Kuna mtu kanunua silverlands na bdo analalamika hawakui na wanakula sana. Cha muhimu hata hizo za mtaani mi ninazo na sasahv ndo nafuga kibiashara maana mwanzo nilifuga kwa matumizi yangu tu.
Kuku we mpe chanjo zote na kuna ugonjwa mmoja mbaya sana unaitwa coccidiosis unakuwa unawapa dawa tu ukiona choo cha ugoro au dalili ya damu.
Vinginevyo hamna changamoto yoyote mwaka jana mwishoni niliuza kuku 160. Sahv nina kuku 270 tayari kwa pasaka...maisha ni kudhubutu maana mwanzoni niliona hawana faida ila nikitoa gharama ya ulishaji faida naiona.
Pumba tani 1 nanunua kwa laki 3. Then mahindi,mashudu,uduvi au dagaa,mifupa na chumvi. Chakula cha kununua cha ready made ni gharama sana maana kuroiler wanakula balaaa hadi usiku kama ukiwasha taa wao ni kula tu hawajui kingine.
Jaribu huwezi jua bahati yako iko wapi mana kila mtu na mkono wake. Kuna mwingine biashara ya kuku anaona hailipi, mwingine biashara ya gari hataki kusikia kabisa,mwingine kilimo anaona hakilipi ila kwa waliotoboa kupitia hivyo vitu ina mana walijaribu bila kuangalia hasara kwa awali.