Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Bila ya mfarakano na talaka kwa Lilith wanaume tungekuwa tunabeba mimba
 
Mkuu hii ni hadithi ya kufikirika tu, kwanza kumbuka Adamu hakuzaliwa bali aliumbwa kutoka kwenye udongo. Kama MUNGU alimuumba huyo Lilith kabla ya Eva, basi ingeandikwa kwenye Biblia wala isingefichwa.

Biblia inasema KWELI na wala haidanganyi. Kilichoandikwa kwenye Biblia ni kweli tupu. Shetani anapenda sana uongo na ndiyo maana amekuwa akija na hadithi nyingi za kutunga za uongo kama hii ya kwako ili awapotoshe Wanadamu wauamini uongo kuliko KWELI ya NENO la MUNGU.
KAMA MUNGU ALIMUUMBA ADAM,BASI KUNA UWEZEKANO NAE MUNGU ALIUMBWA JE ALIUMBWA NA NANI?
 
Mkuu labda nimsaidie Mshana Jr kujibu hili..... Ni kweli Adam na Lilith walikuwa na nguvu sawa actually zaidi hata ya malaika ila Adam aliondolewa nguvu hizi za kiungu pale alipokula tunda ila unachosahau ni kwamba lilith aliondoka bila kula hilo tunda actually mambo ya tunda yalikuja baada ya Hawa kuletwa kuziba pengo la lilith.... Hivyo Lilith aliondoka na nguvu zake kama ambavyo shetani aliondoka na nguvu zake alipotolewa mbinguni... Ila Adam nguvu zake ziliisha siku anakula tunda hicho muhim tutambue


Lilith hakula tunda mkuu hivyo ile hukumu ya Adamu ya kwamba atakufa ni ya Adam na hawa pekee ndio maana shetani yeye mpka leo yupo hai na lilith pia sababu wao bado walibaki na nguvu zao za siku zote ila kama Mungu angetamka kuwa wote waliomfanya adam afanye dhambi wafe basi lilith na shetani wangeshakufa kitambo sana kma adam na hawa.

Kama hilo ni dogo kwanni usishangae Yesu aliyekuja kuleta wokovu aliishi miaka 33 pekee hapa duniani ila aliyepinga wokovu toka Yesu wa hapa duniani amekufa yeye bado anaishi milele na anazidi kupotosha watu?? Ukipata jibu la hapo ndio utaelewa kwanni Mungu hakumhukumu lucifer/ lilith kifo siku ile Adam ameasi kwa kula tunda.

Ni hayo tu
Iz hadithi za kulazia watoto wa wazungu usingizini...TUWATAFUTE WANAOTUCHEZEA AKILI.
 
Mwanzo 1:26-28
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; WAKATAWALE samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba MTU kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, MWANAUME na MWANAMKE ALIWAUMBA.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.




Biblia inafikirisha sana Aisee ALIWAUMBA inamaana walikuwa ni wawili na si mmoja

Ukisoma vizuri utaona inakwambia BAADA YA KUWAUMBA AKAWAPA JINA ADAMU......

hivyo haikuwa imetanabaishwa jina ni la nani kati yao(tulifichwa makusudi)
ADAMU AKAMZAA SETH(wale wawili wakazaa mtoto aliitwa Seth)


Biblia ina mengi sana ila ukweli ni kuwa Lilith alikuwa mke wa Adamu na wakapata mtoto kabla ya kuja kuwapo Eva
Ukisoma vizuri utaona walikuwapo kabla ya huyo shetani kuja duniani na katika uumbwaji wao Lucifer alikuwa pembeni ya Mungu kabla na baada ya uumbwaji wa Adamu

Ref:NA TUUMBE MTU KWA MFANO WETU(Mungu hawezi kujiambia mwenyewe neno Tu...hivyo walikuwa wapo wengi katika kikao cha uumbaji huo ila mambo yariharibika baada ya Lucifer kuja na kumpeleka Lilith kuzimu,Mungu nae akampa Adamu mbadala wake kutoka katika nyama zake si Mavumbini kama wale Adamu wa kwanza waliotoka mavumbini)

Biblia haisomwi kama Gazeti jaman
Licha ya bibilia kutosomwa kama gazeti ni mkitabu Fulani wa uongouongo sana.
 
Mkuu hii ni hadithi ya kufikirika tu, kwanza kumbuka Adamu hakuzaliwa bali aliumbwa kutoka kwenye udongo. Kama MUNGU alimuumba huyo Lilith kabla ya Eva, basi ingeandikwa kwenye Biblia wala isingefichwa.

