Mkuu labda nimsaidie
Mshana Jr kujibu hili..... Ni kweli Adam na Lilith walikuwa na nguvu sawa actually zaidi hata ya malaika ila Adam aliondolewa nguvu hizi za kiungu pale alipokula tunda ila unachosahau ni kwamba lilith aliondoka bila kula hilo tunda actually mambo ya tunda yalikuja baada ya Hawa kuletwa kuziba pengo la lilith.... Hivyo Lilith aliondoka na nguvu zake kama ambavyo shetani aliondoka na nguvu zake alipotolewa mbinguni... Ila Adam nguvu zake ziliisha siku anakula tunda hicho muhim tutambue
Lilith hakula tunda mkuu hivyo ile hukumu ya Adamu ya kwamba atakufa ni ya Adam na hawa pekee ndio maana shetani yeye mpka leo yupo hai na lilith pia sababu wao bado walibaki na nguvu zao za siku zote ila kama Mungu angetamka kuwa wote waliomfanya adam afanye dhambi wafe basi lilith na shetani wangeshakufa kitambo sana kma adam na hawa.
Kama hilo ni dogo kwanni usishangae Yesu aliyekuja kuleta wokovu aliishi miaka 33 pekee hapa duniani ila aliyepinga wokovu toka Yesu wa hapa duniani amekufa yeye bado anaishi milele na anazidi kupotosha watu?? Ukipata jibu la hapo ndio utaelewa kwanni Mungu hakumhukumu lucifer/ lilith kifo siku ile Adam ameasi kwa kula tunda.
Ni hayo tu
Mshana na Zitto hii hoja ya Adam na lilith zen hawa ukitumia biblia kama source huipati tuanzie pale mwanzo 1:26 Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; (hapa wanazungumzia mtu wakwanza) wakatawale samaki wa baharini na ......(hapa wanazunguzia couple nyingine/ama more than one peron ambayo itukiijumlisha na yule wa kwanza tunapata pengine watu wa 3 ama zaidi)
mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, (hapa mtu wa kwanza anaumbwa) kwa mfano wa Mungu alimuumba, (bado tunamzunguzia yule wa kwanza) mwanaume na mwanamke aliwaumba. (couple inaumbwa)
mpaka hapo tuna watu wa3 tofauti mwanaume peke yake zen mwanaume na mwanamke kuanzia mwanzo 1:28 Mungu anawamilikisha wale watu watatu/wote dunia anawapa utawala.
Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya aridhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.(namna yule wakwanza alivyoumbwa ama huyu ni mwanaume wa 3, japo sitaki kuamini hivyo)
Mwanzo 2:15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya edeni, ailime na kuitunza. 2:16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu akisema "matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, (yule mtu wa kwanza ndie tunamzungumzia hapa achana na ile couple kumbuka mpaka hapo yuko peke yake hajapata kampani/mwenzi)
Mwanzo 2.18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye(wazo au mpango wa kumtengenezea mke/mwanamke wawe couple pia linazaliwa)
Mwanzo 2: 21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake , 22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. (mwanamke wa pili anaumbwa now we have 2 women with 2 or 3 men)
Baada ya hayo yote nashawishika kuamini kua hakuna mwanamke alie muacha walieumbwa nae, na yale maelezo yote ni ufafanuzi tu wa namna hawa wawili walivyopatikana, pengine sasa tuseme ile couple ya kwanza ndio iliyokuja kudanganya hii couple ya pili ambayo hii nayo inakuja kuwa hoja tofauti kabisa na hii yako ya lilith. na ikiwa lilith ni mmoja kati ya ile couple ya kwanza je mumewe yuko wapi au alienda wapi? usiniambie ni huyu shetani/lusifa sababu yeye tunaambiwa aliumbwa kwa moto tena kabla ya dunia kuuumbwa