Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Very contradictory!!!Naamini watanzania wana macho na masikio.Kama wapinzani ni wa dizaini hii,CCM itakuwepo for lots of years to come.

Uko sawa kabisa ndugu, mf sasa hivi kikwazo kikubwa cha CHADEMA ni wapinzani zaidi kuliko hata CCM yenyewe, sbb mi sion kwa nini hawajaunganisdha nguvu kum-support Slaa amabaye anaonekana anakubalika. Matokeo yake ni kwamba wanataka kura zigawanyike kusudi CCM ishinde. Vyama pinzani hapa Tanzania ni viwili tu CHADEMA na CUF ile ya Zanzibar (CUF ya bara ni mamluki tu hawana kitu). Inanishangaza sana unakuta watu waelewa kama akina Mvungi lakini eti wako TLP, unajiuliza maswali mawili unakaa kimya, ...sijui kama ni kweli!
 
Unauhakika Tanzania hakuna Tatizo la uchumu? Dr. Slaa ni kilaza ndio maana mpaka akumbushwe ndio afanye kitu.

Mkuu hata mimi nakubaliana na wewe 100% kuwa Dr. Slaa ni kilaza na kuthibitisha hilo inabidi Dr. Kikwete asimame na Slaa kwenye mdahalo ili tulithibitishe hilo, au wewe unaonaje?
 
Mkuu nilikuwepo kwenye mkutano, Ruge alitajwa mara moja tu tena na msanii wa bongo flava alipokuwa anatoa risala. Dr. Slaa aliongea zaidi mambo makuu 9 yaliyomo kwenye manifesto ya uchaguzi, mojawapo ni kubadili katiba ambayo wananchi hawafahamu kuwa ina uhusiano moja kwa moja na mustakabi wa maisha yao, kwa mfano kiongozi wa Takukuru atawajibika kwa bunge na sio kwa raisi ili rais akiiba aweze kukamatwa pia.

Pia alizungumzia kuwa maendeleo ya tertiary industries ambayo yanaignite uchumi wa nchi ndio kipaumbele na raslimali nyingi tunazo. Pia aliongea kuhusu mapato ya serikali karibu asilimia 75 yanatumika kuendesha serikali ambapo si vema.

Mkuu wa mkoa mmoja anatembea akiwa na zahanati ikiwa ni thamani ya shangingi lake. Na akasema CHADEMA watafanya nini badala yake.

Dr. Slaa is, in my book, a master of content, a master detail. No wonder Kikwete hawezi kusimama nae kwenye mdahalo!!
 

Ulichoandika ni tafsiri yako kwa vile tayari una udini ndani mwako. Unatakiwa uondoe 'prejudices' kwanza ili uweze kutoa hoja inayojitosheleza na siyo tafsiri yako. Kwani vyama ambavyo kiongozi ni mwislamu wakimchagua mkristo ni danganyatoto pia au ni kwa Chadema tu?
 

Kumbe tatizo lako ni kuwa wazanzibari hawakupewa nafasi wanayostahili! Wakati kuna wenye madigirii kibao amechaguliwa asiye na elimu ya juu! Lakini hao marais wenu wa Zanzibar wana au walikuwa na elimu gani ya kutisha? Wewe kama unaona hawa jamaa Chadema ni wadini na wenye haki ya kuvaa kanzu ni CUF peke yao, basi wanyeme kura yako! Wale ambao wanajali zaidi integrity kuliko kijikaratasi ( hasa ukizingatia vyengi ni vya kununua) watawapa kura zao!

Amandla.........
 

Nafikiri wanaongelea kukumbushwa pale walipokuwa wakimgusa Slaa na kumnog'woneza, na hii ilikuwa ni ktk kumtaarifu juu ya muda na mkwara wa tbc1 kutaka kukatiza matangazo, sasa kwa mtu asiyeweza fikiria mbali kwake yeye hiyo ni kumkumbusha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…