Ufumbuzi wa kelele nyumba za ibada

Ufumbuzi wa kelele nyumba za ibada

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Baadhi ya nyumba za ibada huhusishwa na kero ya kelele kwa majirani. Huu hapa ni ufumbuzi:

1. Kila jengo la ibada lenye vipaza sauti vifunguliwe kwa manufaa ya walio ndani ya majengo tu.
2. Majengo ya ibada wanaweza kusababisha kelele wapendavyo, lakini watumie udhibiti wa kelele zisifike nje ya majengo yao.
3. Kengele na Adhana za kuita watu ibadani zisichukue zaidi ya muda fulani kama ilivyo kawaida.
4. Viongozi wa dini zote wasaini voluntarily "Code of Conduct" yenye kuahidi kuzingatia suala la udhibiti wa kelele.
5. Serikali iandae mwongozo wa kugredi nyumba za ibada kulingana na ukubwa wa kelele (decibels) zinazofika nje ya mipaka ya nyumba hizo za ibada, kwa kuzingatia "Code of Conduct" tajwa hapo juu.

Matokeo yake, ndani ya nyumba za ibada patakuwa na kelele kadiri waaminio wanavyotaka, pasi na kuleta kero kwa majirani wasiohusika.
 
Wazo zuri naunga mikono yote miwili pia mimi ni mkristo ila kelele zimezidi. Kuna Ibada mmoja ilifanyika muda si mrefu na watu kama 20 walikufa wakati ibada hiyo inaendelea na mpaka leo mimi (sijui wewe) sijasikia lolote la maana kuhusiana na ajali hiyo unategemea makelele tu yawe ya kanisa au msikiti ndio yatawastua unaowalenga kufikisha ujumbe huo wakusikie. Yangu macho na masikio
 
Utakapobanwa ndipo utakapojua unapiga kelele kukera watu au unapiga kelele za kulia kuomba msaada.
 
Wazo zuri naunga mikono yote miwili pia mimi ni mkristo ila kelele zimezidi. Kuna Ibada mmoja ilifanyika muda si mrefu na watu kama 20 walikufa wakati ibada hiyo inaendelea na mpaka leo mimi (sijui wewe) sijasikia lolote la maana kuhusiana na ajali hiyo unategemea makelele tu yawe ya kanisa au msikiti ndio yatawastua unaowalenga kufikisha ujumbe huo wakusikie. Yangu macho na masikio
Baadhi yetu tunaamini kile tunachokiamini ni kizuri mno, kiasi kwamba lazima tukifikishe kwa wengine hata kama hawataki, watatushukuru baadaye... Jambo ambalo linaondosha hata maana ya neno lenyewe.

Mungu alikuwa na uwezo wa kutupiga kabali tumuabudu tutake tusitake, lakini katuachia utashi wa kuamua kumuabudu au la. Kwa hiyo si sahihi kulazimisha wasioko ibadani kushiriki ibada kwa kuwafungulia maspika ambayo wazi walengwa ni walio nje ya majengo husika.
 
Hii tabia inakera sana, Sasa sijui wanaweka vipaza sauti kwaajiri ya nin.. wajirekebishe kuna watu wengine ni wazee au wagonjwa wanaishi karibu na ayo majengo, mtu mwingine amechoka anahitaji kupumzika lakin fujo tu.. na aya mambo yapo afrika tu sijui tunaipaza saut kubwa uhisi Mungu ndio usikia kwa haraka
 
Nimefuatilia kwa muda mrefu swala hili kinachowanyima wengi usingizi na judhani sababu ni kelele za nyumba za ibada ni misongo ya mawazo na maisha magumu kama mtu yupo bar analala fofofo licha ya makelele na mziki mkubwa sembuse ukiwa nyumbani

Wewe unadhani mtu kulala fofofo sehemu yoyote ndio hana msongo wa mawazo? Umepotoka. Umeshajiuliza juu ya watu wenye matatizo ya kupata usingizi? Wagonjwa? Wazee? Watoto wachanga?

Nchi hii tunahitaji kiongozi atakayeweza kukemea na kuweka sheria juu ya mambo fulani fulani bila kuogopa kunyimwa kura na watu aliowagusa.

Kuna baadhi ya nchi haya mambo hayapo na watu wako responsible kwenda katika nyumba zao za ibada kuabudu bila kuitwa itwa. Kelele za ma Bar, vigodoro, na za watu wa dini sio afya kwa sababu ni mojawapo ya Pollution.

