Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

NDUGU SMU, kazi yako iko ndani ya uwezo wetu.Tuna uzoefu na hiyo kazi.Kuna wapo ambao tayari tumekwisha waanzishia mradi kama wako na wamefanikiwa, kwa mfano kuna mteja ambaye tumemwanzishia mradi na kwa sasa,kila mwezi anatoa kuku 5000 na kuwapeleka sokoni.Yeye anatotoresha na kufuga kuku wa kienyeji.Kila kuku anauzwa kwa shs.10,000 kwa bei ya jumla,ebu imagine kuku 5000 ni sh. ngapi anatengeza,ukipiga hesabu hapo utaona kila mwezi anatengeneza milioni 50.Akitoa gharama,let say milioni 20,je kuna kuna kazi gani ambayo unaweza ukaearn milioni 30 kwa mwezi!Kwa hiyo kama utahitaji ufafanuzi zaidi nitumie namba yako kwenye private message nitakutumia yangu.

kaka nimesoma post zako ,nimevitiwa na elimu ya ufugaji wa kuku,naomba nikutafute ,
 
Mkuu hao kuku 500 0 wanachukua nafasi ya ukubwa gani? NA je ni wa kienyeji au kisasa?
 
Nina eneo kama ekari 2 kijiji cha kivinja B ambacho kipo kilometa 10 kutoka Jaribu Mpakani (njia ya kwenda Lindi). Napanga nifuge kuku wa mayai. sasa kwa uzoefu wako unadhani nianzie kuku wangapi amabo wanaweza kulipa kila mwezi - kwa maqana nipate mayai ya kutosha kuyaleta mjini Dar na kuyaiza kwa faida. Natanguliza shukurani.
 
Ningependa kufahamu kuhusu mazingira yanayohitajika kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa nyama(machotara). Nimeuliza hivyo ili isije ikatokea kuna mazingira mengine huwa siyo mazuri kuendana na hali ya hewa, udongo wa mahali nk. Pia kuhusu ufugaji wa kuku wa nyama ingependa kufahamu gharama(matji mdogo wa majaribio) inayoweza kutumika kwa ajili ya kuanzia. Kutokana na uzoefu wako Zantsan unaweza kufahamu kuwa mtu anayejaribu anaweza akaanza kwa kiasi gani. Mabanda ukubwa wake pia nk. Je hawana shida katika kujichanganya na mazingira mengine nje ya banda? Ningependa pia kufahamu kuhusu ushauri kimasoko.
 
Habari Ndugu Zantsan,

Nitumie na mimi contacts zako.

Hata mimi nataka kuanzisha ufugaji wa kuku.

Naanza mwanzo kabisa kwenye mabanda.

Nahisi nahitaji msaada mkubwa zaidi
 
samahanini wadau napenda kupata ushauri hivi nnao kuku wa kisasa wa mayai miambili hamsini je polo la chakula cha kg 50 nilishie kwa siku ngapi
 
Wafuatiliaji wote wa uzi huu, Msipate shaka labda kwa kuchelewa kuwajibu maswali yenu, wakati mwingine nabanwa kidogo na majukumu lakini nawafuatilia waulizaji wote nami muda si mrefu nitamjibu mmoja baada ya mwingine kama ilivyo ada.Kwa hiyo kama kuna maswali endeleeni tu kuyauliza.
 
Ningependa kufahamu kuhusu mazingira yanayohitajika kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa nyama(machotara). Nimeuliza hivyo ili isije ikatokea kuna mazingira mengine huwa siyo mazuri kuendana na hali ya hewa, udongo wa mahali nk. Pia kuhusu ufugaji wa kuku wa nyama ingependa kufahamu gharama(matji mdogo wa majaribio) inayoweza kutumika kwa ajili ya kuanzia. Kutokana na uzoefu wako Zantsan unaweza kufahamu kuwa mtu anayejaribu anaweza akaanza kwa kiasi gani. Mabanda ukubwa wake pia nk. Je hawana shida katika kujichanganya na mazingira mengine nje ya banda? Ningependa pia kufahamu kuhusu ushauri kimasoko.
Adataro, Katika ufugaji wa kuku mazingira yeyote yanafaa kwa shughuli ya ufugaji kitu cha msingi nyumba ya kuku iwe na ventilation ya kutosha. Ufugaji ni tofauti na kilimo cha mazao ambacha klila zao lina hitaji aina yke ya udongo. Kuhusu gharama nadhani huko nyuma ya huu uzi nimeongelea naomba jaribu kupotia ila ---- hutaelewa nitafute nitakuelekeza.Kwa anayejaribu kama ni kuku wa nyama anaweza kuanza na kuku 250 na wa mayai kuku 100. Masoko ya kuku Tanzania siyo shida kuna mahotel mengi,supermarket nk wote wanahitaji kuku. Ukuba wa mabanda pia unaweza kurefer nyuma nayo nimeelezea.
 
Ningependa kufahamu kuhusu mazingira yanayohitajika kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa nyama(machotara). Nimeuliza hivyo ili isije ikatokea kuna mazingira mengine huwa siyo mazuri kuendana na hali ya hewa, udongo wa mahali nk. Pia kuhusu ufugaji wa kuku wa nyama ingependa kufahamu gharama(matji mdogo wa majaribio) inayoweza kutumika kwa ajili ya kuanzia. Kutokana na uzoefu wako Zantsan unaweza kufahamu kuwa mtu anayejaribu anaweza akaanza kwa kiasi gani. Mabanda ukubwa wake pia nk. Je hawana shida katika kujichanganya na mazingira mengine nje ya banda? Ningependa pia kufahamu kuhusu ushauri kimasoko.
Adataro, Katika ufugaji wa kuku mazingira yeyote yanafaa kwa shughuli ya ufugaji kitu cha msingi nyumba ya kuku iwe na ventilation ya kutosha. Ufugaji ni tofauti na kilimo cha mazao ambacha klila zao lina hitaji aina yke ya udongo. Kuhusu gharama nadhani huko nyuma ya huu uzi nimeongelea naomba jaribu kupotia ila kama hutaelewa nitafute nitakuelekeza.Kwa anayejaribu kama ni kuku wa nyama anaweza kuanza na kuku 250 na wa mayai kuku 100. Masoko ya kuku Tanzania siyo shida kuna mahotel mengi,supermarket nk wote wanahitaji kuku. Ukubwa wa mabanda pia unaweza kurefer nyuma nayo nimeelezea.
 
