Mkuu Kichwa mbovu asante sana kwa hii elimu unayotupa, ingawa jina yako humu JF haiendani na nondo hizi.
Mimi nafuga kuku wa mayai (kisasa) 550, wiki ya 12 sasa, pia nafuga kuku wa kienyeji sio chotara, kwa nje. Huwa nawatreat wote (layers na wa kienyeji) na wanarespond vizuri na sijapata scare ya magonjwa. Kuku wa kienyeji wamerespond vizuri as nilianza nao 10 tu ila wanatagiana na kuangua vifaranga sana ninao sasa kama vifaranga 40, wa saizi tofauti wengine wakubwa na wadogo, nimewaacha na mama zao maana nilijaribu kuwafungia wenyewe na kuwalisha , hawa vifaranga, hawakurespond vizuri. Nawafungia na mama yao kwa muda (kunguru nouma) alafu nawaachisha mama zao wakatage tena. Nafugia kwenye compaund yangu eneo la 30 by 60 enclosed walls.
Swali: Nafikiria kuleta majogoo ya chotara, ili wapande hawa kienyeji nipate kuku bora kwa ajili ya kuuza nyama, yaani niachane kiasi na pure kienyeji. Nia yangu mayai yakitagwa yatamiwe na hawa wa kienyeji ili nitoe vifaranga vikue niuze kuku wa nyama, kwani wa kienyeji maumbo madogo kama usemavyo. Sasa kwa baadhi majibu uliyokuwa unatoa kwenye hii mada nimepata ujumbe kuwa lazima nipate parent stock kutoka nje? au sikukupata vizuri? kwamba haya mayai mpaka yawe treated lasivyo vifaranga havitakuwa na afya? lakini ni wa kienyeji ndio wanataga sio hawa chotara....bado sijafikia hatua ya kutotolesha na mashine...Natanguliza shukrani, Mola akubarik zaid,