Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Kwa utotoaji wa kuku wa kienyeji kwa uhakika tumia incubator za kutoka brinsea uk ambazo zinapatikana golden ball tanzania ltd mkabala na wizara ya mifugo .
 
Kuna Hili la Mbegu za Mapapai kutumika kutibu, Minyoo ana Ugonjwa wa fatal Coccidiosis, na utumiaji wa Mbegu uligunduliwa Huko Togo na wafugaji wa Kuku wa Togo wanatumia sana Mbegu za Mapapai
 
JF itakuwa na maana kama mada kama hizi na nyinginezo zilizo "KICHWA" zitakuwa zikipamba "NEW POST" na si mada ambazo hazina maana!!!
 
Mama Joe nashukuru sn jamani!
Na hakika maagizo yako nitayayafanyia kazi na nitarudisha majibu.


 
Last edited by a moderator:
Kwa utotoaji wa kuku wa kienyeji kwa uhakika tumia incubator za kutoka brinsea uk ambazo zinapatikana golden ball tanzania ltd mkabala na wizara ya mifugo .

Mkuu na bei yake in range vp? Kwa incubator ndogo kabisa?

Sent using wireless by wire
 

Au unachanganya damu na pumba
 
Ndugu zangu mimi ninapata tabu sana ninapotaka kuwatengenezea kuku wangu funza au mchwa kwani bado sijaelewa vizuri namna ya kuwatengeneza hawa wadudu.naomba mwenye ujuzi huo anipige msasa kidogo.
mama timmy mimi si mgeni sana hapa jf.Huwa si comment chochote nachukuwa tu maujuzi.Ila nimeona nitoe mchango wangu kwa hili.Tafuta kinyesi cha ng'ombe cha tumboni (inabidi upate aliyechinjwa) jaza kinyesi kwenye mfuko wa rambo,funga mfuko vizuri,chimba shimo,fukia na uache kwa muda wa week 1 then fukua utakuta funza wakubwa sana. n.b. Nimeelekezwa sijajaribu.
 
Kubota, Mama Joe, Mama timmy, guta Hii picha ni ya kifaranga cha kuku wangu nimeipiga leo, Vilikuwa vifaranga 30 kimebaki kimoja nacho ndio hiki kiko hoi. Chanjo zote nilishawapa na dawa njingi zikiwemo za mafua na antibiotic kadhaa lakini wapi ugonjwa huu umeng'ang'ania. umeua vifaranga vingi sana na baadhi ya kuku wakubwa. Pia ugonjwa husabisha kuku kutoa udenda wakati fulani na huisgiwa nguvu za miguu pia. Naombeni ushauri maana huku niliko kijijini na ni kama vile bwana mifugo wetu hapa bush kaishiwa na utaalam katika hili kanishauri mara kadhaa bila mafanikio.


Kifaranga hiki ni chotara wa jogoo wa Malawi na tetea wa kienyeji.






Ukiangalia vizuri unaona kama kishwa pia kama kimevimba sijiu nini tatizo.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana popiexo , magonjwa ni tatizo kubwa sana kwa vinyoya, kwa haraka haraka naweza kusema kuna wakati kuku wangu walikuwa wanatoa udenda na kupiga kama tyafya, pia kinyesi chao kilikuwa cha kuhara, niliwapa dawa ya vitamin introvit A+wf na vetoxy 20 wakapona, nilikwenda pale kariakoo sokoni nikanunua.

Lakini kwa sasa hata mimi nahangika na vinyoya nimewapa dawa aina nyingi lakini wanaendelea kupukutika tu. sijajua kwanini vinyoya hawa respond vizuri kwenye dawa. ila kuna mtu kanishauri kuzingatia lishe bora kwenye hawa vifaranga. kama vichwa vinavimba ni dalili ya kuwa na lishe isiyo na ubora. Pia soma thread hapa zina ushauri mbalimbali, Kubota, Mama Joe, Mama timmy wameeleza sana kwenye magonjwa hapo waweza zamia.

