Ufugaji wa Nguruwe

Ufugaji wa Nguruwe

Degelingi_One

Member
Joined
Nov 17, 2018
Posts
72
Reaction score
121
Wakuu salaam.

Kutokana na hali ilivyo ngumu huku mtaani, kijana nimejipiga na kupambana nikakusanya kiasi cha 300k. Nataka nijitupe kwenye ujasiliamali wa ufugaji wa nguruwe. Wataalamu wa haya mambo nipeni uzoefu hasa:

1. Mabanda ya kufugia
2. Muda sahihi wa kuuza
3. Ulishaji, Mara moja au Mbili kwa siku
4. Changamoto za magonjwa
5. Soko la Nguruwe hasa mkoani Iringa

Shukrani

1624960805497.png

Siijui hiyo biashara wala huo ufugaji kiundani, lakini kwa huo mtaji wa laki tatu huenda ni mdogo sana, hutoboi. Hiyo laki tatu inaweza kutosha kununua watoto kadhaa wa nguruwe au kujengea banda tu.

Nawaza tu kuhusu Banda la kufugia, Watoto wa nguruwe, Chakula la kuwalisha, madawa nk.

Kwenye biashara ya ufugaji, faida kubwa iko ikiwa itafuga kwa wingi. Kwa mfano kwa nguruwe, kama utaanza kwa kununua watoto basi labda wasipungue 10, ama kama ni majike basi yawe yana mimba kama mawili hivi.

Mziki upo kwenye kuwalisha, hao viumbe naambiwa huwa wanakula vilivyo (uzuri wana kula vitu vyovyote tu, japokuwa ikitaka wakue chap chap na kunenepa kwa haraka kuna chakula wanashauri wapewe).

Pia nasikia nguruwe mchanga mpaka akue uweze kumuuza kwa faida nzuri itakuhitaji mtunze kama miezi nane hivi.

Yote kwa yote huyo kiumbe ni mtamu, hata sisi waislamu huwa tunamtafuna kimya kimya kwa siri siri.
 
Kwa mazingira niliyopo miundo mbinu kama mabanzi na nguzo gharama zake ni ndogo sana mkuu
Gharama ya kununua nguruwe, madawa na chanjo, vyakula na hayo mabanzi ya bei rahisi unayosema.

Kumbuka biashara yoyote inapoanza, hela huwa inatoka tu na sio kuingia. Unadhan gharama za kuendesha huo ufugaji mpaka uanze kuuza ni kiasi gani?

Kuna sheria moja nilijiwekea, kama nataka kufanya biashara ambayo inahitaji Tsh 1000, na mimi nina hiyo hiyo, basi huwa sifanyi. Maana utaishia kupoteza hela tu.

Kuanzisha biashara, walau uwe na mtaji kiasi mara mbili ya kinachohitajika, au basi kizidi kile kinachohitajika.

Kumbuka biashara haina kanuni rasmi kwamba ukiapply lazima ifanikiwe, kuna mambo kwenda mrama. Kama itakuwa hujajipapanga vzr, basi itafia njiani.

Kwahiyo mkuu hata kwenu mngekuwa na mashamba ya miti, ili upate mbao na mabanzi bure, bado hiyo 300k haitoshi.
 
kwa Zanzibar soko lake lipoje
Kama ilivyo pombe ambapo kwa Zanzibar haizalishwi lakini inaletwa kutoka bara na kuuzwa maeneo maalum.

Nguruwe nayo ni hivyo hivyo, hawafugwi (japokuwa kisiri nasikia kuna mchaga mmoja mbabe anafuga Unguja), Kitimoto inaletwa Zanzibar na inauzwa kwenye maeneo mahususi tu, hususani kwenye hoteli za kitalii tu.

Hivyo kufanya hiyo biashara inabidi uwe na connection na hizo hoteli halafu uwe unaleta Cargo yako kila baada ya muda fulani. Kwa sasa biashara ya utalii imedorora sana, hakuna watalii hivyo soko la hizo mambo liko down.

