Habari za humu ndani waungwana. Huwa nafurahi sana na mada za humu ndani. Leo nina mada kuhusu mafundi na garage tunazopeleka magari yetu kwa matengenezo.
Nimemiliki gari moja(rav4) kwa miaka 4 mpaka sasa. Katika safari zangu garage huwa kuna kitu kinakera mara kwa mara nimeona niombe msaada kufaham labda tatizo liko wapi.
Nimekutana na baadhi ya mafundi wanaokuwa na haraka ya kuhukumu tatizo kabla ya kudadisi na kuchunguza vya kutosha. Mfano, gari linagota breki inapokanyangwa kwenye foleni. Mwendo zaidi ya hapo tatizo halisikiki na wala haigoti kwenye bump wala mashimo. Fundi anashauri kubadili shock-absober, link zote mbili na stabilizer bush mbili. Sikubaliani naye kwa ailimia 80.
Sio mara ya kwanza ishu kama hii imenitokea ama nimeshuhudia gari limeenda garage kwa tatizo A, fundi kasema ni B na akatibu B kwa gharama kubwa kesho yake tatizo lipo pale-pale. Na kwa vile hamna warrant ya kazi kwa maamndishi, ndo bas tena nahesabia nimefanya maboresho hata kama sio lengo kwa mda ule.
Jambo hili silipendi na sijajua kama ni mimi mbishi sana, ni gari mbovu kupindukia, fundi, ama garage ninakoenda ni wapigaji ama unakuaje.
Unakuta umetumia hela ndefu na mda kurekebisha mambo ambayo sio na tatizo bado lipo palepale.
Sijajua yananikuta mimi tu ama wapo wengine.
(Mimi mbishi kiasi chake, sikubali hata siku moja kunywa dawa ya maleria kama naumwa meno, hata kwa bakora sinywi mpaka daktari aeleze uhusiano wa meno na maleria.)
Asanteni, naomba maoni yenu na mchango kwa tatizo la breki kwa sasa.