Edward Chapa
Member
- Jun 30, 2012
- 72
- 12
NDUGU SMU, kazi yako iko ndani ya uwezo wetu.Tuna uzoefu na hiyo kazi.Kuna wapo ambao tayari tumekwisha waanzishia mradi kama wako na wamefanikiwa, kwa mfano kuna mteja ambaye tumemwanzishia mradi na kwa sasa,kila mwezi anatoa kuku 5000 na kuwapeleka sokoni.Yeye anatotoresha na kufuga kuku wa kienyeji.Kila kuku anauzwa kwa shs.10,000 kwa bei ya jumla,ebu imagine kuku 5000 ni sh. ngapi anatengeza,ukipiga hesabu hapo utaona kila mwezi anatengeneza milioni 50.Akitoa gharama,let say milioni 20,je kuna kuna kazi gani ambayo unaweza ukaearn milioni 30 kwa mwezi!Kwa hiyo kama utahitaji ufafanuzi zaidi nitumie namba yako kwenye private message nitakutumia yangu.
Kiwango cha chini ni ya mayai 60 ya kukuMfano ni kuanzia mayai ngapi?
kiwango cha chini ni mayai ngapi
Adataro, Katika ufugaji wa kuku mazingira yeyote yanafaa kwa shughuli ya ufugaji kitu cha msingi nyumba ya kuku iwe na ventilation ya kutosha. Ufugaji ni tofauti na kilimo cha mazao ambacha klila zao lina hitaji aina yke ya udongo. Kuhusu gharama nadhani huko nyuma ya huu uzi nimeongelea naomba jaribu kupotia ila ---- hutaelewa nitafute nitakuelekeza.Kwa anayejaribu kama ni kuku wa nyama anaweza kuanza na kuku 250 na wa mayai kuku 100. Masoko ya kuku Tanzania siyo shida kuna mahotel mengi,supermarket nk wote wanahitaji kuku. Ukuba wa mabanda pia unaweza kurefer nyuma nayo nimeelezea.Ningependa kufahamu kuhusu mazingira yanayohitajika kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa nyama(machotara). Nimeuliza hivyo ili isije ikatokea kuna mazingira mengine huwa siyo mazuri kuendana na hali ya hewa, udongo wa mahali nk. Pia kuhusu ufugaji wa kuku wa nyama ingependa kufahamu gharama(matji mdogo wa majaribio) inayoweza kutumika kwa ajili ya kuanzia. Kutokana na uzoefu wako Zantsan unaweza kufahamu kuwa mtu anayejaribu anaweza akaanza kwa kiasi gani. Mabanda ukubwa wake pia nk. Je hawana shida katika kujichanganya na mazingira mengine nje ya banda? Ningependa pia kufahamu kuhusu ushauri kimasoko.
Adataro, Katika ufugaji wa kuku mazingira yeyote yanafaa kwa shughuli ya ufugaji kitu cha msingi nyumba ya kuku iwe na ventilation ya kutosha. Ufugaji ni tofauti na kilimo cha mazao ambacha klila zao lina hitaji aina yke ya udongo. Kuhusu gharama nadhani huko nyuma ya huu uzi nimeongelea naomba jaribu kupotia ila kama hutaelewa nitafute nitakuelekeza.Kwa anayejaribu kama ni kuku wa nyama anaweza kuanza na kuku 250 na wa mayai kuku 100. Masoko ya kuku Tanzania siyo shida kuna mahotel mengi,supermarket nk wote wanahitaji kuku. Ukubwa wa mabanda pia unaweza kurefer nyuma nayo nimeelezea.Ningependa kufahamu kuhusu mazingira yanayohitajika kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa nyama(machotara). Nimeuliza hivyo ili isije ikatokea kuna mazingira mengine huwa siyo mazuri kuendana na hali ya hewa, udongo wa mahali nk. Pia kuhusu ufugaji wa kuku wa nyama ingependa kufahamu gharama(matji mdogo wa majaribio) inayoweza kutumika kwa ajili ya kuanzia. Kutokana na uzoefu wako Zantsan unaweza kufahamu kuwa mtu anayejaribu anaweza akaanza kwa kiasi gani. Mabanda ukubwa wake pia nk. Je hawana shida katika kujichanganya na mazingira mengine nje ya banda? Ningependa pia kufahamu kuhusu ushauri kimasoko.
