Kuku bwana
Ndugu wana JamiiForums,
Ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajiriwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.
Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi. Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk, Watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.
Karibuni kwa mjadala.
Upi muda sahihi wa ulishaji wa hawa ndege kwa wastani wa masaa 24 ya siku nzima?
Mathalani kuku 100 watahitaji kilo ngapi za chakula kwa siku? Na je mlo hutofautiana kati ya jinsia za hawa ndege?
Ni haya tu kwa kuanzia.
Muda sahihi wa kuwalisha kuku ni kuanzia saa mbili asubuhi mpaka watakapo maliza share yao kwa siku.Kiasi cha chakula(kgs) watakachokula mfano kuku 100,itategemea umri wao,hivyo ulitakiwa unipe umri wao katika wiki kwani kiwango cha chakula hubadirika kila wiki.
Nitahitaji kiasi gani cha fedha ili kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku?
Ndugu Lweganwa, kiasi cha fedha kitakachohitajika itategemea na ukubwa wa mradi wako,yaani idadi ya kuku na uwepo wa mabanda ya kufugia.Kama mradi wako utahusu mpaka ujenzi wa mabanda dhahiri kiwango cha pesa nacho kitakuwa kikubwa.Pia itategemea aina ya kuku utakao wafuga kama ni wa nyama au mayai.
Mie naomba uzoefu wako tu kwa ufupi..Hasa Changamoto na Masoko.
Na kwa beginner unanishauri nianze na kuku wangapi/au mtaji Tshs ngapi?
Na je, ninaweza kuwa na mifugo mingi katika eneo moja ee.g kuku,nguruwe,mbuzi (hasa kwa suala la maambukizo ya magonjwa) Mimi nahitaji kufuga kuku wa kinyeji nyumbani(sio shamba)kwa kuanzia vifaranga wasiozidi 50. Nina mabanda madogo tayari ila
1. Sijui wapi pa kupata vifaranga vizuri vuya kienyeji ambao wakitaga watakua na uwezo wa kuatamia mayai na kuangua wakaongezeka
2. Risks za kufuga hao kuku tukiacha wizi. Yaani magonjwa kama kuna yasiyotibika au vipi maana sina uzoefu na ufugaji
Pia naomba kama hutajali na upo kwa ajili ya kusaidia ukubali kukutana na wafugaji wanaoanza (mimi mmojawapo)ili tuelekezane na kuuliza maswali na hata kutembelea mabanda ya wafugaji walioendelea if possible.
Nianze nawe ndugu yangu Zion Daughter,kwanza umeuliza uzoefu wangu kwa ufupi hasa changamoto na masoko.Kwa upande wa changamoto ni kwamba wafugaji wengi wa kuku hushindwa kuyatambua magonjwa mbalimbali ya kuku pale yanapotokea hali inayopelekea kuku wengi kufa kwa magonjwa.Kujua ugonjwa inamsaidia mfugaji kuchagua dawa sahihi.Endapo kuku watapatiwa dawa sahihi hupona haraka kama walipata maambukizo ya ugonjwa.
Changamoto nyingine ni ughali wa chakula cha kuku hasa kutokana na kucompete na binaadamu.Na kuhusu masoko,kiukweli soko la kuku sio tatizo. Demand ya kuku pamoja na mayai ni kubwa sana kuliko uzalisha uliopo.Kuhusu kukushauri uanze na kuku wangapi au mtaji shilingi ngapi hapo itabidi kwanza uniambie unahitaji kufaga kuku wa aina gani,maana kuna kuku wa nyama wa kisasa (Broilers),kuna kuku wa mayai wa kisasa (Layers), pia kuna kuku machotara na kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama na mayai.
Na kwa wale wanaotaka kuanzishisha mradi wa utotoreshaji wa kuku watahitaji kuwa na kuku wazazi yaani Parent stock. Pia uniambie aina ya ufugaji mfano ufugaji huria,nusu kuria au wa ndani bila kuku kutoka.
Suala la ufagaji wa kuku kuchanganya na mifugo mingine kama ulivyo ainisha kwy swali lako inaruhusiwa ilaa ni kwa kuku wa kienyeji hasa wanaofugwa huria.Kinyesi cha mifugo mfano mbuzi,ng'ombe nk husaidia kutengeneza funza ambao ni chakula kizuri kwa kuku.
Nafikiria kufanya mradi mkubwa kiasi wa kuku wa mayai na/au wa nyama (layers na broilers) - nafikiria cycles za kuku
elfu 5 mpaka 10 hivi. Ninalo eneo (shamba) kubwa tayari kwa shughuli hiyo. Lakini kwanza natafuta mtu mwenye uzoefu (wa ufugaji wa kibiashara) na ambaye anaweza kunisaidia kufanya feasibility study ya mradi huo. Je, unaweza kunisaidia kazi hiyo? Unahitaji taarifa gani kutoka kwangu ili kufanya kazi hiyo kwa ufanisi?
