Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Kweli Macho Mdiliko!Kuna tofauti yoyote kimaisha unayoiona toka mwaka 2005 hadi 2010?A very fair question.
Hakuna! Watanzania wanazidi kuwa hohehahe bin dhoofu!! Vibaka na machangu wanazidi kuongezeka. Watu wamekata tamaa ya kufanya kazi kwani wachapakazi hawana maendeleo na mafisadi wanapeta!!
 
nipo mitaa ya crdb lumumba

umati wa wana chadema unapita kwa miguu ukielekea jagwani, unapita makao makuu ya ccm
du jangwani patatosha kweli leo
 
ndugu muendelee kutujuza kinachoendelea huko kwani wengine hatutabahatika kuhudhuria au kuangalia tv
 
samahani sijaelewa uhusiano wa ndege za jeshi na kampeni, ni nini hii?
 
Leo wenyewe CHADEMA hawapo siunajua wanategemea internet ya maofisini kwao na leo si siku ya kazi na hawana internet majumbani mwao. Tuwasubiri j3 wajewakutukaneeeeeee kwani kwao ustarabu ni zero.

Kama ulikua huna chakuchangia ungenyamaza!!:focus:
 
Dubo:inawezekana,hakuna anayejua ila Tanzania kwanza na uhalisi wa mambo uwepo wazi.Kuendesha nchi ni jambo nyeti jamani!!
 
Nimeisoma ilani ya Chadema na mwanzoni kabisa nimeanza kuona tatizo lile lile ambalo Chadema wanasema wanapingana nalo.Longolongo na kutoweka jambo wazi kwa mapana yake.Sehemu iliyoanza kunipa mashaka kabla hata sijafika mbali ni hii:

Ufisadi ni nini?

Tunapozungumzia Ufisadi tunazungumzia mfumo na muundo wa utawala ambao umetengeneza utamaduni wa kuishi kiujanja ujanja, matumizi mabaya ya madaraka na vyeo, ufujaji wa mali ya umma, wizi wa fedha za umma, utaratibu wa kubebana na ajira zinazotegemea kujuana, na mahusiano ya watawala na watawaliwa ambayo msingi wake ni woga, vitisho, na kujiona watu wanastahili zaidi kuliko wengine. Ni mfumo uliodidimiza tawala mbalimbali duniani na ambao pasipo kuushughulikia kwa makusudi unasimama kama tishio lilopo na la hatari kwa Tanzania kuliko vita. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema kuwa "ufisadi na rushwa ni adui mkubwa zaidi wa maslahi ya wananchi wakati wa amani kuliko vita" (Bungeni, Mei 17, 1960, kikao cha 35 cha bajeti).

Ufisadi ndio kizuizi kikubwa cha kuboresha maisha ya watu wetu; ni kikwazo kikubwa katika kujenga na kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria na haki za raia. Ufisadi ndio kikwazo kikubwa kabisa cha maendeleo ya nchi. Ndio kusema, juhudi zetu za kujiletea maendeleo kama nchi haziwezi kufanikiwa bila kwanza kukomesha ufisadi.

Tumekuwa na miaka takribani 50 ya CCM. Wameahidi kila aina ya ahadi na wamefanya kila makosa, lakini tukawavumilia na tukawapa nafasi nyingine tukiamini kwamba mambo yatabadilika. Kila tulipowapa nafasi, hali ilizidi kuwa mbaya, tukasogea kutoka kubaya kwenda kubaya zaidi. Lengo lao kubwa limekuwa ni kushinda uchaguzi, ili waendelee kutumia madaraka tunayowapa kwa ajili ya kujinufaisha kwa njia ya ufisadi.

Ni wakati wa mabadiliko, na fursa ya kufanya mabadiliko ni huu uchaguzi wa 2010 na siyo 2015. Tukisubiri wakati mwingine tutakuwa tumechelewa sana. Na tukiwapa nafasi nyingine moja CCM ya kututawala tena tutakuwa tumewapa leseni ya kuendelea kutawala wapendavyo na tutakuwa tumejihukumu sisi wenyewe na uzao wetu katika maisha ya umaskini wa kudumu.
Katika sehemu hiyo ni wazi kuwa Chadema wanataka umma uamini kwamba matatizo yote tuliyo nayo yanatoka na utawala!

Wanataka tuamini hata wale watu wanaotumia vyandarua kufugia kuku badala ya kujikinga na malaria kuwa ni tatizo la watawala.

Wanataka tuamini kuwa serikali inawafuatilia wakwepa kodi sugu kuwa ni unyanyasaji simply kwa sababu JK kapita mahali basi hata kama TRA walitaka kudai kodi basi wasidai tena.

Wanataka tuamini hata kushindwa kwetu kuweka akiba na kujaa kwenye sehemu za starehe siku za kazi,kuchangia mambo ya burudani zaidi kuliko elimu na maendeleo yote hayo kuwa ni tatizo la serikali!!!!!

