Agrey998
JF-Expert Member
- Jul 8, 2019
- 417
- 550
Miaka ya karibuni vijana wengi wamejiingiza katika biashara ya ufugaji wa Mbwa wa kisasa kwa kuimport mbwa nje kama Germany shepherds long coat, Boerbull, Caucasian shepherd, Rottweiler's na wengine na wakifika hapa huwazalisha na kuuza watoto (puppies) huku wateja wao wakubwa wakiwa ni matajiri au Watu ambao nao wanaingia kwenye biashara hiyo.
Puppy mmoja wa miezi miwili ukikuta ni hizi local breed za shepherd anapatikana kwa laki tano au lak nne
. Lakini ukikuta ni Germany shepherds original basi ni laki tisa hadi milioni na mbwa mwenye uzao mzuri anaweza kuzaa hata watoto kumi.
Ukiuza ni milioni 10 japo utaingia gharama za chanjo kama Dhlp na pavo virus ambazo ndio za muhimu ili mbwa wasikufie na pia usafi ni muhimu sana na ufanywe kila siku na pia kuwalisha lazima uwalishe kisasa tena wale hata mara mbili kwa siku na uwape protien suppliments ili kuwaboost . Hapo ndio utaona pesa.
N.B. Hii kazi kama ni mtu mwenye kinyaa Bora uache maana itakutesa .
Hii kazi ukitaka ikulipe lazima uipende sana.
Hii kazi inahitaji uvumilivu wa hali ya juu
Ukifanya hii kazi basi lazima uwe na mishe nyingine pembeni ya kukuingizia hela .
Mwisho ni kwamba pesa sio rahisi pia kwenye ufugaji huu lazima upambane.
Nawasilisha