Juzi nimelala, imefika saa kumi alfajiri kwa mbaali nasikia kispika kinaimba kwaya, kimeimba weee mara mtu akaanza mahubiri na inavyoonekana alikuwa anahubiri sehemu ya wazi, na wala hakuwa na watu anapiga tu makelele pekeyake, hiki kama sio kichaa ninini?

Nani amemwambia kila mtu anajisikia kusikia hayo makelele? Makanisa ya kilokole ndio yamezidi huu upuuzi. Acheni kelele kuweni wastaarabu, mara mia muombe kuhubiri nyumba kwa nyumba kama mashahidi, ili anayewafungulia kwake awe ameridhika na ujio wenu, na asiyeridhika hatafungua nyumba yake, acheni kelele, ustaarabu ni kitu cha bure.
 
Hoja inaungwa mkono, nyumba za ibada zinapaswa kuwa nje ya makazi ya watu, na vipaza sauti au speaker ziwe ni kwa ajili ya walioenda kwenye huduma ya kiroho. Hii ya kupigia watu kelele au kuwatisha watu asubuhi haina maana.
 
Baadhi ya nyumba za ibada huhusishwa na kero ya kelele kwa majirani. Huu hapa ni ufumbuzi:

1. Kila jengo la ibada lenye vipaza sauti vifunguliwe kwa manufaa ya walio ndani ya majengo tu.
2. Majengo ya ibada wanaweza kusababisha kelele wapendavyo, lakini watumie udhibiti wa kelele zisifike nje ya majengo yao.
3. Kengele na Adhana za kuita watu ibadani zisichukue zaidi ya muda fulani kama ilivyo kawaida.
4. Viongozi wa dini zote wasaini voluntarily "Code of Conduct" yenye kuahidi kuzingatia suala la udhibiti wa kelele.
5. Serikali iandae mwongozo wa kugredi nyumba za ibada kulingana na ukubwa wa kelele (decibels) zinazofika nje ya mipaka ya nyumba hizo za ibada, kwa kuzingatia "Code of Conduct" tajwa hapo juu.

Matokeo yake, ndani ya nyumba za ibada patakuwa na kelele kadiri waaminio wanavyotaka, pasi na kuleta kero kwa majirani wasiohusika.
Chief unganeni kama mtaa, muiteni Mtaalamu wa Mipango Miji(Ofisi ya Mkurugenzi) aje awasaidie kutafsiri kibali Cha kufungua Kanisa eneo hilo. Na Kama matumizi ya Ardhi yamezingatiwa!?

Kama anacho kibali kwa mujibu wa matumizi ila hamkushirikishwa kwa maana ya mkutano wa wananchi kuridhia kupitisha maombi hayo.. hiyo forgery na mnaweza kuipinga na itafutwa.

Kama Hana kibali mnaruhusiwa kabisa kuomba msaada wa Halmashauri kufunga mpaka atakapo pata kibali.

Sasa ikiwa atarudi kuomba kubadili matumizi kupitia Serikali ya Mtaa, mnaruhusiwa kuweka pingamizi na hoja zenu zikawekwa bayana mezani..Kama hawezi kuzitimiza ili afanye kazi zake bila kuwabugudhi Basi itabidi aende mahala pengine.

Sheria zipo na ziko waazi kabisa shida ni wananchi wengi hatuzifahamu na Wala hatuzitumii.

Naunga Mkono hoja.
 
NENO LITAWAFUATA HUKOHUKO
Sawasawa basi nikurudishe nyuma wakati teknolojia ya vipaza sauti haijabuniwa kabisa.,
NENO LITAWAFUATA HUKOHUKO
Ha ha - Pole sana kwa taarifa yako hazisaidii kitu .Waanzilishi wa hizo dini hawakutumia vipaza sauti na walifanikiwa sana kuwaelimisha watu. Kelele hazimfanyi mtu kuelimika kwenye mada yeyote iwe siasa , dini mziki n.k.
 
Mleta mada umeshapumzika ila uzi bado unaishi. Duh maisha haya.
 
Ukitaka kupanga sehemu inabidi uulizie JIOGRAFIA ya eneo...kelele zimekuwa kama MASHINDANO!!!!
 
Binadamu wanalalamikia sauti nyumba za ibada lakini za mabaa hawazilalamikii.

Anyway, mwandika uzi alishakufa
 
Back
Top Bottom