Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

mkuu mi nafuga bata, vipi niweza kukaribia?
 
Ankojei ="ANKOJEI, post: 15364066, member: 31431"]naomba unitumie meseji ya neno "kuku" kwenda +255 752 693 692
Ankojei nimekutumia bana kange ndomile leleno[/QUOTE]
Lutamyo we mmatengo au mpoto.
Panyambiki pa matengo bambo lighale nga kuchoka achoka derefa
 
Nimevutiwa na ushauri wako. nataka nianze kufuga kuku wa kizungu wa nyama. ndio nipo kwenye matayarisho ya banda.
 
Je wewe ni mtotoleshaji au unapenda kuwa mtotoleshaji wa Vifaranga wa kuku wa kienyeji walioboreshwa na unakosa vyanzo vya uhakika vya kupata mayai bora yenye mbegu? Kampuni yako ya KINASORU EAST AFRICA (T) LTD inakuhakikishia kupata mayai hayo kwa kiasi chochote utakachokihitaji. Huna haja ya kuhangaika kufuga mwenyewe. Tunakuuzia mayai na kazi ya utotoleshaji unaianza mara moja.

KINASORU EAST AFRICA (T) LTD inajivunia kuwa na mtandao mpana wa wafugaji au outgrowers ambao kampuni inawasimamia. Tuna jumla ya wafugaji (outgrowers) 60 Morogoro mjini, 30 Dodoma mjini, 1, Dakawa Mvomero . Tunaendelea kuwatengeneza outgrowers wengine katika mikoa ya Singida, Tabora na Ruvuma. Lengo letu ni kuwa na mtandao mpana zaidi wa wafugaji wa kuku wa asili walioboreshwa Tanzania kuweza kutosheleza soko la watotoleshaji.

Mfumo wetu wa biashara unatoa faida kwa mfugaji, kampuni yetu pamoja na mnunuaji.

Mfugaji yeye ananufaika kwa kupata uhakika wa soko mara baada ya kuku wake kuanza kutaga. Ananufaika pia na ushauri na huduma za ugani ikitokea kuku wake wanaumwa pamoja na madawa na chakula pale anapoishiwa chakula na kukosa pesa. Kwa maana nyingine mfugaji anawekwa katika mazingira ya uhakika na kazi anayoifanya.

Kampuni yetu inanufaika kwanza kwa kuwa na uhakika wa kupata mayai bora na yenye sifa ya kutotoleshwa kwa kiasi chochote tunachokihitaji na kwa wakati kupitia wafugaji wetu tuliowatengeneza na hivyo kutusaidia kutatua changamoto ya oda kubwa tulizokuwa tunazipata kutoka kwenye makampuni yanayozalisha kuku hao wa asili walioboreshwa. Vile vile tunapata faida ya kuaminiwa kwa kampuni yetu kutokana na kusambaza mayai yanayokidhi vigezo na kuwavutia wateja wetu wengi. Katika kuhakikisha kuwa Kampuni yetu inanufaika kidogo na mtandao wetu wa wafugaji kuku wa asili walioboreshwa, tunaongeza asilimia kidogo kwenye mayai tunayoyakusanya kutoka kwa wafugaji wetu, tunashukuru inatusaidia kupata chochote kwa ajili ya kuendesha ofisi yetu. Halikadhalika, tunauza vifaranga wa kuku wa asili walioboreshwa kwenye mtandao wetu wa wafugaji. Kwahakika Hakuna biashara isiyokuwa na faida.

Wateja wetu wa mayai tunawasaidia kutafuta masoko ya vifaranga wao kwenye mtandao wetu wa wafugaji na hata wale walionje ya mtandao wetu wa wafugaji ambao wanahitaji vifaranga bora kutoka kwenye kampuni yetu mara baada ya kutotolewa kutoka kwenye mashine. Kitu kingine, wateja wetu wa mayai wananufaika na elimu ya uanzishaji na uendeshaji wa mradi wa utotoleshaji wa vifaranga. Tunawafundisha na kuwaelekeza nini ufanye au vitu gani vya msingi uzingatie ili uweze kuanzisha mradi wa uzalishaji wa vifaranga. Je mayai kabla ya kuingizwa katika machine na kuanza kutotoleshwa yanatibiwaje? Kampuni yetu haikuachi peke yako itakufundisha kila kitu kitakachokufanya uzalishe vifaranga bora kabisa watakaokupa jina mtaani.

