Wakuu neema iwe juu yenu.
Naomba nielezee changamoto na faida nilizokumbana nazo katika ufugaji wa kuku.
Nanze na broilers ambao watu wengi huwaona hawana faida.
kwakweli kama unafuga hawa kuku na ukawa na soko kwa wakati nikimaanisha kuwa kuku wamefika siku za kuuzwa na soko likawa linaeleweka basi ukiuza vizuri utaona faida nzuri sana kwa mana kuku hawa ukiwa mzoefu unajua ni idadi ngapi ya mifuko ya chakula kuwalisha mpaka wafike muda wa kuuzwa.
Changamoto inakuja pale wamefika kipindi wauzwe halafu unakuta soko halieleweki kwa mfano una kuku 500 bandani basi itakubidi kuwalisha mfuko mzima wa kilo 50 kwa kila siku na kwa kufanya hivyo kwa siku hata 5 soko likichelewa basi ujue kuku ndo wamekula faida na pindi uuzapo utarudisha pesa ya mtaji tu.
Ushauri wangu kwa kuku wa aina hii mfugaji unatakiwa uwe na soko tayari ili ifikapo muda wa kuuza basi wasiendelee kukaa bandani na kutafuna faida yenyewe.
Kwa sasa nafuga hawa kuku aina ya kutoiler japo wenyewe wanaita kienyeji chotara. Kuku hawa ni wazuri sana sababu ufugaji wake hautofatiani kama wale wa asili.
Kuku hawa ununuapo vifaranga huwezi tambua majike ni wangapi na madume mangapi ila tunakuwa na imani kuwa uwiano siku zote unalingana.
Faida ya kuku wa hii ya kuroiler ni mayai yao.
kwa mana mayai huuzwa mengi kwa ajili ya utotoreshaji pamoja ya kula.
Mayai haya hayana tofauti na yale ya kienyeji pure na soko lake lipo wazi wazi. Faida nyingine ni hawa kuku wanapokua unakuwa na idadi kamili ya majogoo na kwa usahuri tunashauriwa kuweka uwiano wa mitetea 7 kwa jogoo 1 kisha unauza majogoo waliobakia.
Majogoo wa kuroiler ufika mpaka kilo 5 ya uzito na kwa haraka haraka unaweza kupata 30,000/= kwa jogoo mmoja.
Ulishaji wake si changamoto sana kama wale wa broiler, sababu unaweza kupata mchanganyiko wa chakula (formula) nzuri ukachanganya mwenyewe na kuona matokeo mazuri.
Changamoto iliyopo ni kwamba uvumilivu wa kuwalea toka vifaranga mpaka wafike miezi 5 hapo ni pesa inatoka tu.
Ushauri wangu kuku hawa pindi ufugapo wahahitaji uangalizi wa hali ya juu sana ili uje upate pesa baada ya hiyo miezi 5.
Magonjwa yanayosumbua sana ni kinyesi cha ugoro (coccidiosis)na kupelekea kuku kupata chorela. Changamoto hiyo ni kwa sababu ya kutopatikana maji salama maeneo mengi.
Mimi nilikuwa nikichemsha maji usiku na kuyahifadhi vizuri ifikapo asubuhi nawapa kuku, ilinisaidia sana kuondokana na maradhi hayo wakati bado wako wadogo mpaka miezi 2.
Changamoto ni sasa hivi kwa mana wamekua wakubwa na wanakunywa maji mengi kulingana na awali.
Ahsanteni sana japo uandishi wangu si mzuri.
Bham cihi.