Habari yako mkuu,
Tafadhali ninaomba uni-PM kitabu cha ufugaji wa kuku wa kienyeji maana mie nae ni mfugaji ila napata changamoto sana juu ya hili
Nashukuru sana na ubarikiwe...
Mradi wa kuku ni mzuri haswa pale ambapo unakuwa na uzoefu wa jinsi ya kuwatunza na kufuatilia soko lake. Kwa mtizamo wangu naona kama unapendelea zaidi kuku wa nyama ambao kiasi fulani ni wagumu kuliko kuku wa mayai.
Ni muhimu ukiangalia yafuatayo kwa ustawi wa kuku wa nyama.
1. Kuwa na banda zuri lenye hewa ya kutosha pamoja na joto la kutosha (unaweza kupata vitabu kutoka kenye veterinary mbali mbali). Banda ni wastani wa mita 4 kwa 4 kwa kuku 200 wa nyama au 100 wa mayai. Hakikisha banda ni safi na umelipulizia dawa kabla ya kuingiza kuku (unaweza kutumia detto).
2a. Kwa mtu unaeanza ni vizuri kutumia chakula cha kiwandani kwa ubora kwani mara nyingi vyakula vya kujitengenezea vinaweza kuwa ma upungufu au kutengeezwa katika mazingira yasiyo mazuri na hatimaye kuwa na matokeo duni. Kumbuka wanahitaji vakula veyenye virutubisho tofauti kulingana na umri (mfano starter & finisher kwa broiler)
2b. Hakikisha wanapata chanjo ya newcastle wiki ya pili kwa kukuwapya utakaowaleta. Ni muhimu sana. Pia viatamini na madini kama utakavyoshauriwa na watalamu wa mifugo
3a. Kama una uwezo mzuri ni vizuri kufuga kwa awamu. Mathalani wapishane kwa wiki 2, (yaani unaingiza kukuwapya kila baada ya wiki mbili). Hii inakupa nafasi nzuri haswa kupunguza gharama za malisho na nafasi, kwani kadri wanapokuwa ndivyo unavyoongeza nafasi ya banda. Kumbuka broiler.
3b. Hakikisha kuna vyombo vya chakula na maji vya kutosha. Kuku wa nyama hawahitaji kwenda umbali mrefu kutafuta maji, na viwe na maji pamoja na chakula wakati wote.
3c. Hudumia kuku wadogo kwanza, ndipo umalizie kwa wakubwa. Usafi ni muhimu sana. Kuwe na masodasti na hakikisha hakuna unyevu unyevu ili wasipate maambukizo ya magonjwa ya baridi.vifo vingi sana huweza kutokea. Ni vizuri ukahakikisha kuwa hakuna kuku wa kienyeji, kwani mara nyingi huwa chanzo cha magonjwa.
4. Soko ndio kichaa kikubwa katika biashara ya kuku wa nyama, na faida yote hupotea baada ya kukomaa endapo soko linakosekana. Jiandae vyema kama ikiwezekana baada ya kufikisha uzito stahili (baada ya wiki 5-6) unawachinja wote na kuwauza au kuwahifandhi ndani ya jokofu na kuwauuza taratibu.
Baada ya hapa unaweza kuangalia nafasi yako ya kukuwa na kuwa uzoefu kupanua biashara. Ushauri wa wataalamu ni muhimu sana kufanikisha malengo, ila pia kumbuka ubabaishaji ni mwingi Afrika!
Je kuna mtu anyejua bei ya incubator au zipi ni nzuri
Asanteni wa kuu kwa jibu
Incubator ya mayai 50 inapatikana wapi na kwa bei gani?
Je kati ya mayai 50 yote yanaanguliwa au inaweza kuwa asilimia ngapi?
Incubator. Zinapatikana ktk maduka ya agro vet . Na mm ni mmoja ktk watu wanaouza
Jinsi ninavyojua mimi pamoja na uzoefu wangu HAKUNA KUKU ANAYETAGA ZAIDI YA YAI MOJA KWA SIKU
But I stand to be collected if im wrong withverifiableevidence
Wadau,bado napokea maswali yenu ili tuweze kusaidiana,lengo watu tuweze kujiajili.Mungu akipenda nitaanza kutupia vitu vingi siku za usoni.
faiz jr,ukijenga banda la mbwa pembeni ya banda la kuku wa kienyeji kuna madhara yoyote? yaan mbwa ana vijidudu ambavyo vinaweza kuleta athari kwa kuku?
Incubator. Zinapatikana ktk maduka ya agro vet . Na mm ni mmoja ktk watu wanaouza
Mfano ni kuanzia mayai ngapi?
kiwango cha chini ni mayai ngapi
faiz jr,
Ikiwa utajennga banda la mbwa pembeni ya banda la kuku wa kienyeji,kuna madhara .Madhara yake ni kuwa mbwa ni chanzo cha kueneza wadudu aina ya viroboto na utitiri. Wadudu hawa wako katika kundi la visumbufu vya kuku,wana nyonya damu san.
Kwa hiyo ni muhimu mbwa wakawa mbali kidogo na unakofugia kuku.
Ndugu wana jamii forum, sasa ni wakati wa kuacha kulalamika, tunapaswa kujituma na kupiga kazi kwa bidii. Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa, kujiajiri kunatoa uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi. Kuajiriwa ni utumwa na kama utapiga hesabu vizuri utagundua kuwa kuajiriwa ni hasara na pia huzuia mtu kuitumia elimu yake ipasavyo hasa ukiajiriwa serikalini. Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.
Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk , kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini. Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.
Karibuni kwa mjadala.
Mkuu nashukuru kwa Ushauri wako,,mim mwenyew ni Graduate nimemaliza mwaka huu na sina appetite ya kuajiriwa. Namshukuru Mungu kanisaidia nikapata kamtaji kadogo na nimeamua kuanza kufuga kuku,, nimeanza na vifaranga 100 chotara kesho vinamaliza wiki 1,, Nitahitaj msaada wako sana bro,, kwa kuanza Naomba unijulishe dawa na chanjo nzuri za kuanza navyo,,,NIKO MPUNGUZI DODOMA!
Hallo Ngamba, Kuhusu kuwapimia chakula, kila kuku atahitaji gram 120, na wakifika miezi sita na kuendelea utawaongezea hadi gram 123 kwa siku na kuhusu utagaji, mara nyingi kuku hasa wa kienyeji huanza kutaga wakiwa na umri wa miezi 6.Niko na maswali machache 1. nina kuku wa kienyeji wana miezi 4 na nusu, nina shida ya kuwapimia lishe, je ni kiasi gani cha lishe niwapatie wako 14 2. ni umri upi kuku huanza kutaga? na jogoo umri upi sahihi wa kufanya kazi mrua?