Alichosema chasha ni sahihi kabisa,mashine zinazotengenezwa hapa nchini ni usanii tupu,watengenezaji hawako serious na kazi.Kuzinunua ni kutupa pesa tu pasi na sababu yoyote ya maana.Hata hizi zinazotumia umeme bado ufanisi wake ni mdogo sana kiasi kwamba haziwezi kukupa faida.Kama uko serious na kazi pata machine kutoka nje ya nchi,mfano China au Italy huko utapata za uhakika.Kisha nunua generator kwa ajili ya emergence hapo utatengeze pesa,haitakiwi kufanya biashara kwa kubahatisha.
Chasha asante sana kwa ushauri wako, ukiwakuta hao watengenezaji wa kibongo jinsi wanavyozifagilia nane nane utasema nimepata.
Mkuu tunashukuru kwa elimu unayotupatia.mimi niliweka vifaranga wa malawi na katika siku ya kwanza hadi ya tano niliwapatia mchanganyiko huu glucose,otc plus na trimazin.je natakiwa kurudia tena mchanganyiko huu kwenye hiyo siku ya 16? Pia, vifo vilikua vingi na baadhi ya dalili ulizozitaja kama kushusha mabawa,kusinzia niliziona nikawapatia ctc20% je ilikuwa sahihi? Na kama kuna nyongeza juu ya hili nitashukuru zaidi.
Asante
Mkuu Kichwa vipi kuhusu Chakula cha Kuku hao Chotara na wakienyeji na lazima kiwe Pure na cha hawa kuku wa kisasa? na kwenye kutamisha mayai ukitumia ile njia ya Kuchagua sex ya mayai unaweza fanikiwa kutotoresha Majogoo tupu au Majike tupu?
Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajiriwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.
Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.
Karibuni kwa mjadala.
Mkuu Kichwa Mbovu
Ni vifaranga wa mayai toka Kampuni gani una recommend mtu kufuga? Vifaranga ambao hawafi sana na wanataga vizuri
Mh. Sabayi,suala la kampuni ni preference ya mtu but kwa upande wangu makampuni ambayo naprefer ni Interchicks,Mkuza,Matembwe-Njombe na Taasisi ya elimu kibaha kwa layers na kwa Broilers Amadori.
Hapo ilitakiwa utumie Vitalyte ikichanganywa na hiyo trimazin 30% na ni lazima urudie siku ya 16-20. OTC plus inatakiwa ijitegemee kwani ina Antiobiotics na vitamin.Inapendekezwa OTC Plus itumike siku ya 24-27 ili kuwakinga dhidi ya magonjwa mbalimbali na kuwafanya wawe na afya njema.Kwenye ctc 20% hukuwa sahihi,dawa hii inawafaa zaidi kuku wakubwa.
Mkuu hivi kuna Kampuni zinazo uza Incubatos za kutoka Nje unazo zifahamu? Make naona mauza uza tu,
Ndio mheshimiwa Chasha nina mawasiliano na makampuni kama matatu hivi yanayotengeneza kuuza Incubator,moja kutoka Uingereza,nyingine kutoka Italy na ya tatu kutoka China.Wengi niliowafanyia mpango na kuagiza hizo Incubators waliagiza kutoka china.Italy na Uingereza mashine zao ni ghali sana.
Nashukuru sana mkuu.pia kuna baadhi ya vifaranga kama watatu wa umri wa wiki 5 wamkua wakivimba jicho je hii ni dalili ya upungufu wa vitamin au ugonjwa mwingine?? na nawezaje kuzuia hiyo hali??je ni sahihi kutumia vitastress badala ya vitalyte?asante
Mkuu Kichwa mbovu asante sana kwa hii elimu unayotupa, ingawa jina yako humu JF haiendani na nondo hizi.
Mimi nafuga kuku wa mayai (kisasa) 550, wiki ya 12 sasa, pia nafuga kuku wa kienyeji sio chotara, kwa nje. Huwa nawatreat wote (layers na wa kienyeji) na wanarespond vizuri na sijapata scare ya magonjwa. Kuku wa kienyeji wamerespond vizuri as nilianza nao 10 tu ila wanatagiana na kuangua vifaranga sana ninao sasa kama vifaranga 40, wa saizi tofauti wengine wakubwa na wadogo, nimewaacha na mama zao maana nilijaribu kuwafungia wenyewe na kuwalisha , hawa vifaranga, hawakurespond vizuri. Nawafungia na mama yao kwa muda (kunguru nouma) alafu nawaachisha mama zao wakatage tena. Nafugia kwenye compaund yangu eneo la 30 by 60 enclosed walls.
Swali: Nafikiria kuleta majogoo ya chotara, ili wapande hawa kienyeji nipate kuku bora kwa ajili ya kuuza nyama, yaani niachane kiasi na pure kienyeji. Nia yangu mayai yakitagwa yatamiwe na hawa wa kienyeji ili nitoe vifaranga vikue niuze kuku wa nyama, kwani wa kienyeji maumbo madogo kama usemavyo. Sasa kwa baadhi majibu uliyokuwa unatoa kwenye hii mada nimepata ujumbe kuwa lazima nipate parent stock kutoka nje? au sikukupata vizuri? kwamba haya mayai mpaka yawe treated lasivyo vifaranga havitakuwa na afya? lakini ni wa kienyeji ndio wanataga sio hawa chotara....bado sijafikia hatua ya kutotolesha na mashine...Natanguliza shukrani, Mola akubarik zaid,
Hongera mheshimiwa Madago kwa kuendesha huo mradi wa kuku wa mayai na wa kienyeji.
Kuhusu majogoo ,ni vyema ukapata ya kisasa kabisa yani pure mfano majogoo wekundu Rhode Ireland red au wale Barred polmouth rock au hybrid yake hawa majogoo ambao ni kaka wa hao kuku wa mayai.Ikikosacross inakusaidia kuboresha ile kosaafu yako na kukuwezesha ufuge kibiashara na kupata faida.
Kwa huo mradi wako wa kuku wa kienyeji huna haja ya kuwa na parest stock wala kutreat mayai kwani project yako ni nndogo.Dawa za kutibia mayai ni ghali kidogo inahitaji wale wenye miradi mikubwa ya utotoreshaji.Utibuji wa mayai huongeza kiwango cha utotoreshaji wa idadi ya mayai,pia huzuia magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa mama kwenda kwa vifaranga.Na pia huwafanya vifaranaga wanaozaliwa kuwa wenye afya wakubwa na wenye afya njema.
Wale vifaranga ilitakiwa uwawekeechanzo cha joto pia uwape zile dawa za kuzuia magonjwa ya vifaranga mfano Ugonjwa wa pullorum na coccidiosis Na pia wangepatiwa chonjo ya mdondo pamoja na Gumboro.
Mkuu hapo kwenye Red, kwani nilazima kuwe na Mradi mkubwa ndo Utibu Mayai? nikiwa natotoresha mayai 1000 sihitaji kutibu hayo mayai?