Jubilant nimekutumia kwenye private message yako ya JF
nami naomba unipm contact zenu mkuu,
nina eneo nahitaji anzisha hii biashara ya kuku wa kienyeji lakini umenitisha kusema wana ukuaji hafifu hivyo nashawishiwika kuhamia kwenye chotara
Kazi kweli, Hao kuku wana nini special cha kuwafanya wasipatikane Tanzania? na Je ina maana kuku wa kisasa wa mayai akiwekewa Jogoo, hili yai halitatotorewa?
Habari zenu wana jamii forum.Nimefurahishwa sana na mjadala huu kuhusu ufugaji wa kuku.Shukrani za pekee zikufikie kaka Kichwa mbovu kwa elimu uliyotupatia,nimechukua contacts zenu ninaahidi kukutafuta.
Hawa kuku mheshimiwa ni kuku maalum,kazi kubwa imefanyika kwenye kutengeneza kosaafu yake.Mara nyingi kosaafu hizi hutengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu ambayo sisi watanzania na waafrika kwa ujumla hatuna utaalamu huu.Hata kenya ambao wanasupply kuku wazazi wa nyama kosaafu zake hawatengenezi wao,wanachofanya wao wanaagiza Grand parent stock kutoka Uingereza then wanaangulisha parent stock na kuwauza.Hawa kuku wa mayai wa kawaida wakiwekewa jogoo, mayai yake yanatotorewa lakini vifaranga wake wanakuwa dhaifu na hufa ovyo kwa kuwa ile kosaafu haikuandaliwa kwa ajili ya kutoa mayai ya kutotorewa isipokuwa ni ya kuliwa tu.Kuku hawa ni hybrid ambayo haifai kuwageuza parent stock
Mtaalamu vipi mnaweza kuwa contracted kwa hapa Dar kuangalia kuku wa mtu na rate zenu zikoje kwa mwezi, yaani unatoa ushauri kwa kufanya visit kwenye banda at least twice or thrice per month na kushauri kuhusu ukuaji, chakula, chanjo, dawa na mengineyo. Au in case of emergence. Gharama zenu?
Asante sana ni pm contact zako nikutafute mwisho wa mwezi huu ninapoanza.Nakushukuru mama Joe kwa kunipa likes,hii inaonyesha una appreciate kile ninachofanya kwa niaba ya wenzangu.
Kuhusu kuwa contracted inawezekana na huwa tunafanya,mara nyingi visiting inafanyika mara 1 kwa mwezi kwa ajili ya kumonitor maendeleo ya mradi, kwa case ya emmegence hapo any time haiangalii ratiba, gharama ni negotiable, kwani lengo ni kuwafanikisha watu watimize malengo yao. Mara nyingi gharama zetu zinakuwa kubwa kidogo kwa mara ya kwanza unapotuita kwa ajili ya kukuconsult, lkn baada ya hapo unakuwa kama mwanachama wetu, hivyo utainjoy huduma kwa gharama nafuu.
Asante sana niPM contact zako nikutafute mwisho wa mwezi huu ninapoanza
Kitaalam vifo inatakiwa viwe 10% ya kuku wote uliowaagaziza.Mkuu habari!nimewahi kufuga vifaranga wa malawi kama 70 hivi ila kumekuwa na changamoto kubwa sana ya vifo vya vifaranga na kuwalea kwa ujumla katika kipindi cha wiki ya kwanza hadi ya tatu.katika muda huo vifo vilikuwa vingi sana.kitalaamu idadi vifo ambavyo vinakubalika ni asilimia ngapi vinginevyo ni kuwa kuna tatizo.Asante mkuu.
Mkuu nina matumaini kuwa una ujuzi na ufugaji wa kitimoto pia
Yes,nina uzoefu pia kwani ni sehemu ya mafunzo niliyoyafanya nikiwa chuo,but kwa Imaani yangu sishughuliki na hawa kitimoto.