Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa; ushauri wa kitalaam, changamoto, mawazo na masoko

Ufugaji wa ng'ombe wa maziwa; ushauri wa kitalaam, changamoto, mawazo na masoko

Salaam wakuu✋🏽

Naomba ushauri juu ya ufugaji wa Ng'ombe wa maziwa kwa muongozo ufuatao; (though not limited to that)
1. Aina gani ya Ng'ombe wa maziwa inatoa maziwa mengi? Kwa maeneo ya joto joto kama pwani na Morogoro.

2. Naweza kuotesha nyasi aina gani kwa ajili ya malisho? Aina zipi zinaongeza sana maziwa. Mbinu za uoteshaji wa malisho zikoje?

3. Naomba mbinu za mpangilio mzima wa utunzaji wa malisho ghalani ili kujihakikishia malisho mwaka mzima.

4. Nipe mbinu za soko la maziwa na pia changamoto za soko.

5. Namna bora ya kuongeza tija katika management ya hawa ng'ombe (mbinu za kivita).

6. Zipi ni changamoto katika ufugaji wa ng'ombe wa maziwa?

7. Mambo gani niyazingatie kabla sijaleta ng'ombe bandani?
 
Salaam wakuu[emoji1424]

Naomba ushauri juu ya ufugaji wa Ng'ombe wa maziwa kwa muongozo ufuatao; (though not limited to that)
1. Aina gani ya Ng'ombe wa maziwa inatoa maziwa mengi? Kwa maeneo ya joto joto kama pwani na Morogoro.

2. Naweza kuotesha nyasi aina gani kwa ajili ya malisho? Aina zipi zinaongeza sana maziwa. Mbinu za uoteshaji wa malisho zikoje?

3. Naomba mbinu za mpangilio mzima wa utunzaji wa malisho ghalani ili kujihakikishia malisho mwaka mzima.

4. Nipe mbinu za soko la maziwa na pia changamoto za soko.

5. Namna bora ya kuongeza tija katika management ya hawa ng'ombe (mbinu za kivita).

6. Zipi ni changamoto katika ufugaji wa ng'ombe wa maziwa?

7. Mambo gani niyazingatie kabla sijaleta ng'ombe bandani?
Siti ya mbele
 
Kwa anayehitaji kujifunza kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na Malisho.

Kuna vitabu(softcopy) bei sh
5000.
Mbegu za Super napier kilo moja sh
5000.

Super napier ni nyasi zenye kiwango kikubwa cha protini, zinakua haraka, zinatoa machipukizi mengi.
Zikitunzwa vizuri zinaweza kutoa tani 180 za nyasi kwenye eneo la eka moja(kwa mwaka)ambazo zinatosha kulisha ng'ombe 15 kwa mwaka mmoja.

Mawasiliano 0756 625 286.
Screenshot_20220926-143246_1.jpg
Screenshot_20220926-143148_1.jpg
IMG_20230220_175336_024.jpg
IMG_20221228_172426_071.jpg
IMG_20230208_090731_854.jpg
IMG_20230325_105351_5.jpg
IMG_20230222_065551_367.jpg
 
Kwa anayehitaji kujifunza kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na Malisho.

Kuna vitabu(softcopy) bei sh
5000.
Mbegu za Super napier kilo moja sh
5000.

Super napier ni nyasi zenye kiwango kikubwa cha protini, zinakua haraka, zinatoa machipukizi mengi.
Zikitunzwa vizuri zinaweza kutoa tani 180 za nyasi kwenye eneo la eka moja(kwa mwaka)ambazo zinatosha kulisha ng'ombe 15 kwa mwaka mmoja.

Mawasiliano 0756 625 286.View attachment 2586643View attachment 2586645View attachment 2586646View attachment 2586647View attachment 2586651View attachment 2586652View attachment 2586654
Mkuu nahitaj nyasi nipande...unapatikana wap
 
Habari ya leo wafugaji nlipotea leo ngoja niwape somo la utunzaji wa ndama nimewamiss mno[emoji16]

Utunzaji bora wa ndama toka kuzaliwa mpaka kufikia miezi mitatu

Baada ya kuzaliwa ndama anatakiwa kuwekwa sehemu kavu yenye kivuli na sehemu isiyofikiwa na mvua kwa urahisi ili kuepuka hatari ya ndama kupata maambukizi wa mfumo wa hewa(pneumonia)

Siku nne za mwanzo

Mara tu baada ya kuzaliwa ndama huhitaji maziwa ya mwanzo ya mama yake yanaitwayo colostrum.Ni muhimu kuhakikisha ndani ya kabla saa sita toka ndani kazaliwa awe ashatumia maziwa haya hivo ni vema nusu saa baada ya kuzaliwa ndama aelekezwe kwa mama aweze kunyonya

Maziwa ya mwanzo yana kiwango kikubwa cha cha viinilishe ukilinganisha na maziwa ya kawaida .Viin lishe ambavyo huwemo ndani ya maziwa mwanzo zaidi ni aina mbali mbali za vitamini madini pamoja na viini kinga dhidi ya maradhi
Viini kinga vya asili dhidi ya maradhi hufyonza kutoka kwenye maziwa ya mwanzo katika kipindi kifupi na kumpa ndama uwezo wa kupambana na magonjwa yanaweza kumuathiri wakati wa utoto na ndo maana ni vizuri zaidi kuhakikisha ndani ya saa sita baada ya kuzaliwa awe ameshapata hayo maziwa hasa nusu saa maana ndipi utumbo wa ndama unakua na uwezo mkubwa wa kufyonza viine kinga hivo.

Kawaida baada ya kuzaliwa ndama huanza kusimimama na kujisogeza taratibu kwenye kiwele cha mama na kuanza kunyonya .