Ufuatayo ni ushuri nilopata kutoka kwa Dafo ;

Sawa mkuu Guta.naomba nikiri kwanza mimi sio mtaalam wa mifugo ila naongea kutoka na uzoefu wangu kwenye ufugaji na hobby niliyonayo katika ufugaji.katika ufugaji hasa wa kuku hiki kipindi cha kuanzia siku 1 hadi wiki ya 4 kuna changamoto sana.na katika kipindi hicho ndio kuku na mazao yaliyobora yanapo andaliwa, kifaranga asipotunza vizuri ni uwezekano wa kutoa mazao bora ni mdogo sana.vifaranga uwa wanasumbuliwa sana na homa za matumbo kama fowl typhoid, coccidiosis etc. kipindi hicho.ugonjwa wa mdondo ndo ugonjwa unaofahamika na wafugaji wengi sana hata wale ambao hawajawahi fuga kuku uwa wanausikia sana huu ugonjwa na sifa kubwa ya huu ugonjwa uwa unasababisha vifo vingi sana na hauna tiba ingawa ukienda kwa watalaamu wanaweza kukupa antibiotics ili kupunguza madhara na baadhi ya kuku wakapona.hivyo basi inashauriwa kuwachanja kuku siku ya 3, siku ya 21 na kila baada ya miezi mitatu.(assumption ni kuwa chanjo ina ubora, umezingatia masharti ya kuchanja na pia usichanje kuku mgonjwa)..baadhi ya dalili za ugonjwa huu kuku husinzia, anakua hali vizuri, hachangamki.
Ugonjwa huo wa kuharisha machano ni dalili ya ugonjwa matumbo na hii ndio dalili kubwa mara nyingi vifo vinakuwa sio vingi kwa muda mfupi.
NB: mara tu uonapo kuku mgonjwa haraka iwezekanvyo mtenge usisite kufanya hvyo mapema na inashauriwa kwa haraka pia uende ukamuone watalaamu wa mifugo kwa ushauri usipende tu kukimbilia kutumia dawa.Pia nakushauri epuka kununua dawa kwenye haya maduka ya mtaani ambayo hayana watalaamu wanakuuzia tu kama wanakuuzia pen.
Pia katika ufugaji usafi wa vyombo na mazingira yao ni muhimu sana hasa vifaranga uwa hawataki kabisa unyevunyevu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Popiexo pole sana kwa kupukutika kwa vifaranga. Matatizo yaliyokusibu hayo ndiyo kisa cha mimi kuanzisha hii thread. Naomba uwe unarudia rudia kupitia masimulizi yangu utagundua ndiyo unamopitia wewe leo. Nakushukuru kuweka picha ya kinyoya inasaidia wasomaji kujua kinyoya ni kuku yupi. Huyo kinyoya anaonyesha dalili za ugonjwa wa kuvimba kichwa, ni ugojwa nilikuwa ninauponya kwa kupaka mafuta ya alizeti kichwani kwenye makovu au madonda. Baada ya muda mfupi sana uvimbe ulinywea na niliponyesha kuku wengi sana. Mafuta ya alizeti hadi leo ninayachukulia kama tiba mbadala!

Maelezo yako na muonekano wa picha ya kinyoya yanadhihirisha kuwa unakabiliwa na tatizo la lishe! Hata ukitibu magonjwa haita saidia sana iwapo hautatatua tatizo la lishe. Suala hili la uhusiano wa lishe na magonjwa nimeshalielezea sana kwenye masimulizi yangu. Na pia nimeelezea tatizo linalotokea unapofungia kuku ndani ! Picha zako zinaonyesha kuku wako hawachungi nje, wanategemea chakula kile tu unachowalisha wewe. Wafugaji wengi huwapa kuku wao pumba za mahindi tu. Ndugu zangu pumba pekee siyo lishe toshelevu hasa kwa kuku waliozuiliwa kuzurula, pumba huwa haina wanga wa kutosha wala protein ya kutosha achilia mbali vitamin na madini toshelevu.

Mimi hawa vinyoya nilikuwa ninawachanganyia mashudu, dagaa na pumba za mahindi. Suala la lishe duni tulitazame kuwa ndio chimbuko kubwa zaidi la magonjwa kwa kuku wa kienyeji kwa vile wafugaji wengi wanawabania sana kuwalisha vema hawa kuku. Haya yote nimeyaelezea huko nyuma kwa uwazi sana. Kuku wa asili hujitafutia chakula wenyewe maporini tunapoamua kuwafungia ndani tunazua balaa iwapo hatujui au hatuwezi kuwapatia balanced diet!

