Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Wana Jf,

Kuna maandiko mengi JF ya ufugaji Kuku wa Kienyeji! Nawasilisha kwenu wadau wa JF mbinu ambazo kwa mikono yangu nimezitumia kutatua changamoto za kuku wa kienyeji! Nimeandika kuwalenga wajasiliamali ambao hawana nguvu kifedha kujenga mabanda kisasa, mashine kutotolesha vifaranga, kutibu magonjwa wala kujenga wigo (fence) n,k. Naomba mzijue mbinu hizi nisije kufa nazo, huu ni mchango wangu kwenu watanzania wenzangu wale ambao mtakuwa hamjawahi kuzisikia mbinu hizi. Mbinu hizi baadhi nilisoma vitabuni nikazijaribu na kuziboresha kwa mazingira yangu duni! Mbinu zingine niliziona kwa wakulima duni kama mimi nikazitumia na kuleta mafanikio makubwa, mbinu zingine nilizigundua mwenyewe na nikafanikiwa sana. Hizi mbinu hazijafanyiwa utafiti rasmi lakini nimeweza kufanikiwa kuwa na kundi kubwa la kuku kwa haraka sana kupitia ujanja huu!!

Mdau wa JF nakualika utembelee uzi huu mara kwa mara kila upatapo fursa ili uweze kufuatilia simulizi yangu maana itakwenda kwa vipande vipande. Mnakaribishwa kuchangia uzoefu wenu ili tuboreke zaidi.

Mbinu hizi zitagusia zaidi: Utotoreshaji vifaranga vingi kwa mara moja bila kutumia mashine! Ukuzaji wa vifaranga vingi kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi, ulinzi wa kuku dhidi ya wanyama maadui, kudhibiti kuku wasizurule, magonjwa niliyofanikiwa kuyadhibiti, ujenzi wa vibanda wenye kukidhi mahitaji mbali mbali. Ni utaalamu nilioupata kwa gharama kubwa na mahangaiko ya muda mrefu, nauleta kwenu ili sote tuendelee kukua pamoja kiujasilia mali.

Stay tuned and keep on visiting this thread!!


===============
UPDATE
===============


 
Mkubwa tunakusubiria bila shaka kabisa Kubota; kwani hakika ni na imani ni mbinu mbadala kabisa unakuja nayo mkubwa wangu! Hii uzi ninaisave left kabisa nikitegemea newz toka kwako! Asante sana! Hapa ndiyo Jf jamani!





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…