Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Wadau naombeni msaada wa elimu juu ya ufugaji wa kuku wa mayai, kuku wa kienyeji au wa kisasa. Kuanzia ujenzi wa banda, pamoja na changamoto zake.
 
Wadau naombeni msaada wa elimu juu ya ufugaji wa kuku wa mayai, kuku wa kienyeji au wa kisasa. Kuanzia ujenzi wa banda, pamoja na changamoto zake.
Pitia pitia humu ndani kuna thread kibao zinazojibu maswali yako.Kama umeanza kuwa mvivu mapema hivi jua umesha-fail.
 
Mkuu Karibu GMBD Consult ltd tunao uzoefu wa kutosha kuandaa michanganuo kutoa ushauri wa mradi wa kuku(broilers, layers, cross breeds n.k) pia tunao uzoefu wa kutosha kwenye kunenepesha ngombe(cattle fattening), ufugaji wa nguruwe n.k Tuna mifano mingi Korogwe 9 kilomtre kutoka Segera on the way to Moshi kuna shamba la nguruwe (400) na Kuku (6,000), Cattle fatterning in Mtibwa, e.t.c Pia tunao uzoefu wa kutosha kwenye animal feed processing(Dodoma - Mapusa Rajab), Mbezi Luis (M & M Food Procesor) e.t.c karibu sana. wasiliana nasi +255715 737302 au +255784 737302 ama kwa email info@gmconsultz.com pia tembelea website yetu www.gmconsultz.com
Website yenu .. ktk miradi mlofanya.. sijaona inayojihusiha na ufugaji... nakubali kusahihishwa..
 
Mradi wa kuku ni mzuri haswa pale ambapo unakuwa na uzoefu wa jinsi ya kuwatunza na kufuatilia soko lake. Kwa mtizamo wangu naona kama unapendelea zaidi kuku wa nyama ambao kiasi fulani ni wagumu kuliko kuku wa mayai.

Ni muhimu ukiangalia yafuatayo kwa ustawi wa kuku wa nyama.

1. Kuwa na banda zuri lenye hewa ya kutosha pamoja na joto la kutosha (unaweza kupata vitabu kutoka kenye veterinary mbali mbali). Banda ni wastani wa mita 4 kwa 4 kwa kuku 200 wa nyama au 100 wa mayai. Hakikisha banda ni safi na umelipulizia dawa kabla ya kuingiza kuku (unaweza kutumia detto).

2a. Kwa mtu unaeanza ni vizuri kutumia chakula cha kiwandani kwa ubora kwani mara nyingi vyakula vya kujitengenezea vinaweza kuwa ma upungufu au kutengeezwa katika mazingira yasiyo mazuri na hatimaye kuwa na matokeo duni. Kumbuka wanahitaji vakula veyenye virutubisho tofauti kulingana na umri (mfano starter & finisher kwa broiler)

2b. Hakikisha wanapata chanjo ya newcastle wiki ya pili kwa kukuwapya utakaowaleta. Ni muhimu sana. Pia viatamini na madini kama utakavyoshauriwa na watalamu wa mifugo

3a. Kama una uwezo mzuri ni vizuri kufuga kwa awamu. Mathalani wapishane kwa wiki 2, (yaani unaingiza kukuwapya kila baada ya wiki mbili). Hii inakupa nafasi nzuri haswa kupunguza gharama za malisho na nafasi, kwani kadri wanapokuwa ndivyo unavyoongeza nafasi ya banda. Kumbuka broiler.

3b. Hakikisha kuna vyombo vya chakula na maji vya kutosha. Kuku wa nyama hawahitaji kwenda umbali mrefu kutafuta maji, na viwe na maji pamoja na chakula wakati wote.

3c. Hudumia kuku wadogo kwanza, ndipo umalizie kwa wakubwa. Usafi ni muhimu sana. Kuwe na masodasti na hakikisha hakuna unyevu unyevu ili wasipate maambukizo ya magonjwa ya baridi.vifo vingi sana huweza kutokea. Ni vizuri ukahakikisha kuwa hakuna kuku wa kienyeji, kwani mara nyingi huwa chanzo cha magonjwa.

4. Soko ndio kichaa kikubwa katika biashara ya kuku wa nyama, na faida yote hupotea baada ya kukomaa endapo soko linakosekana. Jiandae vyema kama ikiwezekana baada ya kufikisha uzito stahili (baada ya wiki 5-6) unawachinja wote na kuwauza au kuwahifandhi ndani ya jokofu na kuwauuza taratibu.

Baada ya hapa unaweza kuangalia nafasi yako ya kukuwa na kuwa uzoefu kupanua biashara. Ushauri wa wataalamu ni muhimu sana kufanikisha malengo, ila pia kumbuka ubabaishaji ni mwingi Afrika!
Shule yenye uhalisia.... udadisi wangu mdogo ktk kuanza mradii mdogo wa hii makitu.. nakutana majibu... yananipoteza kabisa..
 
Naomba mchanganuo wa gharama/ mahitaji ya kufuga kuku wa kisasa broilers nataka kuanza na vifaranga 100

Naomba kujua gharama za
Vifaranga
Chakula cha kuku
Chanjo/dawa
Banda
Mahitaji mengine
 
Wadau naomba kujua ni wapi naweza kujifunza ufugaji wa kuku, na samaki hapa Dar
 
Hey JF Members.

Ee bwana kuna mtu anaweza kunipa msaada wa mchanganuo wa kufuga kuku. Naona soko la kuku ni kubwa sana. Hii ni biashara ambayo soko lake liko tayari. hotels, functions, vibanda vya chipss.. Yeyote mwenye idea naomba msaada please!
Habari kwa MTU yeyote mwenye interest ya kufuga kuku Nina banda tegeta masaiti nakodisha,banda na vyombo vyangu vya kuku na machine ya kunyonyoa manyoa.mwenye interest ya kufuga kuku anakaribisha kuona.whatssap 0786057996/call 0756661761.
 
Mkuu we ni mfugaji au unataka kunza kufuga maana si kuna watu nimewaunga alafu wakaanza kupost vitu tofaut na maudhui ya group wakatolewa na ww kweli muhitaji
Niunge mkuu, 0653997090
 
Sasa mimi ushauri wangu kwako ni kwamba ufuge kuku kuanzia mia moja kwanza ili upate uzoefu. Kama unataka kufuga kuku 1000 kwa kuanzia inabidi upate afisa mifugo ili akupe ushauri wa kuaminika kuzuia hasara. contacts zake 0752576267
Kuku 1 anaweza kutaga mayai mangapi hadi kumtoa?
 
Back
Top Bottom