Ufundi, fundi na garage

Besar

Member
Joined
Oct 30, 2016
Posts
16
Reaction score
7
Habari za humu ndani waungwana. Huwa nafurahi sana na mada za humu ndani. Leo nina mada kuhusu mafundi na garage tunazopeleka magari yetu kwa matengenezo.
Nimemiliki gari moja(rav4) kwa miaka 4 mpaka sasa. Katika safari zangu garage huwa kuna kitu kinakera mara kwa mara nimeona niombe msaada kufaham labda tatizo liko wapi.

Nimekutana na baadhi ya mafundi wanaokuwa na haraka ya kuhukumu tatizo kabla ya kudadisi na kuchunguza vya kutosha. Mfano, gari linagota breki inapokanyangwa kwenye foleni. Mwendo zaidi ya hapo tatizo halisikiki na wala haigoti kwenye bump wala mashimo. Fundi anashauri kubadili shock-absober, link zote mbili na stabilizer bush mbili. Sikubaliani naye kwa ailimia 80.
Sio mara ya kwanza ishu kama hii imenitokea ama nimeshuhudia gari limeenda garage kwa tatizo A, fundi kasema ni B na akatibu B kwa gharama kubwa kesho yake tatizo lipo pale-pale. Na kwa vile hamna warrant ya kazi kwa maamndishi, ndo bas tena nahesabia nimefanya maboresho hata kama sio lengo kwa mda ule.

Jambo hili silipendi na sijajua kama ni mimi mbishi sana, ni gari mbovu kupindukia, fundi, ama garage ninakoenda ni wapigaji ama unakuaje.
Unakuta umetumia hela ndefu na mda kurekebisha mambo ambayo sio na tatizo bado lipo palepale.
Sijajua yananikuta mimi tu ama wapo wengine.

(Mimi mbishi kiasi chake, sikubali hata siku moja kunywa dawa ya maleria kama naumwa meno, hata kwa bakora sinywi mpaka daktari aeleze uhusiano wa meno na maleria.)
Asanteni, naomba maoni yenu na mchango kwa tatizo la breki kwa sasa.
 
Hilo ni moja mkuu, pili ni gereji nyingi hazina mfumo/utaratibu maalumu wa kufanya service ya magari. Mathalani, manual za magari mengi zinashauri ufanye service ya namna gani kwa km kadhaa. Service ya gari iliyotembea km 5000 haipaswi kuwa sawa na gari iliyotembea km15000.

Sasa hawa wataalamu wetu, kama unafanya service kila baada ya km 3500, basi we ukipeleka ni Airfilter, Oilfilter, Engine oil, Brake adjustments, ATF baaaasi haijalishi ni km3500 zipi!!! Wakifanya Zaidi ni kwasababu umepeleka gari ikiwa na tatizo
 
Hapo kweli mkuu, shukran, kama nikijaliwa tutatafuta uvumbuzi kwa tatizo la utaratibu wa service coz naamini ukosefu wa utaratibu maalum kunachangia gharama za matengenezo na ubovu wa gari.

,
 
Tatizo la breki kugota 'ku!' lilisababishwa na break pad moja (mpya) ya ndani kutokaa sawasawa kwenye bracket yake na caliper. Ilikuwa inalika upande wa chini so contact haikuwa nzuri. Ni tatizo gumu kutambua nimeliona mitandaoni na wateja wengi waliishia kubadilisha baadhi ya vitu. Kwangu mimi nimerudishia pad ya zamani, ila nashuku brand itakuwa sio ya uhakika sana. So tatizo sorted!
Asanteni.

 
Pole,inategemea,both sides inaweza kuwa problem,
Kwa fundi...kama ana haraka au anatumia uzoefu ndio wanakuwaga wanatoa majibu ya kubahatisha,vilevile kama mteja ana haraka au na yeye anajifanya fundi then hapo fundi anaamua kutoa defect ilimradi,lakini hiyo ni beyond professional.
Mi ni fundi,ila sometime inanichukua zaidi ya mwezi kulikagua gari lakini nikitoa defect ujue ni ya uhakika.
Maana mafundi wanakumbatia kazi nyingi kushinda uwezo na mwisho wa siku kama hana task management nzuri anaishia kubahatisha.
 
Kuusu service inatokana na gari inafanya kazi mazingira yap ya kawaida au magumu na sevirze za kawaida ni kama vile engine oil,oil filter,fuel filter,greasing,teminal,gear box oil and differencial oil pia check breka pad and lining

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaelewa brake kugotaa hapa nieleze kwa lugha nyingine ili nikupe mchango wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo fundi anaye mnunulisha mteja shock-ups kwa tatizo la brake ni muuaji.
Brake kugota inategemeana kwanza kuna swala la
*Brake pads
*brake lines zinavujisha
*master cylinder imechoka
*wheel cylinder zina shida
*Power brake booster(Hii inahitaji vimaelezo kidogo) nikipata mda nita share
*calipers zinavujisha
*Valve zinazo balance hydraulic system zimekufa
**Anti-lock brake systems (ABS) hii nayo iki malfunction huleta matatizo kwenye mfumo wa brake lakini kwa mtindo wa kipekee...Hii husaidia gari kusimama hapo hapo ila kuseleleka ukipiga brake yako.
Wakali wa donta tunaita hii kitu Nta!
* mafuta ya brake hayapo yakutosha hivyo system kuingia upepo na kusababisha air bubbles ndani ya system.
Na kama unavyojua brake fluid inasifa ya kutokua compressed ,hivyo upepo ukiingia directly inapoteza hiyo sifa.
upepo unaweza kuwa compressed hivyo husababisha brake pedal kua kama sponge na brake system kupoteza ubora kisha hilo tatizo la kugota ndipo hujitokeza.
*Mwisho aina ya brake fluid unayotumia...
DOT-3 ndio recommended fluid na manufactures wengi wa magari mfano Toyota,Mistubishi etc
DOT-3 pia ndio brake fluid ambayo imekidhi vigezo vilivyo wekwa na Department of Transportation (DOT) duniani.
DOT-3 imekua designed kuhimili kutokutanuka wakati wa baridi na kuchemka wakati wa joto kali.
Brake fluid inayo kua na sifa opposite na nilizo taja hapa husababisha kugota kwa brake.

