Tunaterejea tena kutazama yale mambo yaliyoacha utata na pengine hayajawahi kujadiliwa na wengi.
Tumeshajadiliana sana kuhudu Eden, Hawa, tunda la mti wa kati(mti wa ujuzi wa mema na mabaya), nyoka na Adam. Katika vyote hivi kuna mtu pia tumemjadili kwa kiasi, mtu huyu hata maandiko hayamtaji wala kumjadili sana. Mtu huyo ni Lilith, mwanamke anayesemekana kuwa mke wa kwanza wa Adam.
Jambo hili la Adam kuwa na mke aliyeitwa Lilith halitajwi kwenye misahafu yetu hii tunayoijua bali kwenye maandiko mengine lakini ya kiimani pia.
Lilith anayetajwa kwenye maandiko hayo kama mwanamke kiburi na mwenye nguvu, na ambaye pia inasemekana alizaliwa sawa na Adam, aliasi na kutengana na Adam baada ya kushindana tabia. Lilith alitaka kuwa na mamlaka makubwa kwa Adam.
Habari za Lilith zinaishia pale alipoachana na Adam, kisha Adam alirejea Eden kuanza maisha ya upweke akiwa kama mtalikiwa na tunaambiwa Lilith alikuja kugeuka kuwa kiumbe cha kuzimu.
Maisha ya upweke Eden yanamfanya Mungu kumtengenezea Adam msaidizi wa kufanana naye
ndipo Adam sasa anamshukuru Mungu kwa kusema. Sasa huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu ....?(wanazuoni wanatafsiri kauli hii kama kwamba mwanzoni alikuwepo mwingine ambaye hakutokana na Adam! )Je mtu huyo ni Lilith?
Maisha mapya ya furaha upendo na mapatano ndani ya Eden kati ya Adam na Eva/Hawa yanamvuta nyoka anayetajwa kama ibilisi akijulikana kama malaika aliyeasi mbinguni (Lilith?) Huyu ndio pekee aliyejua siri ya uumbaji (ukiacha Mungu) na siri ya tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya!
Kwa hakika Lilith hakupenda kabisa kuona Adam akiwa na mwanamke mwingine na hilo liko wazi hata kwa kizazi cha leo. Ule usemi wa wanawake hawapendani asili yake ni huku. Lilith kwa uwezo alionao anavaa umbo la nyoka na kumlaghai Eva/Hawa ale tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mti ambao Adam alizuiwa kula matunda yake.
Bibie Eve/Hawa bila kujua nia ovu ya nyoka anakubali kula tunda la mti wa kati ambalo aliliona ni TAMU na linapendeza kwa macho! Kilichofuatia baada ya hapo kinajulikana wazi. Nyoka akawafitinisha Adam na mkewe Hawa kwa Mungu. Wakafumbuliwa macho yaonayo na kujiona wako uchi.
Nyoka akalaaniwa kuwa atatembea kwa tumbo
Eva akalaaniwa kuwa atazaa kwa uchungu
Adam akalaaniwa kuwa atakula kwa jasho na wote wakafukuzwa Eden palipokuwa na kila kitu cha bure.
Lengo la Lilith la kulipa kisasi likawa limetimia na kwa mtazamo huo inawezekana kabisa Lilith ndio ibilisi....!!!