Ufugaji wa Mbwa!

Ufugaji wa Mbwa!

john hotsam da1

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2012
Posts
396
Reaction score
79
Habari za muda huu wakuu,

Nimepitia nyuzi nyingi jukwaa hili kwenye upande wa ufugaji nimeona asilimia kubwa wamejikita kwenye ufugaji wa kuku,inaelekea inalipa hii! Anyway me nmekuja kivingine,hili ni wazo tu na kama nikiridhika nalo sana naweza fanya kweli (make it reality),nakukaribisha

Suala zima liko hivi;

Nanunua mbwa wadogo (puppies) wa aina(breeds) zinazopendwa mf german/australian shepherd, Rottweiler or poodle say few females n a single male roughly each costs 300k tzs.

Banda ninalo (nafugia local breeds currently) so ni kubadilisha matumizi tu hapo Mbwa mmoja anakuwa tayari kushika mimba kwenye umri wa mwaka 1-2 (recommended) na baada ya miezi miwili atazaa.Tuseme bei ya mbwa mdogo kipindi hicho itakuwa 350k na nna average ya vitoto vitano..do the arithmetics!!

Nimeelezea wazo langu kwa ufupi na bado sina ujuzi mkubwa kuhusiana na mfugo huu.naelewa chakula ni gharama bila kusahau chanjo kila mwezi ila nna imani baada ya miaka miwili itakuwa ni mradi wenye tija

Nishauri tafadhali!
 
Wazo zuri mkuu, if you do the math hapo kuna faida kubwa tuuh cha muhimu ni mbwa wale vizuri na wawe na usimamizi mzuri.
 
Kwa ushauri tuu maana hii kitu tayari ni ajira hakikisha mbwa wako ni pure breed na wawe register kwa association ya hyo breed, hapo utapata wateja kutokea hadi ukraine mtu ana book kwa hyo site anakutumia hela wewe unasafirisha puppy
 
Hivi pure breed kama ya Germany Shepherd, Rottweiler n etc kinyumbani hapa TZ wanaweza patikana wapi?
Baadhi ya maduka ya dawa za mifugo huuza puppies au huwa na connections za wafugaji
Mf ni pale Moroko right after yard ya magari

Ila ukipata connection ya direct na mwenye puppies bila middle man huwa ni bei poa zaidi
 
Nitacheki nao, si pale kwa Dr Sinare (am not sure with the name kama lipo sahihi) ila am sure ndio hapo unapo pazungumzia.
 
Kama unamaanisha pure as pure, utadanganywa...ni raia wachache sana wana hiyo breed, na hata wakiwa nayo inakuwa crossed sana. Labda ujaribu taasisi Kama polisi etc.
Kuna breeder wana pure breed na wengi wanawanunua kwenye breed association kama umefuatilia hizi thread nilisema ukiwa na pure breed una mreguster kwenye association ya breeder wa hyo breed hvyo basi soko hutegemei tanzania na mfano mtoto w rotwailer wa miezi miwili ni usd 800..
 
Jinsi ya kupata hizo association kibongo bongo siochangamoto kweli, maana la sivyo ukinunua nje ya TZ gharama itaongezeka.
 
ukifuga wale wenye mafuta utapata soko zuri sana IRINGA na NJOMBE
Sidhani kama hili ni jukwaa la utani mkuu!!

Nilinunua rottweiler 2 dume na jike mwaka 2014 kwa 3.6m(1.8 @) jike amezaa mara ya kwanza watoto saba nikauza kila mmoja laki saba,mara ya pili amezaa watoto sita na nimeuza kwa million @,sasa hivi Nakula faida tuu
 
Kweli unakula faida tuuh,
Kwenye uzao wa kwanza ukutaka kubaki na kajike mkuu ili uongezee yawe majike mawili na dume moja au you are not doing it for commercial ingawa unakula faida kidogo kidogo humo humo?, by the way hivi mbwa jike anapata joto kwa mwaka mara ngapi? Me maisha yangu yote nimebahatika kufuga madume tuuh, Mkuu kama itawezeka tupiamo na kapicha ka Rottweiler wako
 
1470225147763.jpg
kwa ambao hamfahamu huyo ndio rottweiler
 
Mimi nimtaalam wa mbwa nimepata na mafunzo msalum miez 6 na hapa nipo nao hata sahv hyo bznezz ni more profitable hata mfugaji wa ngombe awez kukugusa,for more info,,,tuwacliane.
mkuu unapatikana wapi na mimi nije nichukue maujuzi.
 
Habari za muda huu wakuu,

Nimepitia nyuzi nyingi jukwaa hili kwenye upande wa ufugaji nimeona asilimia kubwa wamejikita kwenye ufugaji wa kuku,inaelekea inalipa hii! Anyway me nmekuja kivingine,hili ni wazo tu na kama nikiridhika nalo sana naweza fanya kweli (make it reality),nakukaribisha

Suala zima liko hivi;

Nanunua mbwa wadogo (puppies) wa aina(breeds) zinazopendwa mf german/australian shepherd, Rottweiler or poodle say few females n a single male roughly each costs 300k tzs.

Banda ninalo(nafugia local breeds currently) so ni kubadilisha matumizi tu hapo Mbwa mmoja anakuwa tayari kushika mimba kwenye umri wa mwaka 1-2 (recommended) na baada ya miezi miwili atazaa.Tuseme bei ya mbwa mdogo kipindi hicho itakuwa 350k na nna average ya vitoto vitano..do the arithmetics!!

Nimeelezea wazo langu kwa ufupi na bado sina ujuzi mkubwa kuhusiana na mfugo huu.naelewa chakula ni gharama bila kusahau chanjo kila mwezi ila nna imani baada ya miaka miwili itakuwa ni mradi wenye tija

Nishauri tafadhali!!
Hiyo k kwenye 300 ina maana gani?halafu mimi kila mbwa ninayemfuga kwa ajili ya ulinzi ikifika usiku akimuona mtu anakimbia kujificha!tatizo ni nini?
 
Hiyo k kwenye 300 ina maana gani?halafu mimi kila mbwa ninayemfuga kwa ajili ya ulinzi ikifika usiku akimuona mtu anakimbia kujificha!tatizo ni nini?
K inamaanisha elfu hivyo 300k tzs ni 300,000 tzs
Kuhusu tatizo la mbwa wako tusubiri wataalamu tu
Wa kwangu nilio nao sasa ni wa kubweka tu ila ukimtisha na jiwe na yeye mbio kutafuta penye usalama
 
Back
Top Bottom