Tamaduni za watu wa Zanzibar ziko tofauti sana na bara.
 
Je ni kweli nguruwe anafugwa ktk makambi ya jeshi na polisi? Pia mtu wa bara anaruhusiwa kumiliki Ardhi Zanzibar?
 
mkuuu nauliza nifahamu namna ya kuoperate kitimoto Zanzibar, ni biashara inalipa vizuri.
Sawa mkuu, huwenda inalipa kwa sababu sijawahi kufika huko ila nakushauri kuwa makini sana.
 
Kama ilivyo pombe ambapo kwa Zanzibar haizalishwi lakini inaletwa kutoka bara na kuuzwa maeneo maalum.

Nguruwe nayo ni hivyo hivyo, hawafugwi (japokuwa kisiri nasikia kuna mchaga mmoja mbabe anafuga Unguja), Kitimoto inaletwa Zanzibar na inauzwa kwenye maeneo mahususi tu, hususani kwenye hoteli za kitalii tu.

Hivyo kufanya hiyo biashara inabidi uwe na connection na hizo hoteli halafu uwe unaleta Cargo yako kila baada ya muda fulani. Kwa sasa biashara ya utalii imedorora sana, hakuna watalii hivyo soko la hizo mambo liko down.

Tamaduni za watu wa Zanzibar ziko tofauti sana na bara.
Kwanini afuge kwa siri, kwani kuna shida gani?
 
Hoteli gani wanatengeneza kitimoto kizuri hapa Zanzibar mkuu?
Kama ilivyo pombe ambapo kwa Zanzibar haizalishwi lakini inaletwa kutoka bara na kuuzwa maeneo maalum.

Nguruwe nayo ni hivyo hivyo, hawafugwi (japokuwa kisiri nasikia kuna mchaga mmoja mbabe anafuga Unguja), Kitimoto inaletwa Zanzibar na inauzwa kwenye maeneo mahususi tu, hususani kwenye hoteli za kitalii tu.

Hivyo kufanya hiyo biashara inabidi uwe na connection na hizo hoteli halafu uwe unaleta Cargo yako kila baada ya muda fulani. Kwa sasa biashara ya utalii imedorora sana, hakuna watalii hivyo soko la hizo mambo liko down.

Tamaduni za watu wa Zanzibar ziko tofauti sana na bara.
 
Kwa kuanzia 300k inatosha. Huku Iringa kwa mfano bei ya nguruwe wadogo miezi 2 "weaned piglet"Ni elfu 50. Hivyo unaweza kuanza na vitoto 3,dume 1 na vijike2. Ni vema kutengeneza banda lenye Concrete kuliko la kichanja cha mabanzi ili nguruwe wasijeruhiwe kwa kujibana miguu.

Gharama ya banda haizidi elfu 60. Pia gharama ya chakula kwa hao nguruwe 3 si kubwa kwani debe la pumba ni elfu 3.Wakiwa wadogo debe la pumba wanaweza kula kwa siku 3 hadi 4 kama utawapa na makombo ya vyakula.

Nguruwe huwa tayari kuzaa akiwa na miezi 6 hadi 7 km wata kua vizuri km ukizingatia vzr kinga ya minyoo hasa ukurutu.Nguruwe akizaa unaingiza pesa kwa kuuza vitoto. Kwa uzao wa kwanza nguruwe mzuri huzaa watoto 8-12 kwa bei ya Tshs elfu 50 unaweza ingiza laki 4 na zaidi. Mungu akupe nini?

Cha msingi lazima uchague mbegu nzuri inayokua kwa haraka na yenye umbo kubwa. Bei ya nguruwe mkubwa wa miezi 8 - 12 huanzia laki 3 na kuendelea, kutegemea uzito wake. Muhimu ni kujipanga kwenye tiba na chakula.
 
Back
Top Bottom