Yes JELA YA WAPENDANAOMkuu hata mie nilipoona hii kitu nilishangaa sana,
Itabidi tuiite JELA YA WAPENDANAO tu au wasemaje???
Asante Mkuu tutalifanyia kazi.Wakuu woote habari zenu,
Nimeendelea kupita pita huku na kule na leo nimekutana na hii kitu toka kwa shamba darasa la mdau mmoja wa ufugaji wa kuku wa kienyeji na amenipa hinti moja muhimu sana,
Anadai kuwa yeye katika uchaguaji wa mayai ya kuatamisha ili kutotoresha kuna kitu anakizingatia sana. Anasema mayai ya kuku wa kienyeji yapo yanayobeba majogoo na yapo yanayobeba majike, Yanayobeba majogoo ukiyaangalia huwa ni makubwa kidogo ukilinganisha na mayai ya kuku majike. Na hapa ndipo anapoweza kucheza tricks zake ili kujua atatotoresha majogoo mangapi na majike mangapi, haendi kwa bahati nasibu kama wanavyofanya wafugaji wengi..
Kama anataka majike mengi, basi atachagua mayai yenye maumbo madogo madogo na kama atataka majogoo mengi atachagua mayai yenye maumbo makubwa makubwa tu.
Stay tuned nitaleta nyingine nilizozinyaka
Jamani wapendwa asante sana kwa michango mizuri Kubota and Asigwa I salute you! Yaani hapa nilikuwa nawaangalia kuku wangu na kuwaza kuna majogoo mbegu nimeipenda je nifanyeje ili iwe endelevu nikianza kutotolesha..... jinsi gani niwatenge ili mayai yatokane na kupandwa na mbegu hizi tu? naona majibu nimeyapata hapahapa..... Mungu awabariki sana. Kuhusu kujua tofauti ya mayai yatayototoa jogoo au tetea na mie hiyo niliisoma mahali inaelezewa hivyo. Asante kwa tiba mbadala tutazifanyia majaribio ingawa tayari mimi kila weekend ninawachemshia majani aidha ya muarobaini, mlonge au aloe vera.... sikuwa najua zinatibu nini hasa ila naona wako vizuri tu
Kusema kweli mlonge mie nimeujua sifa zake kwa binadamu kabla ya kutumika kwa kuku, unasifika kuwa una vitamin nyingi, unatibu magonjwa mengi, mwanzo nilikuwa ninawapa tu kama majani laini yaliyopo bustani, lakini nimekuja kuisoma kwenye "Mwongozo wa ufugaji bora kuku wa kienyeji" cha Heifer International kumbe kwa kuku unatibu pia magonjwa mbalimbali. Majaribio yangu ni nikiona dalili za kuku mmoja tu kuharisha na sio kuwa wagonjwa ninawapa wote mlonge kwenye maji lakini kawaida majani yake wanakula tu kama chakula pia kuongeza vitamin. Nimekopi baadhi ya mimea na tiba zake toka hicho kitabu ila ni vizuri mtu ukitafute na ukisome choteShukrani sana,
Vipi umewahi kujua mlonge longe unasaidia nini katika ufugaji maana naona watu wanautumia sana kwa kuku ila kila nnaye muuliza hana jibu....
Mama Joe asante Mkuu, yaani hii modification ya JELA imenisisimua sana.
Safi sana,Madawa ya asili yatokanayo na mimea yanayosaidia katika tiba na kinga za maradhi mbalimbali ya kuku. Sehemu za mimea zinaweza kuwa: Majani, Magome, Mbegu, Maua au Matunda Umuhimu wa kutumia tiba zenye asili ya mimea: Hupatikana kwa urahisi. Ni rahisi kutumia. Gharama nafuu. Zinatibu vizuri. Hazina madhara. Baadhi ya mimea inayotibu maradhi ya kuku: Mwarobaini (Majani, Mizizi, Magome): Hutibu magonjwa yafuatayo: Typhoid. Kuzuia Kideri. Kuhara. Mafua. Vidonda. Shubiri Mwitu (Aloe vera): Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12. Mchanganyiko huu unaweza kutibu: Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka)- inyweshwe kabla kwa kinga. Homa ya matumbo (Typhoid). Mafua (Coryza). Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). Mbarika (Nyonyo): Hutibu Uvimbe. Weka majani ya mbarika ndani ya majani ya mgomba kisha weka ndani ya jivu la moto, kisha kanda sehemu yenye uvimbe kwa kutumia majani hayo ya mbarika. Mlonge (Mlonje): Ina vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine. Mlonge hutibu: Mafua. Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). Homa ya matumbo Ini. Konfrei: Ina madini na vitamini nyingi. Hutibu vidonda na majipu. Ndulele (Dungurusi, Makonde, Tura/Ndula): Majani hutibu Minyoo. Matunda hutibu Vidonda. Papai (Majani): Chemsha magao mawili ndani ya maji lita 6 hadi ubakie na lita 1. Poza kisha chuja. Hutibu: Minyoo Mwembe: Majani magao mawili, ponda na chemsha ndani ya lita 6 za maji hadi ibaki lita 1. Wape kwa siku moja. Mwembe hutibu: Homa ya matumbo. Mafua. Kinga ya Kideri/Mdondo. Mpira: Chemsha majani au mizizi. Mpira hutibu: Tumbo Vidonda na majipu Minyaa (Cactus): Hii ni aina yenye majani manene-hadi kufikia nusu nchi na mapana hadi kufikia upana wa viganja viwili vya mikono. Minyaa hutibu: (Angalia inaunguza au kubabua). Vidonda. Ngozi. Uzazi. Pilipili Kichaa: Pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdonde (lakini mapema kabla maradhi kuingia).