Inapotokea mama anarusha mateke unaweza kumfunga miguu ili na kumuweka ndama akaanza kunyonya

Pia iwapo ataonekana ni mdhaifu kuweza kunyonya unaweza kumkamulia maziwa kutoka kwa mama yake na kumnyesha kwa kutumia artificial teat (chuchu za ndama) au chupa na hakikisha umesadifisha vifaa vya kunyweshea kwa maji ya moto pamoja na disinfectants (mfano V-Rid)
Kiasi cha kunyweshea ni lita 1.5 mpaka 2 kunywesha pia kuna hitaji umakini au mtu mzoefu ili ndama asijepaliwa maziwa yakaingia njia ya hewa na kuleta hatari ya kumpoteza hivo hakikisha chuchu au chupa inakua juu ya ulimi unapokua wakati ndama anapatiwa maziwa


IKITOKEA NDAMA KAMPOTEZA MAMA
Namna ya kumsaidia ndama ikitokea mama yake amekufa ni mkupatia maziwa ya ng'ombe mwingine ambae pia amezaa siku hio hio na huyo au kumtengenezea artificial colostrum

Artificial colostrum (maziwa mbadala ya mwanzo ) changanya
Yai moja
300mls za maji
600mls za maziwa ya kawaida
Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya mnyonyo
Kijiko kimoja cha chai cha mafuta ya samaki

Mchanganyiko unatakiwa kua sawa joto la mwili la 39 centrigrade sawa na joto la mwili wake
Na atatakiwa kupatiwa mara tatu kwa siku asubuhi mchana na jioni ndani ya siku 3-4

aina za unyweshaji wa maziwa kwa ndama
1.kumruhusu ndama kunyonya kwa mama yake
2.kumpatia maziwa ndama baada ya kukamua

1.kumruhusu ndama kunyonya kwa mama yake

Utaratibu ufanyika kwa kumruhusu ndama kunyonya kabla ya kukamua au baada ya kukamua kwa kumuachia ndama maziwa kwenye kiwele .Kutumia utaratibu inashauriwa ni vema kupima kiasi cha maziwa yanayotolewa na ndama ili kuhakikisha ndama anapata maziwa ya kutosha na na upimwaji unafanywa kwa kukamua maziwa yote na kujua kiasi cha maziwa ng'ombe anachotoa kwa wakati huo

-Faida ya kutumia njia hii ni kua maziwa atakayonya ndama kunauhakika wa kua safi na salama kwa ndama kua na joto linalotakiwa.
-Kupunguza uwezekano wa ng'ombe kuugua magonjwa ya kiwele (mastitis)

-Changamoto za njia hii ni kua ndama anaweza kutumia maziwa kiasi kikubwa ukiringanisha na mahitaji na kusababisha hasara kwa muuzaji wa maziwa au ndama kuachiwa kiwango kidogo zaidi na kuperekea udumavu na afya duni kwa ujumla


2.Kumpa baada ya kukamua

Njia hii inashauriwa kumnywesha ndama mara tu baada ya maziwa kukamuliwa ili yawe katika joto linalotakiwa na kuzingatia usafi wa vyombo vya kunyweshea
Ikiwa maziwa yamepoa yatatakiwa kupashwa joto na kufikia joto la mwili wa ng'ombe 30 centrigrade kabla ya kumnywesha ndama

-Faida ya njia ndama atapatiwa maziwa kutokana na mahitaji yake hivo hatutegemei kupata hasara au ndama kudumaa.

-Changamoto ya njia hii ni kua hatari ya ndama kupata magonjwa ya kuharisha(calf scours) iwapo usafi wa vyombo ama joto la maziwa havitazingatiwa

Matunzo ya ndama siku nne na kuendelea
Ndani ya mwezi wa kwanza wa kuzaliwa mfumo wa umeng'enyaji wa chakula kwa ndaman hua sawa na wanyama wenye tumbo moja (monogastic) kwani ndani anategemea maziwa kupata virutubisho kama ilivo kwa wanyama wengine na kwa stage hii ndama anakua hana uwezo wa kuchakata vyakula vyenye asili ya majani au nyasi

Kupitia hivo kuna matunzo ambayo ndama atakiwa kupatiwa yatayoweza kumfanya apate uwezo haraka wa kuanza kufanya umeng'enyaji wa vyakula vya aina hio kama ng'ombe wakubwa

Namna ya kufanya ndama ni anapofikisha siku wiki moja tu atakakiwa kuanza kufundishwa kula vyakula vikavu mfano calf stater au concetrates ambapo utaanza kumfundisha kwa kuchukua chakula na kumpaka mdomoni kwa juu aanze kusikia harufu na baada ya hapo ataanza kula kidogo kidogo mpaka anamaliza mwezi anakua ameshaanza kula vizuri baada ya hapo utaanza kumpatia majani malaini

-Kila siku ndama atatakiwa kupatiwa maji ya kutosha ila kuzingatia ni kuweka maji mbali lisaa limoja kabla na baada ya kunyonyweshwa

-Unapozidi kumpatia ndama virutubisho vya kutosha na ukuaji wa wake unapoenda vizuri unazidi kuongeza uwezekano wa kumuachisha mapema kuendelea kuuza maziwa

-kuanza kutumia chakula mapema kunamfanya mfumo wa chakula kukomaa upesi na kumpunguzia ndama uwezekano wa kupata magonjwa ya kuharisha
Tatifi zinaonesha ndama wengi waliokunywa maziwa mengi hupata magonjwa ya kuharisha kwa urahisi.
 
mkuu wapi pure breed ya fresian inapatikana kwa hapa tanzania.
 
Back
Top Bottom