GHARAMA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA.
Katika ufugaji inawezekana umekuwa ukiona miradi ya watu ukawa unaona miradi ya watu jinsi ilivyo mikubwa.unapenda Sana kutembelea katika miradi mbalimbali, pia na wewe unawazo la kufuga lakini unashindwa kujua ni mtaji shingapi utakaotosha kuanzishia ufugaji wa kuku.
Ndugu siyo lazima wewe kuanza na mradi mkubwa kama unanyoiona ya wengine. Hao mpaka kufika hapo wamechukua muda kidogo na wamekutana na changamoto nyingi.
Hivyo hata mtaji mdogo kabisa unaweza anzisha mradi wako wa ufugaji wa kuku baada ya muda na wewe utakuja kutembelea katika mradi wako.
Katika ufugaji wa kuku kuna aina nyingi za kuku leo tuangalie katika ufugaji wa kuku wa nyama broiler.
Kila aina ya kuku kuna vitu vya muhimu na haya ni mahitaji ya ufugaji wa kuku wa broiler.
Eneo
Mtaji
Banda
Vifaa
Chakula/maji
Madawa
Vifaranga
Hayo ndo mahitaji kwa kuku wa broiler leo hatuta ongelea hayo mahitaji, tutaanza kuongelea gharama za matunzo kuanzia kununua vifaranga hadi kuuza na faida yake ipoje! Kwa kawaida watu hujua kuku mpaka uwe na mtaji mkubwa hapana! Hata mtaji wa laki 550,000/= unaweza kufuga kuku broiler na ukapata faida jinsi unavyoendelea kufuga na mtaji wako utaendelea kukuwa.
Hapa tuananza na mtaji mdogo wa kuanzia vifaranga 100. Kuna makampuni mengi yanauza vifaranga. Kuna bei tofauti tofauti shng 1700,shng 1800 na 1900 kwa hapa tutatumia vifaranga wa 1800.
Utanunua vifaranga 100Γ1800=180,000/=
Siku umeenda kuchukua unatakiwa uku nyuma uwe umekamilisha yafutayo.
Banda umesafisha vizuri, unatenga Kona moja ambayo unatengeneza umbo la duara au box ndani ya duara kutakuwa na maranda na pia weka magazeti, magaziti usaidia maji yakimwagika utaweza kusafisha kirahisi.
Bila kusahau vyombo vya chakula na maji, chanzo cha joto unaweza tumia jiko la mkaa, balbu, chungu au taa ya chemli.
MATUMIZI KATIKA CHAKULA.
Vifaranga 100 kwa wiki 4 mpk 5 unaweza tumia mifuko 5 ya kg 50 mpaka kuuzwa.
Wiki mbili za mwanzo??
Starter pilet mfuko mmoja 60000 kwa mifuko 2.
60000Γ2= 120,000/=
Wiki tatu.
grower pilet mfuko mmoja 59,000/=
Wiki nne.
Finisher pilet 59,000/=Γ2. = 118,000/=
Chanzo cha joto. 15,000/=
Pesa ya akiba 30,000/=
Madawa na maranda unaweza gharimu 35,000/=
JUMLA?
180,000 + 120,000 + 59,000+ 118,000+ 15,000 + 30,000 + 35,000 = 547,000/=
Kwahiyo matunzo Hadi kuuza yata gharimu 550,000/=
Katika kuuza kuku mmoja shng 7000 Γ 100= 700,000/=
Faida itakuwa shng. 150,000/= kwa mwenzi mmoja?
Utakavyoendela kufuga mtaji wako utaongezeka. Na utazidi kuwa mzoefu katika ufugaji wa kuku wa broiler. Na pia bei ya chakula utofautiana na hii bei niliotumia hapo kutokana na chakula kupana lakin kuna she chakula kg 50 unaweza uziwa 55,000/=.