Biblia inasema KWELI na wala haidanganyi. Kilichoandikwa kwenye Biblia ni kweli tupu. Shetani anapenda sana uongo na ndiyo maana amekuwa akija na hadithi nyingi za kutunga za uongo kama hii ya kwako ili awapotoshe Wanadamu wauamini uongo kuliko KWELI ya NENO la MUNGU.
Unauhakika upi kama haisemi Uongo au haijaacha kitu kwa sababu bibilia imeandikwa na watu
 
Kitabu gani kimeandika hii kitu ya lol lilith??.. Na sisi tukipitie.....

Nachofahamu Adam alikua first man, na alikua first man sababu alikua mmoja wa Malaika MBINGUNI aliyeongoza mapambano Kati ya lucifer na Mungu kule MBINGUNI tunaiita (Pre-mortal) life... Award yake akapewa aje Duniani aanzishe mankind...... Sasa huyu lilith hata kwenye Pre-mortal life hakuwepo.

Tunajua waliokua kwenye Maisha kabla Dunia haijaumbwa ambao walikua mashuhuri kule kwa kazi zao. Baadhi Yao ni

JESUS CHRIST - JEHOVAH
MICHAEL - ADAM
GABRIEL - NOAH
LUCIFER - SATAN/DEVIL

Na wengine wengi.

Jina la kushoto ni Pre-mortal name, jina la kulia ni Mortal (earth) name.. Mfano YESU KRISTO kwenye pre earth alikua anaitwa JEHOVAH.

Sasa huyu lilith hatujui alikua Nani kule na aliletwa kwa mission gani Dunian maana Adam, eve na wengine walioanzisha Dunia kama viumbe wa kwanza walikua wana kazi ya kufanya.
Yehovah ni neno LA kiebrania lenye maana mungu kwa kiswahili
 
shukrani mshana.
kwa wale mnopinga kwa kutumia "biblia" kile
wasichokijua wengi ni kuwa biblia alitengenezwa na kanisa, kulikua na rundo la vitabu vilivyo andikwa na watu mbali mbali kwa kipindi cha miaka mingi, watu kama wewe na mimi walikaa na kukubaliana vitabu vipi wachukue viunde mkosanyiko wa vitabu atakao tumika na kanisa na ndipo biblia alipozaliwa, walifanya kazi nzuri ya kui promote . hivyo kuna vitabu vingi sana vilivyo achwa na kuna vingine vimeongezwa miaka mingi baadae, kama wewe unadhani biblia ilitoka mbinguni basi rudi shule kadai ada yako maana uliibiwa
Mkuu vipi ile bibilia ya Barnaba
 
Kuna jamaa alitoa historia Fulani ya chanzo cha binadamu mkabeza cmkumbuki ila ntamfuta yule ana nondo haswa hivi vingine ni hadithi tu za kusemekana.
Asante kwa kushiriki na kuchangia mjadala
 
Nakumbuka ulishawahi kuleta mada kuhusu nyoka kufanya ngono na hawa lakini tunafumbwa kuwa walikula tunda

Na hii ya leo inashabihiana na ile

Nimefungua akaunti mpya ili kujibu kwa uwazi na uhalisia kuhusu hili
Mimi nimeolewa na nina watoto watatu nimewahi kusaliti katika ndoa yangu kwa sababu ya malumbano na mume wangu

Mtu wa kwanza kusaliti nae ni mwaka juzi mwishoni na kabla hata sijasaliti niliota nyoka mkubwa sana kaingia ndani na kumng'ata mume wangu nikafika kumuokoa baada ya wiki mbili kwa mara ya kwanza nikasaliti ndoa yangu
Siku zikapita nikaachana nae huyo mtu

Wa pili kabla sijasaliti nae niliota hivyohivyo pia nyoka akinikimbiza na kunichapa kwa mkia wake

Wa tatu mume ndie aliota aking'atwa na nyoka

Najizuia kuacha lakini kuna shida ktk ndoa yangu kupambana na hisia za kimwili napo ni ngumu

Sasa basi kuna uwezekano mkubwa pale eden tunda lililoliwa ni ngono kati ya nyoka na eva tunafumbwa tu

KWAHERINI
Dah pole sana lakini huo ndio uhalisia tunda la mti wa kati ni ngono...! Full stop! Tunajaribu tu kuvunga lakini hata via vya uzazi viko katikati ya mwili kiuhalisia
 
Nilikuwa nina mwananamke anaitwa LILY,nilimpenda sana lakini alichokuja kunifanyia,mungu ndio anajua,naunga mkono hoja ya Mshana Jr kuwa huyo lilith ndio ibilisi shetani aliyefitinisha ndoa ya adam na eve....
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Back
Top Bottom