Ufundi wa Lwandamina, Pluijm, Niyonzima, kikwazo cha ubingwa Msimbazi

Ufundi wa Lwandamina, Pluijm, Niyonzima, kikwazo cha ubingwa Msimbazi

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kumekuwa na mategemeo makubwa sana kwa hawa ndugu zetu 'Mikia' ya kuwa wanaweza kuchukua Ubingwa.

Lakini kuna vikwazo vikuu 3 ambavyo wanapaswa wavivuke kwa namna yeyote. Kushindwa kuvivuka hivi vikwazo ndio njia pekee ya wanaJangwani kuvishwa Ubingwa kwa mara ya 3 mfululizo.

Lwandamina:

Nimejaribu kuiangalia mechi ya leo na kufanikiwa kugundua kuwa licha ya kuwa kwenye muendelezo wa Ligi, kocha anaonekana bado anatafuta kuijenga team. Anaonekana ni aina ya kocha ambaye ana filosofia ambayo anataka kuitumbukiza klabuni. Najua kadiri mechi zinavyosonga filosofia yake itakuwa katika damu za wachezaji. Hivyo kufanya kuwa vigumu zaidi kwa timu pinzani kupata ushinda hata ushindi wa sare.

Njia pekee ya kukiruka kikwazo hiki ni kuushawishi uongozi wa Yanga na Mashabiki wote kuwa Lwandamina sio kocha bali ni mfuga kuku kutoka Zambia


2. Hans van DePluijm:

Mkurugenzi huyu wa ufundi..... anakuwa mwiba mchungu sana kwa klabu ambazo zina mikakati ya ziada. Nadhani kuonekana kwake pale uwanjani akirekodi baadhi ya matukio na mapungufu kunaipa team msaada wa ziada kujua wapi wanakosea na wapi wako sawa.. na wapi pa kufanyia marekebisho.... Bila kujali mwl lwandamina ameona au haja ona.

Njia pekee ya kuvuka kikwazo hiki ni kuhakikosha HvPliujm hatazami mechi yeyote ile ya LigiKuu

Je nyinyi wenzetu mnae kama huyu?

3. Niyonzima H. H

Najua mnajiuliza kwanini huyu ameingia hapa.
Ufundi wa huyu Kijana akiwa uwanjani unafanya na unakupa sababu nzuri ya kuamini kuwa team ya Yanga SC itatwaa ubingwa msimu huu 2016/17. Kijana Niyonzima anafanya mambo ambayo bila shaka hakuna mchezaji aliyewahi kutokea hapa VPL aliwahi kuyafanya.
Uwepo wa huyu Jamaa kiwanjani ni chachu kuu ya ushindi.

Ili ufanikiwe kuharibu kikwazo hiki hakikisha si tu unamshawishi Lwandamina bali pia Hans Pliujm kwamba jamaa asicheze na nafasi yake ichukiliwe na mwingine.
 
Uwezo wako wa kufikiria ndo umefika mwisho kwan wakati mnafungwa na Jku niyonzima .Lwanda - AMINA na huyo mfuga kitambi hawakuwepo???
 
Maisha ni popote mbona yule mchezaji wa Ghana Gyan Asamoah aliondoka England na kwenda arabuni
Jamaa anadhani kila mtu ana ndoto za kucheza EPL.....
 
Niyonzima angekuwa yuko poa asingezeekea VPL. Ni hayo tu!!

Mbona PELE alizeekea kwao!

Inamaana hakukuwa na EPL, LaLiga, Serie A au Bundesliga kipindi yupo kwenye form?

Niyonzima ameshinda vingi akiwa Yanga SC kuliko mchezaji yeyote yule wa Simba SC aliyepata ichezea Simba SC kwa muda mrefu.... [emoji23]
 
Hebu pitia rekodi za mechi kati ya yanga na jkt alafu ndio uje kujaza server!
 
Hebu pitia rekodi za mechi kati ya yanga na jkt alafu ndio uje kujaza server!
Unamaanisha nini mkuu?

Sio kwamba nashindwa kuleta rekodi za Yanga dhidi ya JKT ruvu tangu 2011...

Ila nataka kujua hoja yako inataka nini zaidi.
 
Back
Top Bottom