Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Hakuwa Malaya. Alitaka haki ya kuwa sawa na Adam kwa sababu wote wametengenezwa kwa udongo. Aliona hakuna sababu ya yeye kuwa chini alafu Adam awe juu.
Adam waliumbwa pamoja na lilith, ba baadae lilith akakorofishana na adam sababu ya umalaya, na tabia mbaya. Ndo akafukuzwa eden. Mungu akatoa ubavu kwa adam

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kufuatalia tunakuja kujua kuwa binadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa Adam na lilith na baadae kuja hawa ?

Kwa anaefaham kuhuc historia hii tubadilishane mitazamo

Hata mimi nimesoma mahala. Na pia katika biblia za mwanzo zinaonyesha/Kuandika kwamba Mungu alifanya uumbaji wa awamu mbili. Aliumba Mtu mume na mke, alafu baadae kupitia yule mtu mwanaume akamuumba mwanamke kwa kutumia ubavu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
kwahiyo lilith kama ni ibilisi basi ni zao la wivu. kwa maana hiyo wivu ni kitu kibaya sana.
 
Habari za Lilith hazijaandikwa popote kwenye Biblia takatifu, na huko zilikoandikwa si kwa wema bali kwa ubaya ukiachilia satanism na atheism.

kumbe upigaji na kula kimasihara imeanza siku nyingi...

kweli nimeamini hamna jipya chini ya jua...
 
kumbe hawa alikuwa na mke mwenza....halafu siku hizi wanajifanya hawataki na kusema ni dhambi na kumbe hizi mambo tangu zama zile..wanawake mtuache jamani...ukiwenza hata bibi hawa yalimsibu...so mtupunzishe ati..
 
tatizo vitabu hivi vitakatibu vimehaririwa mno ..mpaka uhalisia umepotea sasa...kuna mambo mengi yamefichwa na hayajulikani kabisa..

kuna machapisho ni siri kubwa mno..na hakuna anayeruhusiwa kuyajua zaidi ya wale viongozi wakubwa wa dini.
 
Ukianza kusoma hizi habari utaanza kupata ham ya kujua zaidi, ukitaka kujua zaidi ndipo hatari ilipo sasa. Katika maisha kuna vitu ukivifahamu vinaweza kuharibu maisha yako au kukupoteza kabisa, the less u know the better
 
tatizo vitabu hivi vitakatibu vimehaririwa mno ..mpaka uhalisia umepotea sasa...kuna mambo mengi yamefichwa na hayajulikani kabisa..

kuna machapisho ni siri kubwa mno..na hakuna anayeruhusiwa kuyajua zaidi ya wale viongozi wakubwa wa dini.
Ukianza kusoma hizi habari utaanza kupata ham ya kujua zaidi, ukitaka kujua zaidi ndipo hatari ilipo sasa. Katika maisha kuna vitu ukivifahamu vinaweza kuharibu maisha yako au kukupoteza kabisa, the less u know the better
Kuna vitu inabidi ujifunze na kuvijua ukiwa huegemei upande wa kiimani la sivyo utapotea mazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam. Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam.

Kuna simulizi nyingi nje ya Biblia zinazokinzana na nyingine kushabihiana kumhusu mwanamama huyu Lakini zote zinakubaliana katika jambo moja kuwa Lilith alimwacha Adam kwakuwa hakutaka kuwa chini ya amri za mwanaume. Hakutaka kuongozwa wala kutawaliwa na mwanaume kwa utetezi kwamba, wote waliumbwa siku moja na kwa malighafi zinazofanana. Hivyo hakuna mkubwa kuliko mwingine.

Sasa asili ya Lilith ni nini!? ni wapi?

Lilith anaonekana mara nyingi kwenye Biblia ya Kiebrania na huko anajulikana kama malkia wa usiku, pepo katili la usiku lenye tamaa kubwa ya ngono... Huku kazi yake kubwa ikiwa ni kuiba watoto gizani usiku. Lilith sio jina jema popote zaidi ya kwenye imani za kipagani na kishetani.

