kuna rafiki yangu anahitaji kufuga kuku wa Kienyeji elfu moja(yaani aanze na vifaranga mpaka hatua watakayoanza kutaga mayai ili atotoreshe kwa mara kadhaa kisha awauze kuku wakubwa),napenda kufahamu gharama za kuwakuza hawa kuku,banda tayari lipo,na gharama ya kuwahudumia kwa hiyo miezi sita itaweza kulipa.nitahitaji kufahamu gharama za kunifanyia mchanganuo huu.
Singo,
Ufugaji wa kuku wa kienyeji unalipa sana isipokuwa usiwe ule wa pure kuku wa kienyeji bali uwe ule wa kuku chotara kwasababu, kimsingi kuku chotara hana tofauti kubwa sana na kuku wa kienyeji kwenye ladha ya mayai na hata kile kiini chake nacho huwa kama cha kuku wa kienyeji, lakini pia hata ladha ya nyama yake huwa kama kuku wa kienyeji, hakuna tofauti hata kidogo.
Faida ya kufuga kuku chotara ni kuwa wanakuwa na ufanisi mkubwa kwenye utagaji na hata ukuaji wake tofauti na kuku wa kienyeji pure. Lakini pia kuku chotora wanachukua tabia ya kuku wa kienyeji kwenye suala la ustahimilivu dhidi ya magonjwa. Kwa mantiki hiyo nashauri huyo rafiki yako afuge kuku chotara badala ya kuku wa kienyeji. Hata hivyo,upatikanaji wa Kuku hawa chotara ni mkubwa na unaweza kupata kwa Idadi yoyote ile unayotaka.
Kuhusu gharama ya mradi wa ufugaji wa kuku chotara 1000 basipo banda ni tsh 20m. Gharama hizo zitahusisha mishahara ya wafanyakazi, gharama za chakula , gharama za kuwanunua wakiwa na umri wa siku moja(DOC), gharama za matangazo, tshirt,gharama za madawa pamoja na vitu vyote muhimu vinavyohitajika katika ufugaji wa kuku hao mfano vinyweo (drinkers),vilishio(feeders), mabox ya kutagia (nest box),bembea (peaches ),maranda nk.
Mradi wa ufugaji wa kuku aina ya chotara unalipa sana hasa kutokana na soko la aina hii ya kuku kuwa kubwa. Watu wengi wanahitaji kuku wa kienyeji na hawa chotara huwa wanauzwa kama kuku wa kienyeji. Kitu muhimu na cha msingi ni kuthibiti vifo.
Gharama ya kukutengenezea business plan ya kuku hawa elfu moja ni tsh.2m, lakini maelewano yapo. Kumbuka business plan tunazotengeneza ni business plan zinazokubalika bank, hivyo mtu anaweza kuzitumia kwa ajili ya kuombea mkopo bank kama atakuwa na dhamana, maana bank pamoja na kuwa na business plan nzuri huwezi pata mkopo mpaka uwe na dhamana (collateral).