Salaam mimi natamani kufuga kuku kwa mfumo wa ndani lakini eneo langu ni dogo sana nimebakiwa na futi saba upana kwa futi 14 urefu, Je ninaweza kujenga mabanda madogo ya ghorofa kwa partition za upana wa futi 4, urefu futi 14 na kimo futi 2.5?
 
Felmwaki, Uwezekano wa ujenzi wa banda la gharofa upo na wengi wanajenga kwa ajili ya matumizi mazuri ya eneo la ardhi. Hata hivyo, nilikuwa natakamani kufahamu kimo cha hilo eneo lako ambalo unataka kujenga banda la ghorafa, maana umesema una eneo la futi 7 upana kwa futi 14 urefu.Je kimo chake ni ngapi ili tuone kama kuna uwezekano ili kimo cha futi 2.5 kiongezwe kwakuwa ni kidogo sana kwenye banda. Kimsingi banda la kuku linatakiwa liwe na kimo ambacho kitamwezesha mtu kuingia hata kwa kuinama ili kuweza kutoa huduma mbalimbali kwa ajili ya kuku ikiwa ni pamoja na usafi. Hata hivyo kwa ujumla eneo lako ni dogo sana kuweza kufugia kuku. Kwa mfano eneo la chini kwa vipimo ulivyotoa utakuwa na uwezo wa kufuga kuku 160 wa nyama aina ya broilers na kama kuku wa mayai ni 50 tu. Na eneo la juu kwa mujibu wa vipimo vyako pia ni kuwa, kuku nyama wataingia 90 na Kuku wa mayai wataingia 30 tu.
 
Mkuu Zantsan hawa kuku chotara wanatabia ya kutoa wastani wa Mayai mangapi kwa mwaka au kwa kipindi fulani? je baada ya kutaga mzunguko mmoja hukaa muda gani na kuanza kutaga tena je nikiwalisha layers mash wanaweza kutaga mfululizo kama kuku wa layers na hapo hapo wakiwa wanapandwa na jogoo? je kuna uwezekano wa kuwahasi majogoo ili kuyanenepesha na ku-control male to female ratio bila kuondoa/kupunguza idadi ya majogoo bandani?
Coturnix, Kuku Chotara kimsingi wana uwezo wa kutaga hadi asilimia 75 kama watapewa matunzo mazuri. Kuku chotara hawana tofauti sana na kuku wa kisasa, kwani nao huwa hawaatamii mayai hivyo kuwafanya kutokuwa na mzunguko katika utagaji kama ilivyo kwa kuku wa kienyeji. Ukiwalisha layers watataga vizuri zaidi ila hawazidi hiyo asilimia 75 kwa kuwa kuku hawa pia wanakuwa na zile trait za kuku wa kienyeji ambao wote tunajua kuwa kuku wa kienyeji sio watagaji sana kama walivyo kuku wa kisasa. Hivyo ile cross waliyofanyiwa na kuwa machotaro ndiyo iliyosaidia kuongeza uzalishaji hadi kufikia asilimia hiyo 75. Kitu cha kuzingatia ili watege vizuri ni management nzuri, ikiwa ni pamoja na kuwapa chakula kizuri na kudhibiti magonjwa. Kuhusu kuwaasi au castration kama ambavyo hujulikana kwa wengi, hiyo technologia kwa kuku bado haijaingia hapa kwetu nchini au inawezekana kama imeingia basi mimi siko aware nayo. Lakini kitu ambacho nafahamu ni kuwa bado tunatumia ratio ya 1:10 yaani jogoo mmoja kwa matetea kumi.
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu wananiuliza juu ya Taaluma yangu, nimeona leo hii niandike hapa ili watu mnijue na muone uwezo wangu ulivyo. Kwanza kabisa mimi ni afisa mifugo, nina certificate of animal health and Production (yaani Astashahada ya afya ya wanyama na uzalishaji), nina Diploma of animal health (yaani Stashahada ya Afya ya Wanyama), na pia nina Bsc. Agricultural Economics and Agribusiness (yaani Shahada ya Sayansi katika uchumi kilimo na Biashara) ya chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo. Nina uzoefu wa masuala yote ya mifugo na Miradi kwa ujumla. Asanteni sana
 
Asante kwa kutoa nafasi ya kuuliza maswali mkuu.....mimi niliamua kuanza kufuga kuku wa kisasa wa mayai. Nina miliki kuku 199. Kwa sasa wako na umri wa wiki 27. Ni mgeni kabisa wa biashara hii. Katika mwongozo wangu inaonyesha wanatakiwa kutaga kwa 90% to 95 kwa sasa. Yaani mayai 179 mpaka 189 kwa siku. Lakini nazalisha wastani wa mayai 120 mpaka 130....nahisi kuna tatizo ingawa sijui nini shida..je nifanyeje niweze kuzidisha uzalishaji?
 
Hao kuku machotara wanapatikana wapi? au ni mpaka nitotoleshe mimi mwenyewe?
 
Back
Top Bottom