Asili ya Lilith inatajwa sana kwenye simulizi za Wayahudi (c 700-1000). Hapa anatajwa kama mke wa kwanza wa Adam waliyeumbwa pamoja (mwanzo 1:27, kisha akafuatia mke wa pili wa Adam baada ya Lilith kuondoka (mwanzo 2:22). Hapa inasemekana Lilith alimuacha Adam kwenye bustani ya Eden na hakutaka kurudi huko na kwenda kugawa kipochi manyoya kwa malaika muasi aliyeitwa Samael. Lakini pia simulizi nyingine zinasema aliondoka na kwenda kungonoka na shetani ili kuendeleza kizazi na uzao wa shetani.

Hii inaweza kuleta uhalisia kidogo kutokana na vile satanism wanavyomchukulia Lilith, kumuamini na kumwabudu kama mungu mwanamke, mke wa baba yao shetani.

Hizi zote ni simulizi nje ya Biblia takatifu lakini kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba kuna hicho kiumbe chenye jinsia ya kike kiitwacho Lilith ambacho hakuna popote kinatajwa kwq wema. Kuna mahali anaelezewa kama mchawi, pepo aliyengonoka na shetani kwa makusudi mazima ya kuendeleza kizazi chao kama tulivyoona hapo juu.


Ibada za kutoa kafara katika satanism

Tunaterejea tena kutazama yale mambo yaliyoacha utata na pengine hayajawahi kujadiliwa na wengi.

Tumeshajadiliana sana kuhudu Eden, Hawa, tunda la mti wa kati(mti wa ujuzi wa mema na mabaya), nyoka na Adam. Katika vyote hivi kuna mtu pia tumemjadili kwa kiasi, mtu huyu hata maandiko hayamtaji wala kumjadili sana. Mtu huyo ni Lilith, mwanamke anayesemekana kuwa mke wa kwanza wa Adam.

Jambo hili la Adam kuwa na mke aliyeitwa Lilith halitajwi kwenye misahafu yetu hii tunayoijua bali kwenye maandiko mengine lakini ya kiimani pia.

Lilith anayetajwa kwenye maandiko hayo kama mwanamke kiburi na mwenye nguvu, na ambaye pia inasemekana alizaliwa sawa na Adam, aliasi na kutengana na Adam baada ya kushindana tabia. Lilith alitaka kuwa na mamlaka makubwa kwa Adam.

Habari za Lilith zinaishia pale alipoachana na Adam, kisha Adam alirejea Eden kuanza maisha ya upweke akiwa kama mtalikiwa na tunaambiwa Lilith alikuja kugeuka kuwa kiumbe cha kuzimu.

Maisha ya upweke Eden yanamfanya Mungu kumtengenezea Adam msaidizi wa kufanana naye
ndipo Adam sasa anamshukuru Mungu kwa kusema. Sasa huyu ni nyama katika nyama zangu na mfupa katika mifupa yangu? (Wanazuoni wanatafsiri kauli hii kama kwamba mwanzoni alikuwepo mwingine ambaye hakutokana na Adam! ) Je, mtu huyo ni Lilith?

Maisha mapya ya furaha upendo na mapatano ndani ya Eden kati ya Adam na Eva/Hawa yanamvuta nyoka anayetajwa kama ibilisi akijulikana kama malaika aliyeasi mbinguni (Lilith?) Huyu ndio pekee aliyejua siri ya uumbaji (ukiacha Mungu) na siri ya tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya!

Kwa hakika Lilith hakupenda kabisa kuona Adam akiwa na mwanamke mwingine na hilo liko wazi hata kwa kizazi cha leo. Ule usemi wa wanawake hawapendani asili yake ni huku. Lilith kwa uwezo alionao anavaa umbo la nyoka na kumlaghai Eva/Hawa ale tunda la mti wa kati; mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mti ambao Adam alizuiwa kula matunda yake.

Bibie Eve/Hawa bila kujua nia ovu ya nyoka anakubali kula tunda la mti wa kati ambalo aliliona ni TAMU na linapendeza kwa macho! Kilichofuatia baada ya hapo kinajulikana wazi. Nyoka akawafitinisha Adam na mkewe Hawa kwa Mungu. Wakafumbuliwa macho yaonayo na kujiona wako uchi.