Au kuna mtu/kampuni unafahamu wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi? Eneo la mradi lipo Dar, lakini nipo flexible kama mtaalamu atashauri nitafute eneo jingine - ili mradi prospects za kupata faida na sustainability ziwe za uahakika wa kuridhisha.
Ndugu yangu Da pretty,Sehemu ya kupata vifaranga wa kienyeji wenye uwezo wa kuatamia na kutotoa si shida hata ukitaka idadi zaidi ya hapo utapata.Kitu cha msingi unaweza ukatafuta namna ya kuwasiliana nami nitakuongoza.
Kuhusu risks ukiacha wizi kama ulivyosema ni kuwa,mara nyingi matatizo ya kuku ni magonjwa.Magonjwa ambayo ni common kwa kuku wa kienyeji ni pamoja na Kideri/mdondo hauna tiba ina chanjo,mafua yana tiba,Ndui(fowl pox) nayo haina tiba ila ina chanjo,Kipindupindu cha kuku(fowl cholera) ina tiba,Taifodi(fowl typoid) una tiba, Coccidiosis, una tiba pamoja ugonjwa wa homa ya matumbo kwa vifaranga(Pullorum), unatibika.
Kuhusu kutembelea wafugaji hiyo haina shida mara nyingi huwa nafanya hivyo kwa wafugaji wanaonza mradi na wale wenye matatizo, na pia wale wafugaji niliowaanzishia miradi ya ufugaji wa kuku huwa nafanya hivyo katka hali ya kuwasaidia.
NDUGU SMU, kazi yako iko ndani ya uwezo wetu.Tuna uzoefu na hiyo kazi.Kuna wapo ambao tayari tumekwisha waanzishia mradi kama wako na wamefanikiwa, kwa mfano kuna mteja ambaye tumemwanzishia mradi na kwa sasa,kila mwezi anatoa kuku 5000 na kuwapeleka sokoni.
Yeye anatotoresha na kufuga kuku wa kienyeji.Kila kuku anauzwa kwa shs.10,000 kwa bei ya jumla,ebu imagine kuku 5000 ni sh. ngapi anatengeza,ukipiga hesabu hapo utaona kila mwezi anatengeneza milioni 50.Akitoa gharama,let say milioni 20,je kuna kuna kazi gani ambayo unaweza ukaearn milioni 30 kwa mwezi!Kwa hiyo kama utahitaji ufafanuzi zaidi nitumie namba yako kwenye private message nitakutumia yangu.
Mimi nataka kufuga kuku,ila nahitaji kujua kati ya wale wa nyama,na mayai..wapi wanalipa zaidi?soko langu litakua Moshi na arusha zaidi. Halafu kama ni wa nyama au mayai, wazuri ni chotara,ama kienyeji ama kisasa? Ukishanijibu maswali mengine yataendelea hapo.
Kimsingi kuku wote wanalipa katika ufugaji,mfano kuku wa nyama broilers,kila wiki ukaingiza let say vifaranga 300 ,ukawafuga kwa kufuata kanuni,ukawafuga kwa wiki 8 ili uwauze kwa tshs. 6000/=.Kama kila wiki utaingiza vifaranga ina maana bechi ya kwanza watakapofikia wiki 8,tayari utakuwa na bechi nyingine 7 zinafuata.Chukulia vifo ni 50 katika kuku 300 ingawa inaweza ikawa chini ya hapo.Kwa hiyo katika kila bechi kila wiki utakuwa na kuku 250.
Kimahesab, kuku 250 ukizidisha mara tshs.6000/=,utapata tshs. 1500,000/= kwa wiki na kwa mwezi utapata tshs 6000,000/=.Mapato ya broilers yanaanza baada ya miezi 2 yaani wk 8 ingawa unaweza ukawauza chini ya hapo lkn kwa uzito wa chini kidogo ndio maana inashauriwa wauzwe wk ya nane.
Kuku wa mayai pia nao wanalipa sana tatizo inatakiwa uwe na mtaji mkubwa kwa ajili ya gharama ya kuwanunua na chakula ,mathalani kwa sasa baadhi ya makampuni ya kutotoresha vifaranga wanauza kila kifaranga tshs.2500.Kila kifaranga mpaka atakapoanza kutaga atahitaji kilo 8 za chakula,ukiongeza na madawa, mfanyakazi nk utajikuta unatakiwa uwe na mtaji mkubwa kweli.Mapato ya kuku wa mayai utaanza kupata kwa wastani kuanzia mwezi wa 5 katikati .Baada ya hapo utakuwa na kazi kuuza mayai tu mpaka watakapo choka wiki ya 80 kama umewatunza kwa kufuata misingi na kanuni boro za ufugaji.
Kama ni kuku wa mayai,wakisasa ni wazuri zaidi kwa kuwa wanataga kwa wingi.Kama ni wa nyama ukiweza kufaga machotara ni wazuri zaidi kutokana na kuwa na soko la uhakika.Watu wengi sasa hivi wanapenda kuku wa kienyeji hivyo machota, nyama yake haina tofauti na kuku wa kienyeji,pia ukiweza kuwafuga kwa miezi 6 utaweza kuwauza kila kuku kwa tsh.10000/= bila mteja anayenunua kulalamika.Kuku pure wa kienyeji wana ukuaji hafifu.
