Kwa Watakao hitaji Vifaranga wa Aina mpya ya Kuku ambayo ni imroved Kienyeji KARI wanaweza oda hii ni breed inayo taga mayai mengi kuliko kuku wa kisasda wa mayai
Ahsante sana rafiki yangu mama joe!twende pamoja , na tuweke uthubutu kwenye ufugaji wetu na tutafika pale tunapopatamani.wao wameweze wana nini hata sisi tushindwe?
Mkuu Suip maximum siku saba ! Isizidi hapo maana yakikaa sana hata kama ikitokea kwa bahati yai likatotolewa kifaranga kinakuwa dhaifu sana kisiweze ku-survive.
Mkuu hiyo stata kama iko standard unapaswa uwalishe hadi waote mnyoya ya ukubwa, yaani hadi manyoya ya kifaranga yatoweke, kipindi hicho huwa tunachukulia kifaranga kimevuka kipindi nyeti na kigumu. Nakushauri tafuta muda usome thread hii yote, nilipitia changamoto hiyo hiyo nikafanikiwa kuitatua na ndiyo chanzo cha kuanzisha thread hii! Kisha fuatilia kinga muhimu ya chanjo kwa vifaranga na madawa mengine. Mkuu nilipokusoma tu kuwa uliacha kuwapa stata baada ya wiki mbili, hili ni jibu tosha kuwa kinachokusumbua ni Lishe. Walishe hiyo stata mwezi mzima au hadi wiki 6 baada ya hapo unaweza kuwapatia chakula chako cha kutengeneza mwenyewe napo usiwabadilishie ghafla, anza kuchanganyia taratibu na hicho ulichotengeneza. Naomba utulie usome thread nzima upate maarifa, ufumbuzi wa tatizo lako ni kujifunza zaidi. Narudia tena soma Thread hii kuhusu changamoto nilizokutana nazo za lishe na magonjwa na ufumbuzi niliofikia itakupa mwanga zaidi.
Wataalam Kubota, Liver mwenzangu na wengineo. Nimeanzisha ufugaji wa kuku wa kienyeji baada ya kuhamasika sana na huu mkanda. Nina kuku tetea 10 jogoo 1 hapo ni vp jogoo na mtesa au anatosha kwa kazi yake? Nina kanga 4 nimewachanganya kwenye banda moja na kuku je kuna athari yeyote? Maana athari ninayoona kwa sasa ni kanga kula mayai kila kuku wa kitaga. Je hawa kuku nimewanunua Tanga miezi miwili iliyopita je jina haja ya kuwapa chanjo kwa sasa hivi? Ni hayo tu wataalam wangu naomba msaada kujuzwa. Mengine yatafuata taratibu kutokana na mazingira nitakayokuwa naona.
Kama hauna hakika na huko ulipowatoa ni vyema kuwapatia chanjo,ugonjwa wa Newcastle Disease ni hatari unapowakumba kuku utauchukia ufugaji,
Jamani hali siielewi kuku wangu wa 2 wamevimba macho upande mmoja tatizo ni nini? Maana nimewapa chanjo ya ndui na pia otc baada ya siku 5 kutoka chanjo. Ila hali inanitia shaka, kuku wanakula na kupiga mishe zao kama kawaida. Wadau wenzangu naomba msaada wenu hapo.