Nyoka akalaaniwa kuwa atatembea kwa tumbo. Eva akalaaniwa kuwa atazaa kwa uchungu.

Adam akalaaniwa kuwa atakula kwa jasho na wote wakafukuzwa Eden palipokuwa na kila kitu cha bure.

Lengo la Lilith la kulipa kisasi likawa limetimia na kwa mtazamo huo inawezekana kabisa Lilith ndio ibilisi!
Mshana jr hii stori ya lilith ni ya kweli nimeifuatilia na kujaribu kupata picha ya nn kilikuwepo nimeona ni kwel sehemu moja ambapo sijapaelewa ni apo kwenye tunda kuna fumbo limefichwa apk ili kukwepa aibu na mm naamin ilo si tunda bali ni sex huyu lilith alienda kumfundisha sex eva na eva nae akaenda kumfundisha adam balaa likaainzia apo na pia mm naamin baada ya eva mungu aliumba mwanamke mwingine au wanawake wengine
 
Chengine nilitaka nikiwasilishe ni hv biblia yetu hii tunayotumia imeandikwa na muingereza ambae yeye alikopi kutoka kwenye vitabu vya kiyahudi na romania ivyo kuna baadh ya vitu hawakuvikopi ili kutengeneza kitabu ambacho kipo portable namaanisha kinachoweza kushikika ndio ikazaliwa biblia lkn ukitafuta biblia za kiibrania za kale ni kubwa mno na habari za lilith zimo humo ila lugha pia ni changamoto hivyo huwez kuelewa
 
Chengine nilitaka nikiwasilishe ni hv biblia yetu hii tunayotumia imeandikwa na muingereza ambae yeye alikopi kutoka kwenye vitabu vya kiyahudi na romania ivyo kuna baadh ya vitu hawakuvikopi ili kutengeneza kitabu ambacho kipo portable namaanisha kinachoweza kushikika ndio ikazaliwa biblia lkn ukitafuta biblia za kiibrania za kale ni kubwa mno na habari za lilith zimo humo ila lugha pia ni changamoto hivyo huwez kuelewa
[emoji120][emoji120][emoji120]Asante sana kwa kutumia muda wako kutafuta ithibati.. Baadhi waliishia tu kupinga bila ushahidi wala kujisumbua kuchimba zaidi

Jr[emoji769]
 
Kwa hiyo Adamu aliumbiwa jini ili amuoe au na yeye alikuwa jini ?
pia mbona adamu alikufa lakini huyo jini yupo hai ?
ila hii story ni kama vile melgibson ndani ya filamu ya yesu.

Move ya yesu ukiaangalia kikirsto/Kiimani utaamini kila kitu na mwisho wake utaishia kulia kwa kuona mateso ya Yesu mwana wa Nazaleti...ila ukiingalia kimtaa mtaaa huku unajiuliza maswali Kwa kila unachokiona unaweza Achana na Mambo ya kuamimini ishu za Dini ukawa unaishi tu kama mababu zetu.
 
Move ya yesu ukiaangalia kikirsto/Kiimani utaamini kila kitu na mwisho wake utaishia kulia kwa kuona mateso ya Yesu mwana wa Nazaleti...ila ukiingalia kimtaa mtaaa huku unajiuliza maswali Kwa kila unachokiona unaweza Achana na Mambo ya kuamimini ishu za Dini ukawa unaishi tu kama mababu zetu.
Thats right ni bora usiwe na dini au ata ukiwa nayo usiamin kila unachoambiwa ni kwa sababu mungu hakuumba dini wala ukabila na kuna siri nying tu kuhusu hii dunia ambazo din nying huwa hawazisemi hii ni kwa sababu ya kuweka maslahi mbele mm ntakuwa wa mwisho kuamini km adam na eva walikula tunda NO i say NO kuna mambo yamefichwa na viongozi wetu wa din ni wavivu hawataki kutafuta ukwel na pia kuhusu tunda la uzima na milele nasema tena halikuwa tunda kuna siri imefichwa na hii ni kwa sababu kuepusha immoral
 
Back
Top Bottom