Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Lilith anayetajwa kwenye maandiko hayo kama mwanamke kiburi na mwenye nguvu, na ambaye pia inasemekana alizaliwa sawa na Adam, aliasi na kutengana na Adam baada ya kushindana tabia.

Mkuu hii ni hadithi ya kufikirika tu, kwanza kumbuka Adamu hakuzaliwa bali aliumbwa kutoka kwenye udongo. Kama MUNGU alimuumba huyo Lilith kabla ya Eva, basi ingeandikwa kwenye Biblia wala isingefichwa.

Biblia inasema KWELI na wala haidanganyi. Kilichoandikwa kwenye Biblia ni kweli tupu. Shetani anapenda sana uongo na ndiyo maana amekuwa akija na hadithi nyingi za kutunga za uongo kama hii ya kwako ili awapotoshe Wanadamu wauamini uongo kuliko KWELI ya NENO la MUNGU.
 
Nakiri kukosea hapo kwenye nyekundu nilitaka kumaanisha kuumbwa...
 
shukrani kwa hii elimu, ngoja nami nitafute zaidi kuhusu huyu Lilith!
 
Hizi hadithi zenu za watu wanaopenda kuijazia BIBILIA na KUONA haijitoshelezi ....ukifuatilia kwa Makini mambo haya Yaliibuka karne ya 19 na nyuma yake Hapa kuwa na hizi story KABISA.

Kwahyo Ndugu hizi story Ni Uongo ...SHETANI atabaki kuwa Roho ilieasi sheria ya MUNGU na kupinga
 
LAANA ni kitu gan mkuu
 
Kitabu gani kimeandika hii kitu ya lol lilith??.. Na sisi tukipitie.....

Nachofahamu Adam alikua first man, na alikua first man sababu alikua mmoja wa Malaika MBINGUNI aliyeongoza mapambano Kati ya lucifer na Mungu kule MBINGUNI tunaiita (Pre-mortal) life... Award yake akapewa aje Duniani aanzishe mankind...... Sasa huyu lilith hata kwenye Pre-mortal life hakuwepo.

Tunajua waliokua kwenye Maisha kabla Dunia haijaumbwa ambao walikua mashuhuri kule kwa kazi zao. Baadhi Yao ni

JESUS CHRIST - JEHOVAH
MICHAEL - ADAM
GABRIEL - NOAH
LUCIFER - SATAN/DEVIL

Na wengine wengi.

Jina la kushoto ni Pre-mortal name, jina la kulia ni Mortal (earth) name.. Mfano YESU KRISTO kwenye pre earth alikua anaitwa JEHOVAH.

Sasa huyu lilith hatujui alikua Nani kule na aliletwa kwa mission gani Dunian maana Adam, eve na wengine walioanzisha Dunia kama viumbe wa kwanza walikua wana kazi ya kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…