Ilani haisemi kwamba hakuna chama kinachoweza kuwaondolea watu umasikini kwa asilimia mia. Natumaini Chadema watajipanga zaidi miaka ijayo kuelezea wananchi kwamba elimu ya kujitambua binafsi ni muhimu sana kabla ya lolote.On top of that Chadema inasema kwamba 2010 ndo wakati muafaka!!!

What are the justifications kwa hili??U mean 2010 ndo Chadema imeona nchi inaporomoka au ni ile "I wana be the boss too"!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Acha kupotosha maneno yaliyoandikwa hapo!!Wewe unajaribu kutengeneza maana unayoitaka wewe ili kuonyesha ubaya usiokuwepo.
Hamna sehemu waliyosema utawala ndo chanzo pekee, zaidi wamesema ufisadi ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu na kwasababu UTAWALA wetu wa sasa ni sawa na UFISADI hivyo utawala ndio chanzo kikuu.

Swala la wanaotumia chandarua kuffugia kuku, ndio ni tatizo la utawala(UFISADI) unaoongeza umasikini kila kukicha!Hao watu wangekua na uwezo wakutengeneza banda la kuku hicho chandarua kingetumika saa ngapi??
 
nipo mitaa ya crdb lumumba

umati wa wana chadema unapita kwa miguu ukielekea jagwani, unapita makao makuu ya ccm
du jangwani patatosha kweli leo

Semilong nadhani utakuwa ni miongoni mwao, utujuze mkuu sio umati tu bali na point ambazo Muheshimiwa Raisi atakuwa anaziongea
 
Nimepita maeneo hayo kwa basi kutokea Magomeni hadi Msimbazi -- na baadaye kwa basi jingine kuelekea Temeke. Majira ya saa 6 hivi nilipitia Jangwani na niliona matayarishi ya kuridhisha na umati mkubwa wa watu wakianza kukusanyika. Sijakutana na basi lolote lililokuwa linabeba wafuasi kuwapeleka mkutanoni, lakini pengine yapo.

Nilipofika Msimbazi --karibu na kituo cha basi kilichopo karibu na kituo cha mafuta cha Big Bon, nilichukua basi la Temeke na tulipoondoka tukakutana na msafara mkubwa wa Chadema ukitokea round about kuelekea Fire kuelekea mkutanoni. Watu wa rika mbali mbali hasa vijana wengi wakishika bendera na picha za Dr Slaa wakpuliza mavuvuzela na kuimba huku wakishindikizwa na askari polisi walisababisha foleni kubwa. Wimbo mmoja nilikuwa nausikia na wao kuitikizana unasema: "mafisadi kaeni chonjo, tumempata kommando, CCM mtajibeba" or something like that. Ilichukuwa basi letu takriban dak 40 kufika round about ya Uhuru St.

MMoja ndani ya basi alishikwa na kiwewe na kuitikia nao, lakini aliwauliza -- mmejiandikisha lakini? Nilimuona Marando na gwanda lake la kombati akiwa kati kati ya maandamano -- bila shaka kulikuwapo viongozi wengine ambao sikuweza kuwaona.

Nimepanga baadaye kuhudhuria mkutano huo mimi mwenyewe na jioni Mungu akipenda nitawaarifu kwa muhtasari yale muhimu yaliyojiri.
 
Mtujuze Kinacho/kilicho jiri jaman mlioko Daslam,wengine tuko mikoani jaman
 
ahsante wakubwa kwa kutujuza, japo bado taarifa hazijawa kamili, watu wa maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto, Mbezi, Tabata, Buguruni, Sinza, ubungo, mtupe shamrashamra za kutosha.
 
LIVE: Hivi sasa TBC1 inarusha matangazo ya moja kwa moja kutoka viwanja vya Jangwani hapa Dar, yakionesha uzinduzi wa kampeni ya CHADEMA.

Kampeni imezinduliwa kwa sala, ambapo mtoto wa Sheikh Yahaya Hussein, Hassan Yahaya Hussein ametoa dua kwa Kiislam naye Grace Shellukindo maombi kwa Kikristo.

Sasa baadhi ya wagombea na viongozi wa CHADEMA wanaongea. Kwa kweli kuna umati mkubwa sana wa watu wa rika mbali mbali, wengi wao wakiwa watu wazima, watoto ni wachache.

Waliosema TBC1 inawapendelea CCM sasa mkae mkao wa kula. TBC1 ni chombo cha UMMA, hakina ubavu wa kupendelea upande wowote ule wa chama cha siasa, kwa kuwa inaendeshwa kwa kodi za Watanzania, walio na wasio wanachama wa vyama vya siasa.

-> Mwana wa Haki

P.S. Dhana ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya inachambuliwa....
 
Kampeni imezinduliwa kwa sala, ambapo mtoto wa Sheikh Yahaya Hussein, Hassan Yahaya Hussein ametoa dua kwa Kiislam naye Grace Shellukindo maombi kwa Kikristo.
Duh...! Ahsante kwa taarifa mkuu
 
Back
Top Bottom