Safi sana,
information nyeti sana hii kwangu.
Ngoja niingize kwenye vitendo maana mambo azuri ukiyaweka kwa vitendo ndio yananoga. Nashukuru sana kwa nondo hizi.
Mungu akubariki......
Kaaaaaaaaa Aza !!!! Hivi ni Aza mpya au yule yule wa enzi? Umefufuka? Dah!! Ni wewe Aza uliwahi kuchangia wakati tu inaanza thread hii? Ukawa unashangaa kuhusu pilika zangu za kuchora mayai na kuokota mayai ingia toka kwenye mabanda! Maswali yako yalinifanya nicheke sana. In fact kama Aza huyo ni wewe basi ni kati ya watu walionichochea sana kuandika. Niliipenda sana Avatar yako na maswali yako matamu, halafu ukapotea jiiiiiii, karibu tena Mkuuu.Kubota umenichekesha eti umejaliwa kuwa na maneno mengi,which is good mana hujui jinsi ulivosaidia ktk jamvi hili,apa ninaprint ujuzi wako na wadau wengine umu nipate kitu nisome...mana mie mvivu sana kusoma through computer au ktk simu macho yanachoka Ibra6 ao mbwa wako wagawe aseee watarudisha nyuma juhudi izi za kuku
mbarikiwe kwa ujuzi huu mliotoa
Kaaaaaaaaa Aza !!!! Hivi ni Aza mpya au yule yule wa enzi? Umefufuka? Dah!! Ni wewe Aza uliwahi kuchangia wakati tu inaanza thread hii? Ukawa unashangaa kuhusu pilika zangu za kuchora mayai na kuokota mayai ingia toka kwenye mabanda! Maswali yako yalinifanya nicheke sana. In fact kama Aza huyo ni wewe basi ni kati ya watu walionichochea sana kuandika. Niliipenda sana Avatar yako na maswali yako matamu, halafu ukapotea jiiiiiii, karibu tena Mkuuu.
Mkuu Suip maximum siku saba ! Isizidi hapo maana yakikaa sana hata kama ikitokea kwa bahati yai likatotolewa kifaranga kinakuwa dhaifu sana kisiweze ku-survive.Kubota nimependa hii mada yako kuhusu mbinu zako za ufugaji wa kuku wa kienyeji,naomba unifahamishe ni muda gani au siku ngapi mayai yaliyohifadhiwa yanafaa kuatamiwa yasije ku- expire.
Wakuu Kubota, Mama Joe, asigwa, Chasha na wengine naombeni mwongozo (mambo ya kuzingatia) nikitaka kununua incubator, nahisi nitaihitaji muda si mrefu. Ila sasa nachanganyikia ipi ninunue! kwa mawazo niliyopata humu so far ni kwamba nzuri ni automatic, sasa kimbembe hizo automatic zenyewe zipo za kumwaga! nimesikia kuna za china, Uk etc, wengine wanaenda mbali zaidi wanadai za chini usinunue, wakati huo huo tunaambiwa vitu vingi vibovu na imara vinatokea huko huko china. Kifupi kwa sisi tusio na ufahamu nzuri wa hizi mashine tunazidi kuchanganyikiwa!
Haya, hapo hapo bado nasikia zinatofautiana uwezo sijui ukubwa, manake nimesikia mdau anatangaza anazo za UK za mayai 64 na mayai 176 kama sikosei, cha ajabu baadhi ya wadau akiwemo Mama Joe akahitaji ya mayai 200 au 300, hapo hapo kuna mdau ameibuka anataka ya 540 daah! mi hapo ni kuchanganyikiwa kwa kwenda mbele.....!!
Wakuu mwenye uzoefu na hizi mashine atudondoshee ABC zake namna ya kupata kitu bora, hata kama unajua point moja tu ya kuzingatia we tumwagie hapa, tukiunganishe na za wengine tutapata kitu kamili, si mnajua hela zenyewe hizi za kudunduliza au mkopo halafu tena uingie mkenge, umejinyima weeee unaishia kununua incubator ya ovyo, inabuma baada ya muda tu au inashindwa kabisa kutoa matokeo mazuri, si tutapata pressure bure aisee!!!