Mkuu Guta umetoa maelezo toshelevu kabisa kwa tatizo linalomsibu Popiexo. Wadau, humu JF kwa upande wa maelezo ya magonjwa na tiba zake nadhani hakuna ambacho hakijaongelewa ni budi tu kuzipitia thread mbali mbali zinazoongelea kuku wa kienyeji na wa kisasa, kuna hazina kubwa ya utaalamu (ikiwamo magonjwa) kwenye thread zilizomo humu JF.
 

ata mm nina mpango huo lakin nimeweka budget ya min incubator ya mayai60 ni dola kama mia2 ivi ila uhakika wa umeme ndio shida.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana wadau ila tusonge mbele, Kubota asante kwa pongezi. Niliona umetaja tiba mbadala nyingi je mafua ya kuku yanayo kinga au tiba unayoifahamu?

Ndugu yangu kama unapilipili mbuzi ukiwarushia inasaidia sana kupunguza kasi. Nilikuwa ninamashina la pilipili mbuzi niyapanda pamoja na maua, (unajua pilipili mbuzi ikianza kuiva hupendeza sana), ulipotokea ugonjwa kuku maana walikua ni vijogoo wa kuku wa mayai nilinunua Tazara, walikuwa wanapiga chafya na kitu kama kwikwi nilikuwa nawarushia pilipili kwa wingi walipokuwa wakizidonoa nilikuwa nikiingia bandani hadi mwenyewe napiga chafya. Ilisaidia sana.
 
Dah Kubota asante sana huu nao huwa unasumbua hata kuku wakubwa
 

Ahsante sana mkuu Kubota. Kuhusu tatizo la kutotoa, nilijitahidi sana kuhifadhi mayai sehemu penye hewa ya kutosha (Wazi) pasipo na unyevunyevu, na niliyaweka sehemu iliyochongoka kuwa chini.Chakula huwa nanua kilicho changanywa tayari sina uhakika kama kina madhara, pia huwapa mabaki ya chakula tunachokula. Kuhusu Jogoo sina hakika maana hapa siku za mwisho niliona akiharisha, sijui kama alikuwa na tatizo hilo hapo mwanzo kabla hawajaanza kuatamia maana alikuwa normal na amechangamka sana, na isitoshe awamu ya kwanza Jogoo huyuhuyu alitumika na akatoa mazao mazuri hawakuharibu mayai. Muda wa kuhifadhi mayai ndo ninawasiwasi nao, maana wametaga kwa muda wa siku kama 14 jumlisha 5 za kusubiriana kuatamia. Lakini hata ambao sikuwasubirisha nao pia hawajatotoa kiwango kizuri wameishia 2 au 4. Pia hawakuwa na pilika nyingi, nilihakikisha naweka dawa ya kuua wadudu, na walikuwa hawaingiliani, nakumbuka ni siku moja tu nilikuta kuku wawili wamebadilishana viota walipokuwa wametoka kula chakula. Lakini niliwarudisha kila mmoja na kwake. Mpaka hapo nadhani mkuu Kubota umenipata.
 
kubota et al,

mimi nina wale kuku vijiogoo nimewanunua kama pilot ya kujifunza ufugaji, jee hawa ni kama kuku wa kienyeji au wanakuwaje? pili naweza wafuga kienyeji?na tatu wanapokuwa wakubwa wanaweza kupanda majike au ni wa mboga tu?
 
nina kamtetea changu cha majaribio hapa,nimejaribu kutumia mbinu ya kukawekea mazingira ya kutotoka toka wakati wa kulalia mayai kwa kuhakikisha chakula na maji kinakuwa karibu anapo lalia, kupulizia dawa ya viroboto ktk kiota cha mayai pia sikuruhusu usumaufu wa aina yoyote.Lengo langu ni kuprove utotoaji utakuaje ?kuna wadau wamewahi elezea ukifanya hivyo kuku uweza kutotoa vizuri.

Baada ya kufanya hivyo matokeo yake ni mazuri kwakweli,ktk mayai kumi niliyo mwekea ametotoa mayai yooote tofauti na kawaida ambapo alikuwa anaweweza akatotoa mayai sita katika kumi au nane katika kumi na mbili/kumi na tatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…