ni shs 2m na ina uwezo wa kuangua vifaranga 3000

Mkuu nahitaji sana hizo incubator, naomba unipatie contacts za hao jamaa ili nichukue ata moja kwa kuanzia.
 
Wakuu mie sasa hivi nakuku 50 wa kienyeji kati ya hao 15 wamebakiza kama mwezi hivi waanze kutaga hawa 35 waliobaki majogoo 3 wawili wanatamia mayai,sasa mwanzoni hawa 30 walikua wanataga mpaka mayai 15 kwa siku lakini cha kushangaza wameanza kupunguza kutaka mdogomdogo mpaka sasa hivi hatagi hata mmoja,kwa wale wazoefu wanipe mawazo imetokea nini?manake nikiwaangalia afya yao iko poa tu.
 
Asante, kwa msaada. Muda huu ninaoelekea kumalza mtihan wa advc kesho, niwakati muhafaka kufikiri kugusa hili, na kulfanyia uchungu kulingana maeneo ninayo ya KDC - MOSHI. Mwanzo mwema kwangu . . .
 

Nimefurahishwa nawe, kama uwezo upo, naomba unitumie data base yako.
 

Je unaujua umri wa kuku wako wote? Je kabila la kuku wako unalijua?
 
Malila hebu tujuze kwa wastani kuku wa kienyeji atataga mayai kwa muda gani? najua kuna kipindi wanapumzika kidogo lakini je wanakoma kutaga mayai kabisa baada ya muda gani? Hawa wa kisasa tunajua baada ya miaka miwili ni basi je hawa wa kienyeji?
 
Wadau natafuta vifaranga/kuku wa kienyeji ambao ni bora kwa ajili ya kufuga. Kwa aliye nao/mwenye kujua wanapatikana wapi naomba anipatie contact wapi wanapatikana kwa maeneo ya Dar au mikoa ya jirani na Dar.

Wasiliana na Dada Matrida (0715-293-229) wa Muvek Development Solutions Ltd, wahusika wakuu wa Mradi wa Usambazaji Vifaranga Chotara.
 
Mods iunganisheni hii na hiyo topiki mama hapo juu ili tuwe namtiririko nakumbukbu sahihi.....kwako mtoa maada majibu mengi yapo kwenye topic inayofanana na hii hapo juu....na nakushauri upite huko pia
 
Huo ni mradi mzuri sana. Kwani kuku wa kienyeji ni wazuri sana kama utawafuga zero grazing. Ni vizuri uanze na kuku sita kwa maana Jogoo mmoja na matembe watano.

Tengeneza kibanda kizuri sana na uweke sehemu nzuri ya stara kwani kuku hawezi kutaga sehemu yenye vurugu. Kuku wa kienyeji kama utawatunza vizuri wanataka mayai 15 mpaka 18. Na kama atatamia vizuri basi utapata vifaranga 15 na wakitunzwa vizuri utapata kuku 13 au 12. Na akifikisha wiki mbili tu vifaranga hivyo unatakiwa kuvitenganisha na mama yao. waweke sehemu maalum na kuna vyombo vya kutunzia vifaranga vya kienyei huko Tanzania bara.

Vile vile jua kwa mwaka kuku anataga mara tano. Na kama kila kuku akipata vifaranga 12 kila mzao kwa mwaka atatoa vifaranga 60. Na kwa kuku watano utapata kuku 300 kwa mwaka.

Chakula cha kuku hawa ni Pumba za mahindi unawachanganyia na vumbi la dagaa. Debe moja la Pumba unachanganya na vumbi la dagaa kilo moja au moja na nusu.

Kumbuka vile vile kuku wanakula sana majani. Usiache kuwapa majani na maji safi ya kunywa. make sure maji unayabadilisha kila siku asubuhi na kuosha vyombo vyao vya chakula ma maji.

Ili kuku wanenepe na kuwa wazito ni vizuri japo mara mbili au tatu pita feri ukawachukulie utumbo wa samaki unaotupwa. Hii inawanenepesha sana. Vile vile kuku wa kienyeji hawana magonjwa mengi kama wa kizungu. Mti wa ayovela ni mzuri sana kuwakinga na magonjwa. make sure that atlest mara mbili au tatu unatwanga majani ya mti wa Ayovela na kisha unawachanganyia katika maji ya kunywa kuku zako.

Kuna mengi sana lakin kama una suala niulize nitakujuza. Kwani mimi niliwafuga sana na nilifikisha mpaka kuku 3500.

Lakin faida ya kuku wa kienyeji ni kuwa bei yake ni kubwa kuliko kuku wa kawaida. Mayai yake bei kubwa kuliko kuku wa kizungu lakin pia hata mayai ya yasiyo anguliwa (mayai viza)vile vile wananunua waganga wa kienyeji.

faida ni nyingi sana.
 
Mkuu Barubaru nami nimejenga banda nataka nifuge kuku wa kienyeji. Nina mashine ya kutotoresha vifaranga. Je mayai ya kuku wa kienyeji yanaweza totoreshwa kwa machine?
Mkuu nisaidie maelezo mengine yoyote ambayo unadhani yatanisaidia katika ufugaji wangu.
 
Thankx bwana Gazeti ,wazo lako nimelipata. Binafsi saizi niko ktk kilimo cha Mpunga kuishia mwezi mei 2012 nitakuwa ktk mavuno then nataraji kulima kitunguu maji mwezi July-October 2012 .Hivyo kutokana na wazo lako nimeona mazao mengine(yale uliyosema ulilima awali) itabidi niyafanyie kz ili kupunguza cost za mradi kuku kwa 2013 mazao hayo yatakapokuwa tayari. Nimeipenda idia yako kwani inatekelezeka ila structure ya mabanda sijaipata. Basi tuzidi shauriana wa jf
 
Ni idea nzuri, but as biashara ni biashara ya kuku, nadhani it will be wise also to say, dont put all your eggs in one basket;

Kwa nyongeza tu ni kwamba, nimegundua watu wengi wanaofanya biashara ya kuku ni middle class, hapo Tanzania, au should i say, even upper class because the areas they live and the environment supports them doing these kind of things; I wish the author would have also, pin point on the "PRACTICAL RISKS" of doing business like this instead of just writing how wonderful it is; maana, ukitumia 100,000 kununua kuku alafu umeamka asubuhi kesho yake wote wamelala, sijui itakuwaje; ANYWAY, Entrepreneurs are risk takers, use your brains;
 
Tafuta mbegu ya KUCHI toka Pemba....paja lake kama la mbuzi...HALAFU MNOFU MWINGI NA LAINI....huuzwa kati ya 20,000-30,000 kama uko Dar nenda ile njia ya chini Mbezi pale kwa Munanka kuna jamaa anawauza

Una contact za huyo bwana anayeuza hao majogoo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…