Felmwaki, Uwezekano wa ujenzi wa banda la gharofa upo na wengi wanajenga kwa ajili ya matumizi mazuri ya eneo la ardhi. Hata hivyo, nilikuwa natakamani kufahamu kimo cha hilo eneo lako ambalo unataka kujenga banda la ghorafa, maana umesema una eneo la futi 7 upana kwa futi 14 urefu.Je kimo chake ni ngapi ili tuone kama kuna uwezekano ili kimo cha futi 2.5 kiongezwe kwakuwa ni kidogo sana kwenye banda. Kimsingi banda la kuku linatakiwa liwe na kimo ambacho kitamwezesha mtu kuingia hata kwa kuinama ili kuweza kutoa huduma mbalimbali kwa ajili ya kuku ikiwa ni pamoja na usafi. Hata hivyo kwa ujumla eneo lako ni dogo sana kuweza kufugia kuku. Kwa mfano eneo la chini kwa vipimo ulivyotoa utakuwa na uwezo wa kufuga kuku 160 wa nyama aina ya broilers na kama kuku wa mayai ni 50 tu. Na eneo la juu kwa mujibu wa vipimo vyako pia ni kuwa, kuku nyama wataingia 90 na Kuku wa mayai wataingia 30 tu.Salaam mimi natamani kufuga kuku kwa mfumo wa ndani lakini eneo langu ni dogo sana nimebakiwa na futi saba upana kwa futi 14 urefu, Je ninaweza kujenga mabanda madogo ya ghorofa kwa partition za upana wa futi 4, urefu futi 14 na kimo futi 2.5?
Coturnix, Kuku Chotara kimsingi wana uwezo wa kutaga hadi asilimia 75 kama watapewa matunzo mazuri. Kuku chotara hawana tofauti sana na kuku wa kisasa, kwani nao huwa hawaatamii mayai hivyo kuwafanya kutokuwa na mzunguko katika utagaji kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji. Ukiwalisha layers watataga vizuri zaidi ila hawazidi hiyo asilimia 75 kwa kuwa kuku hawa pia wanakuwa na zile trait za kuku wa kienyeji ambao wote tunajua kuwa kuku wa kienyeji sio watagaji sana kama walivyo kuku wa kisasa. Hivyo ile cross waliyofanyiwa na kuwa machotaro ndiyo iliyosaidia kuongeza uzalishaji hadi kufikia asilimia hiyo 75. Kitu cha kuzingatia ili watege vizuri ni management nzuri, ikiwa ni pamoja na kuwapa chakula kizuri na kudhibiti magonjwa. Kuhusu kuwaasi au castration kama ambavyo hujulikana kwa wengi, hiyo technologia kwa kuku bado haijaingia hapa kwetu nchini au inawezekana kama imeingia basi mimi siko aware nayo. Lakini kitu ambacho nafahamu ni kuwa bado tunatumia ratio ya 1:10 yaani jogoo mmoja kwa matetea kumi.Mkuu Zantsan hawa kuku chotara wanatabia ya kutoa wastani wa Mayai mangapi kwa mwaka au kwa kipindi fulani? je baada ya kutaga mzunguko mmoja hukaa muda gani na kuanza kutaga tena je nikiwalisha layers mash wanaweza kutaga mfululizo kama kuku wa layers na hapo hapo wakiwa wanapandwa na jogoo? je kuna uwezekano wa kuwahasi majogoo ili kuyanenepesha na ku-control male to female ratio bila kuondoa/kupunguza idadi ya majogoo bandani?
Faiz jr hilo siyo tatizo hata usiwaze sana kitu cha msingi mwongezee chakula chenye lishe kamili, inaonekana una mnyima chakulajogoo langu la kienyeji limeacha kuwika,je hilo linasababishwa na nini?