Leo niuzungumzie ugonjwa wa mafua(
Infectious coryza)
Mafua ni ugonjwa mojawapo unaoshambulia mfumo wa upumuaji wenye tabia ya kumfanya kuku kutoa kamasi puani,kupiga chafya,kichwa kujaa maji na kuvimba.Ugonjwa huu huwaathiri kuku,bata mzinga na kanga.
Mafua ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege wa umri wote lakini zaidi ni kwa wakubwa.Ueneaji wake ni kwa njia ya hewa na chanzo chake ni ndege wanaougua au waliougua.
KISABABISHI
Mafua ya kuku husabibwa na Kimelea(Bacteria) kiitwacho
Haemophilus paragallinum
DALILI ZA MAFUA
Dalili za mafua huanza kuonekana kuanzia siku ya 3-10 toka kuambukizwa.Sehemu zinazodhihirika zaidi ni pua, macho, mapafu, koo na koromeo.
1. Kuku kuzubaa na kuto makamasi wakati mwingine yenye damu.
2. Kubadilika rangi ya mapanga(Comb and wattle) na kuwa ya rangi ya bluu
3. Huvimba macho,hali inayosabababisha kuku kuziba jicho moja na wakati mwingine yote mawili
4. Kuvimba mapanga na uso
5. Kukosa hamu ya kula na kupunguza utagaji
6. Kuku kukoroma wakati wa kupumua
7. Kuhara uharo wenye harufu mbaya hasa kama kuna maambukizi mengine ya vimelea
8. Vifo ni vichache na kuku hupona baada ya wiki
NAMNA YA KUZUIA
Usafi wa mazingira na kuhakikisha hakuna vimelea wanaosababisha ugonjwa huu
Kuku wagonjwa watengwe mbali na kuku wazima
Hakikisha vifaranga wanaagizwa kutoka kwenye makampuni yanayofuata kanuni bora za ufugaji
TIBA
Mafua ni ugonjwa unaotibika,mfugaji unaweza kumwona afisa mifugo aliye karibu nawe ili akuandikie dawa sahihi ya kutumia.
Ningependa unifahamishe kwa kuku hao wa kienyeji au mchanganyiko/machotara unahitaji eneo lakiasi gani kwa kuku 1000? Ukubwa wa mabanda? Na ukubwa wa eneo watakao shinga kwa mchana/nje?
Na utagaji wao unakuaje, ni kila siku au? Nia yangu ni kuwauza kwanza majogoo kwa ajili ya nyama pale watakapofikia umri na uzito wa kutosha, na hao majike watage msimu mmoja au miwili ndio niwauze. Na je ninaweza kuwasialana na wewe kwa njia gani zaidi ya hapa JF?
Ahsante
NAFASI INAYOHITAJIKA KWA KUKU 1000 WENYE RIKA TOFAUTI (MABANDA YA KUKU)
| RIKA | CHICKS
VIFARANGA | GROWERS
KUKU
WANAOKUWA | LAYERS
KUKU
WANAOTAGA |
UMRI
KTK
WIKI | 0-6 | 7-20 | 20-80 |
KUKU/ENEO LA
M[SUP]2 [/SUP]MOJA ZA MRABA | 12 | 9 | 6 |
M[SUP]2 [/SUP]ZINAZOHITAJIKA
/KUKU 1000 | 83.7M[SUP]2[/SUP] | 111.2M[SUP]2[/SUP] | 166.6M[SUP]2[/SUP] |
| | | |
Eneo watakaloshinda kuku 1000 wakati wa mchana, ambao hufugwa ktk mfumo wa nusu huria ni mita za mraba 10,000 .Hii inamaana kwamba ,kuku mmoja anahitaji eneo lenye mita za mraba 10.Kuhusu utagaji kuku wa kienji hana sifa ya utagaji wa mayai mengi.Kuku wa kienyeji hutaga kwa mzunguko.Kila mzunguko mmoja hutaga hutaga wastani wa mayai 15 na kuanza kuatamia,kutotoa na kulea vifaranga.Mzunguko huo huchukua wastani wa kipindi cha miezi 4 hadi 6 .Hali hiyo hiyo humfanya atage mayai machache kati ya mayai 30 hadi 60 kwa mwaka ukilinganisha na kuku wa kisasa ambao hutaga mayai 270 hadi 300.
Kuku wa kienyeji ukitaka watage mayai mengi wasiruhusiwa kuatamia,kila mayai yanayotagwa yaokotwe na kuhifadhiwa na kama mfugaji atahitaji kutotoresha, kama kuna kuku wengi ,ni vyema ikatumika machine ili kuzalisha vifaranga wengi zaidi.Kuku wa kienyeji anapokuwa kwenye mzunguko wa utagaji,kila siku hutaga yai moja.
Mawasiliano yangu nimekutumia kwenye private message yako ya jf,nenda kwenye notification yako fungua utaona.
Last edited by kic