Machache hayahusiani na tatizo lako ila yatakusaidia wapi pa kuangalia brake zikikuzingua tena.
 
Sijaelewa brake kugotaa hapa nieleze kwa lugha nyingine ili nikupe mchango wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app


yaani inakuwa kama vile kuna nyundo inagonga maramoja tu ukikanyaga breki. Yaani mwanzo wa kupunguza mwendo wa gari, ndo umeamua sasa inabidi nipunguze mwendo, haswa kwenye foleni ambapo gari halina kasi, utasikia 'ku!' upande wa mbele. Huu mlio unakuwa kama vile stabilizer bush inayochoka huwa inagonga.
 
g

asante mkuu kwa somo safi sana.
 

Nakubaliana nawewe kabisa, kama fundi ama mtaalam halafu mteja anajifanya fundi ama mjuaji, huwa haileti picha nzuri sana. Wapo wateja hawana idea hata kidogo na huwa ni usumbufu tu. Upande wa pili wapo mafundi hawajiamini ama wababaishaji, yaani hataki kusikia historia ama matengenezo ya awali ili kuelewa tatizo kwa kina, hivyo alichohisi yeye ndicho hicho hicho.
Nimekutana na mafundi kama vile wanatafuta kazi ya ziada, mara hii imechoka, hii ya kubadilisha, kumbe imebadilishwa ndani ya mwezi mmoja. Pale fundi anapoteza maksi na kumpoteza mteja.
Kama professional, nadhani kuwa msikivu, kuwa open kwa idea tofauti haswa pale unapokuwa huna uhakika na ishu ni muhimu, utajifunza. Pia kujua umsikilize mteja mpaka wapi na akihoji umwelezee kiasi gani na kwa lugha gani.
 
Vizuri sana Bw. Besar
Pole sana kw masaibu yaliokupata kw huyo msanii. Ulivyonena hapo, udadisi mbovu au ukosefu wake ndio chanzo cha hii shida.
Udadisi sio jambo rahisi tunavyochukilia. Sanaa hii uhitaji ujuzi/uelewa mzuri na wa ndani wa chombo au mfumo unaodadisi; uzoefu na ufahamu wa misingi, sheria na maadili ya kisayansi; maendeleo na mabadiliko ya uundaji magari/mitambo; utumizi na uelewa wa mifumo ya udadisi (diagnostic machine) na lingine la muhimu na msingi ni mda.
Magari na mashine huwa ni mkusanyiko wa mifumo mingi, na mifumo yenyewe ni mkusanyiko wa vyuma na sehemu mbalimbali ili kutenda kazi maalum. Mkusanyiko - mfumo, huzingatia sheria za sayansi kw. mfn. Piston katika cylinder utenda kazi yake ya kutembea pale kwa sababu Panapokua na mlipuko, hewa au gesi uongeza nafasi ya ujazo kwa sababu ya kuichukua ile kawi(Energy) inayotoka kwa mlipuko. Bila shaka wenzetu walio gobea kwa kemia wanaelewa na wanaweza eleza tukio hili viuri zaidi. Hapo basi ile pistoni ambayo ni kama mfuniko utembezwa na ule msukumo wa hewa. Kutoelewa misingi na sheria za sayansi ni kizuizi kikubwa kabisa kisichoweza kupitika ili kufaulu kwenye zoezi la udadisi.
Watengeza magari na mifumo waweza kutumia njia tofauti kutekeleza jambo flani katika muundo wao kwa sababu mingi kama vile kuokoa hela, kuboresha mfumo au pia kua tofauti. Mercedes Benz wamegobea katika matumizi ya mskumo/mvuto wa hewa katika kutekeleza mambo tofauti kwenye gari kama loki za milango, kuzima engine za diesel na pia katika ubadili gear kwa gearbox automatic zisizotumia umeme; wengineo hutumia umeme au mikono(levers) kutekeleza shughuli hizi.
Kila muunda chombo ndie anayekielewa kwa kina ingawa kuna wakati wataalam wa nje hua na uelewa zaidi wa chombo katika mazingira; bila shaka haya ni mambo mawili tofauti. Katika ulimwengu wa sasa unaotumia mifumo ya computer, muunda kifaa hua na lugha/kifaa maalum cha kuwasiliana na mifumo yake ili kuidadisi. Ni muhimu sana kutumia mifumo hii kwa kua hiyo ndio uwasiliana vikamilifu na chombo, vingine havipiti sebuleni. Ni kama kujaribu kuwasiliana na mChina bila kujua kiChina, pale kuna kaz.
Lingine ni MDA, bila shaka ili ni swala linalojieleza. Matatizo mengi ya mifumo hasa engine ujitokeza baada ya matumizi mfumo unapopasha. Hivyo basi ni muhimu fundi kuelewa yanayotendeka ili kufikia pale, njia ya pekee ni kuangalia utendaji(observe). Pale ndipo mtaalamu anapoweza kuona yanayotendeka na kupata suluhu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee hii kitu inanikuta mida hii, nimeenda kuchek ABS inawaka muda wote, naona limekuja swala la oil ya gearbox while ABS inahusiana na brake system. Mafundi wa Dar bana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Somo murua kweli kweli... nina shida binafsi na gari langu, naruhusiwa kuja PM??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…