Kinasoru East Africa (T) LTD inafanya kazi ya kuwaunganisha wafugaji na wazalishaji wa vifaranga na kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa zinakuwa bora na zenye kukidhi viwango.

Huduma nyingine ambazo Kinasoru East Africa (T) LTD inazitoa ni kuuza vifaranga wa Mayai (Layers), Vifaranga wa Nyama (Broilers),na Vijogoo. Pia tunauza vichanganyia mbalimbali vya kutengenezea chakula cha kuku na mifugo mingine mfano Nguruwe. Tunasaidia wafugaji kupata masoko ya mifugo na mazao yake. Tunatoa semina za mafunzo ya ufugaji wa kibiashara na ushauri katika miradi inayohusiana na mifugo, ikiwemo Kuku au jamii zote za ndege, Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, Sungura, Nguruwe na Samaki. Tunatoa huduma za Vijana wa kusimamia mashamba ya mifugo, vijana wetu ni waadilifu na waliowafundishwa vyema usimamizi wa miradi ya ufugaji. Pia tunasaidia katika kuanzisha na kusimamia miradi ya wateja wetu. Tunafanya farm feasibility study na Farm Planinng. Tunatoa huduma zote za ugani mfano matibabu, ushauri wa ufugaji bora, uandaaji wa chakula cha mifugo na mpango wa ulishaji, tunasaidia ng'ombe kuzaa, tufanya upandishaji ng'ombe kwa njia ya chupa au Artificial Insemination nk.

Tuna wataalam na mifumo inayozesha utoaji wa huduma zetu kwa uhakika na kuwafikia wateja wetu popote walipo.

Ofisi zetu za KINASORU EAST AFRICA (T) LTD, Ziko Dodoma Mjini, Mtaa wa Nduka Chamwino Bonanza, Mbele Kidogo ya Soko la Maisha Plus.

Aman Ng'oma, Mkurugenzi Mtendaji Simu namba 0767989713, 0715989713 na 0786989713. E-mail: amanngoma@gmail.com

Karibu kwa huduma bora na za uhakika.
 
Kuku wa mayai ratio yak ni 6 kwa 1sqm.....kama unataka kufuga 500 x 6, mean uwe banda la 300sqm : Ingekuw kuku nyama hapo ungezidisha kwa 10: Kila la heri! Ila layers si lele mama ile miezi 6 mwanzo! Utapigika hasa!
 
Habari wandugu na poleni kwa majukumu ,Naomba msaada wenu na ushauri kuhusu kuku wa kisasa wa nyama ,jinsi ya kuwafuga tangu kuwapokea siku ya kwanza hadi kufikia kuwatoa.Chonjo zote na mpangilio wote wa kuwapa dawa na vitamin.
 
Za sahizi ndugu...
Naomba kujua mbegu nzuri ya kuku wa mayai .....
Kwani nataka kufuga kuku wa mayai ila nimeambiwa inabidinijue mbegu gani ni nzuri kwa kufuga hapa jijini DSM.

Asanteni
 
Wasiliana na mabwana mifugo ila pia unatakiwa uwe na mtaji wa kutosha ili kununua vyakula vya kuku ili washibe wapate kutaga zaidi
 
Mimi pia nahitaji. Mkuu Sirdirashy ungeeleza hapa kwa kifupi ungekuwa umesaidia watu wengi kwa wakati mmoja. Ni ombi tu.
 
Akutafute wapi sasa na yeye ameona hapa ndipo pahala anapoweza kupata msaada, we unamtaka aje faragha kunani?

Mkuu hajalazimishwa kunitafuta ni issue ya kuja tu private anipe email yake nimrushie huo muongozo basi hakuna lengine
 
Mkuu hajalazimishwa kunitafuta ulitaka niandike page 20 hapa siwezi kutoa mchanganuo wangu hapa wa biashara
Ni moyo tu mkuu, kwakua upo hapa kama mwana familia wa jf unapotoa msaada kwa mtu mmoja unakuwa umewasaidia wengi saaana kwa mara moja, hii itakuondolea usumbufu kwa kila mahitaji kukutafuta kwa wakati wake. Utaalam wako utusaidie na cc ambao tunahitaji kujifunza kupitia mada hii. Kama ni rukhsa kila atakae kukutafuta wala usijali, nita PM.
 
check kuroiler ni mbegu nzuri, wanatunza kama wa kienyeji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…