Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Wajamen nina vifaranga wa kienyeji wapatao 150. Lakini tangu juzi wameanza kuinamisha vichwa na kushusha mabawa kwa kasi ya ajabu na mpk nachat hivi vifaranga zaidi ya 8 wameshakuwa soo na hata 4 wameshakufa,Nimewapatia tiba ya hizi dawa ya kisasa toka maduka lengwa na bila ya mafanikio,Jamani mwenye kujua kinga/tibabu ya gonjwa hili anijuze. Kwani vifaranga nilishawapa Newcastle kinga ya kideri,nimewapata Antibiotics kbl hata hawajaugua lakini naona bado ni bure kbs wadau!

Jamani mwenye mbinu mbadala anijuze wandugu!

Pamoja daima!
 
Pole mkubwa, beba mmoja uende nae kwa mtaalam akamcheki
 
endelea kutumia dawa. pili rudi tena na wanaoumwa au hata kilichokufa pengine dalili zilikuwa sio wazi usikate tamaa maana hata hapa dalili hujatoa zote, mf wanaharisha? kupumua? chafya? pia kideri ndio gumboro? maana wk ya 1 newcastle wk ya 2 au 3 gumboro. ngoja wataalamu waje watujuze
 

Mama joe!

Kwa kweli nimepitiwa tu kwani dalili ya hawa vifaranga ni wanahara kama chokaa lakini baada ya kuwapatia ile dawa ya Ancoban na ile ya mafua na wengine wanahara maji na muda mwingine wanahara kahawia kabisa.

Naomba kama una mbinu naomba ushauri wako pls!

Thankx!
 
nakushauri tena rudi na elezea dalili au beba kilichokufa. Na kwa vile ni ugonjwa wa kuharisha wale wagonjwa watenge ila hakikisha kila kifaranga kinakunywa maji ya dawa ikibidi utumie kijiko kwa wagonjwa sana. Jitaidi usafi maji vyombo na banda pia. Kuharisha ni maji machafu weka water guard, vzombo osha kwa sabuni kila siku. Ondoa matandiko au maranda maana yamepata uambukizo. Endelea na dawa na zingatia vipimo watapona ila sio automatically
 
sijapitia post zote ila katika second generation ya hao kuku wanaume 55 na wanawake 170 umewapataje maana hawawezi kuzaa 1:4 nahisi itakua 1:1.
 
Naulizia bei ya incubator ndogo.Ningependelea incubator ya kiwandani kwa sababu nimeshindwa ku-regulate joto kwenye incubator ya jua kali.Hali ya hewa inabadilika sana na kufanya mabadiliko makubwa kwenye joto la incubator za jua kali.
KWA MTU ANAYETAKA INCUBATOR ZA AINA YOYOTE ANAWEZA KUNITAFUTA KWA EMAIL honestaugustine@yahoo.com NITAWEZA KUFANYA MPANGO WA YEYE KUPATA INCUBATOR KUANZIA 8EGGS NA KUENDELEA KWA BEI NZURI KULIKO ZOTE AMBAZO MMESHAWAHI KUSIKIA. HIGH QUALITY UHAKIKA WA KUTOTOA KWA MASHINE 95%. TUWASILIANE KWA QUOTATION ZA BEI. UTATAKIWA KUSUBIRI 1MONTH TU. ASANTENI
 
Waazo zuri sana Mkuu@... Usichoke pia ktk kutupatia mawazo ya bishara hata ktk taaluma zingine.
 
Mkuu nashukuru kwa mawazo murua kabisa, nipo katika mchakato wa kuanza huu mradi nita ku pm ili uweze kunipa ushauri zaidi!!!!! Ubarikiwe saana!!!!!

 
GAZETI umeshawahi kufanya biashara ya kuku wa kienyeji? Nakuuliza kwa kuwa nafanya hii biashara kwa miaka miwili sasa, ni biashara inahitaji uvumilivu kwa kuwa kuku wanakufa kila siku, mayai wanataga kwa vipindi virefu vya kupumzika, sio kama unavyowaambia watu, msifanye mchezo unawekeza kila kitu kuanzia muda na fedha zako. Jiulize kwa nini uswahilini kuna kuku wengi wa kienyeji ila umaskini unaongezeka kila kukicha? mambo sio marahisi kama unavyowaaminisha watu GAZETI.
 
naona umeignore gharama za kutengeneza banda la hao kuku (250,000 haitoshi)
Kwa tathimini ya kimaradi , hauonyeshi uhalisia wa kiutekelezaji endelevu, sababu anazotoa ni ni za kununua kuku tu, je kuchanja kuku, kutibu,chakula na virutubisho, gharama za masoko, kiutendanji katika kipindi hicho, na pia kumbuka hawa ni wanyama utekelezaji wake si wakinadharia kama mdau alivyoeleza.Swali ingekuwa rahisi naman hiyo vijijini wa, watu si matajiri?
 
mambo yanawezekana tafadhali
 

mambo yanawezekana tafadhali. kinachotakiwa ni kutokuwa na mawazo ya kushindwa. sasa ndugu kupelwa unataka kufuga kuku halafu usiwachanje? kinachotakiwa ni determination tu na kuelewa biashara unayotaka kufanya.

nchini kenya kuna mtu kawa millionaire kwa ajili ya kuku Soma chini hapa:

Egged on by pride, his simple act of resignation as a carpentry teacher led one Nelson Muguku to explore what has turned to be a billion shilling venture. It all started as a hobby, keeping a few chicken in his teacher's quarters, while pondering what to do next. He survived by selling a few eggs from the chicken. Today, the man owns and runs Muguku Poultry Farm in Kikuyu, Kiambu, estimated to be worth more than Ksh 3 billion. It is one of the largest hatcheries in the country with a capacity to hatch some 200,000 chicks per day. Besides, Muguku is the largest individual shareholder in Equity Bank. Currently he is holding 7,515,085 shares. RIP +
 
habari zenu wakuu.kwa wanaohitaji mayai ya kuku wa kienyeji yanapatikana,tunaweza wasiliana,naomba kuwasilisha.asanteni.
 
habari zenu wakuu.kwa wanaohitaji mayai ya kuku wa kienyeji yanapatikana,tunaweza wasiliana,naomba kuwasilisha.asanteni.
Mkuu mbona kisa siku mnaambiwa namna ya kuweka tangazo ili likae kibiashara lakini mnarudia yaleyale!?
Hakuna price, location, contacts, delivery mechanism, yanauzwa kwa kiasi gani ...
Hata hivyo matangazo yana jukwaa lake
Kila la heri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…